Aqua
JF-Expert Member
- Jul 23, 2012
- 1,657
- 1,231
Kitu ambacho watu wa dini hawajui ni kwamba "ndani ya kanisa kukiwa na mtu mmoja au wawili wanaotenda dhambi Munguhapendezwi na kanisa hilo".Sasa jinsi watenda dhambi wanapokuwa wengi kanisani hilo kanisa linakuwa ni chukizo kwa Bwana.Ndiyo maana tunashauriwa kutubu mara tu unapogundua umetenda dhambi,na roho wa Bwana atakushuhudia,lakini kama umezoea kuitenda hiyo dhambi Roho huondokaka ndani yako na hapo mtu anakuwa hata akitenda dhambi ndani yake hajisikii hukumu.Kama uko hivyo jua umeshatekwa na shetani na hauko salama,na hata ukiomba unaona kabisa maombi yako ni kama matamshi tu hayaendi kokote.Mrudie Mungu wako leo,muda uliobaki ni mchache,mwenye masikio na asikie.