Ukweli mchungu: Kikwete family ni Royal Family watatutawala milele

Ongeza sauti mkuu

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Aisee raisi anayepotezea na kukaa kimya baadhi ya watu wanauwawa na kupotezwa hiyo sikuikubali kabisa
Hakuna unachojua! Wewe unafkiri yeye angesemaje?! Kwani hakuna taasisi maalum zilizoundwa kuchunguza hayo?! Polisi na vyombo vingine vya ulinzi vina kazi gani?!

Ulitaka Rais avae gwanda, ajichore majivu na yeye aingie msituni kuwasaka waliopotea?! Na kwann walipotea?!


Unamjua J.F Kennedy wa Marekani?! Unajua sababu ya kufa kwake?! Msiwe tu mnaongea kwa mihemko... hizi ni elimu pana
 
Mbona sasahivi hayo matukio hayatokei?
 
Hawatorudia ule ujinga
Lakini ujue rohoni kwa mtu ni mbali sana ! Mtu yeyote unayemwamini sana sana siku moja ghafla anaweza akakugeuka mpaka ukashangaa. !! Hiyo huwa ni mipango ya Mungu !! Leo binti ya Rais mstaafu wa Angola yupo kikaangoni alijipatia mamilioni ya dollar isivyo halali kipindi baba yake yupo madarakani. ! Je huyo Wa sasa si aliaminiwa na Rais mstaafu Do Santos kwamba ni mwenzao ?! Au huyo wa sasa ni wa kutoka chama kingine. ?!
 
JK n familia yake hawajawaondolea watu umaskini?. Mleta mada kaandika uchimvi kwenye andiko lake ingawa wenye akili wamemuelewa anamaanisha nini.

JK kapigana mpaka MOI ikajengwa, haijawaletea matibabu mamilioni ya watanzania wanaupata ajali kila kukicha?.

Kapigana mpaka mwendo kasi ukajengwa, haujaleta mabadiliko katika maisha ya wakazi wa Dar?.

Kila rais ukimsikiliza mtanzania wa kawaida wa mtaani hajafanya lolote, ni mwendo ule ule wa malalamiko.
 
Elimu inamuondoaje mtoto wa mkulima, bodaboda, machinga na baamedi toka ktk lindi la umaskini?
Waulize mamilioni ya watanzania waliokuja Dar kufuata elimu miaka ile ya 1980 na leo hii ni mawaziri na wakurugenzi wa mashirika, watakupa majibu ya uhakika zaidi.
 
Kwahiyo issue siyo elimu. Hata ktk utetezi wako hakuna mahala umetaja elimu. Na hapa ndipo kwenye hoja yangu.
Elimu inachangia sana, inakupatia kitu kinachoitwa ushawishi mbele ya jamii. Unakwenda benki unajua umuone nani mambo yake yafanikiwe. Unakwenda wizarani unajua umuone nani mambo yako yanyooke.

Elimu inakupa influence mbele ya jamii, inakupa ujanja wa kufanya biashara ziweze kudumu.

Bill Gates tumeanza kumjua miaka zaidi ya 20 na mpaka leo bado yupo juu kipesa. Bakhresa tumeanza kumjua miaka ya 1980 mwanzoni mpaka leo yupo juu kipesa. Kukaa juu katika chati za matajiri ni matokeo ya ushauri wa wanaowazunguka ambao huwezi kuupata kama huna elimu pana.
 
Yule mzee siasa anazijua sana
Rais waliokuja baada ya Nyerere wamemshinda Nyerere kwa kila kitu; kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi na kwa kuzalisha mafisadi.

Huyu Ridhiwani hafai kabisa. Kumuongezea vyeo vingi kutaleta matatizo katika Law and Order situation ambayo sasa hivi ni tete sana .
Siyo kama vile ana matatizo yoyote. Mambo yake yanaenda vizuri. Sijui kwa nini unamuongezea sifa
 
Mbona sasahivi hayo matukio hayatokei?
Nani amekwambia?!

Wewe unajua kila kinachoendelea Tanzania hii na Afrika mashariki yote?!


Na kwamba wewe unasema hayatokei tetea hoja yako kwann hayatokei?!

Na tetea hoja yako ya mara ya kwanza kwann yalikuwa yanatokea?!
 
Watu wenye asili ya rangi nyeusi tuna shida ya unafiki na uzandiki wa hali ya juu!...

wakumbushe na swala la kujenga shule nyingi sana za Serikali na kurudisha masomo yaliyokuwa yamefutwa miaka mingi iliyopita. Eti mtu kusoma biashara kipindi kile na uwe competent lazima uende Nje... maana hayakuwepo hayo masomo na watu waliyoyakutia hayo masomo vyuoni kama vile IFM na CBE walio wengi walikuwa wanajionea chenga tu na kuishia kulamba mchanga (kufeli vibaya)

je! hawaoni wimbi la wasomi liliongezeka na limeongezeka ingawa majority hawana ajira ila si haba wasomi hewa tunao hata wenye akili za kujitambua kidogo ingawa bado ni majingamajinga sana! Zingatia kwamba:- (kujitambua ni chaguo, wengi hawajachagua kujitambua)

Kikwete huyohuyo baba wa watu ingawa ana mapungufu yake ndo kwenye kipindi chake watu/vijana/watoto wengi walichepuka kuzipata Diploma zao na waliobahatikaga kupata ajira ilikuwa ni kwenye kipindi chake. Ule mfumo wa watu kumaliza kidato cha nne na kwenda zao chuo ulishamiri kipindi chake na wengi walifanikiwa kupata shahada zao. Leo hii wanaiamini ile kauli ya "kufeli kidato cha nne, sio mwisho wa maisha"


Kipindi chake hichohicho watanzania walio wengi hasa wapiga madili (Halali na batili) mambo yaliwaendea vyema na walio wengi walijenga mahekalu na vibanda kwenye kipindi chake.

Watoto wa walalahoi mpaka waliopata division "4" za "30" walienda jeshi na wapo! Leo hii wana ajira, maisha yanasogea na familia zao na bado wako jeshini na wanaujua mchango wake na wanamu-appreciate sana! Sizungumzi kutetea wala siongei kwa mapenzi ya Chama.

Kuzunguka kwake nje nia haikuwa ni kula bata kama wanafki wengi na wasiolewa wanavyosema. Mwenye kuijua Diplomasia na uhusiano wa kimatafa wanaelewa.


Yapo mengimengi alifanya ila wabongo kinachowazuzuaga ni kutaka kimuonekano hapa kuwe kama New-york! Wao ndo wanaona maendeleo πŸ˜…πŸ˜…πŸ™ŒπŸΎ
 
Siyo ukweli mchungu; mchungu kwa nani? Ni ukweli mtamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…