SIKUBALIANI NA HOJA HII.
Watu mnatiana ujinga sana. Mnalishana sumu sana. Ukisoma maoni ya walio wengi utaona lawama nyingi wanapewa wanawake, maneno ya chuki na kejeli wanapewa wanawake, na wengi wanaotoa maoni wana mtazamo hasi sana juu ya wanawake. Wengi wanaonekana waliumia kwenye mahusiano au wanaendelea kuumia kwenye mahusiano lakini kwa mtazamo wao wanawake ndio chanzo cha matatizo na wao ndio wenye makosa. Wengi wanatoa uzoefu wao binafsi au mifano yao binafsi kama hukumu au hitimisho kwamba wanawake ni wabaya, hii si sahihi. Hebu tujiulize, hivi wanaume hawana makosa kwenye uhusiano? Kwa hiyo shida zote zinazotokea kwenye mahusiano wewe mwanaume huna mchango kwenye shida hizo? Yaani wewe ni malaika na msafi ila mwanamke ndiye siku zote mkosaji? Si kweli! Changamoto kubwa ninayoiona hapa ni wanaume wengi hasa vijana KUKOSA UELEWA NA MAARIFA, kuhusu masuala ya mahusiano na kumwelewa mwanamke. Mahusiano ni sanaa ambayo lazima ujifunze jinsi ya kukabiliana nayo kila siku. Kukosa kwako uelewa na maarifa kusiwe kisingizio kwamba mwanamke ni mtu mbaya. Yaani, huwezi kulaumu gari lenye changamoto za kiufundi kwasababu wewe inakusumbua kuliendesha au hujui jinsi ya kulitengeneza, hapo tatizo si gari, tatizo ni WEWE usiye na maarifa.
Wanawake ni viumbe bora sana kuweza kuwepo hapa duniani, swali ni kwamba UNAWAELEWA? Ndoa ni jambo jema sana kuwahi kutokea hapa duniani, kuna faida nyingi sana raha za kuwa kwenye ndoa, tatizo UNA UELEWA? UNA MAARIFA? Kukosa kwako maarifa na uelewa kuhusu wanawake haimaanishi kwamba wanawake ni wabaya, au uwachukie wanawake, jipe muda JIFUNZE ili uwaelewe na uendelee kufurahia maisha yako wewe na wanawake.
Wanawake wapo, na wataendelea kuwepo, wewe mwanaume huna namna bali ni kuwa mpole jifunze jinsi ya kuishi naye mwanamke na maisha yaendelee.
Kama hamjui ombeni msaada mpate maarifa na uelewa kuhusu wanawake badala ya kulialia tu.