Niwe mkweli tu.
Tangu Lissu alipoanza kumtukana Raisi, kutukana waalimu wake na watu wengine wanaomzidi umri, kielimu na mengineyo nilimkataa sana kuanzia hapo.
Nilimsikia na kumsoma katika taarifa yake flani kwa umma anawavuta na kuwahusisha IGP na DG wa TISS kwenye siasa zake na kuwaamrisha katika kauli zake nikaona huyu hatima ya siasa zake za kulewa sifa atakuja kuharibu maisha yake mazuri ya kisiasa na kazi zake za kisheria siku moja.
Ujasiri wa kuwatukana wale wataalam waliohusika kwenye taarifa ya uchunguzi wa makinikia aliutoa wapi?
Kwamba yeye ni msomi na mahiri sana kuliko wale wote kwenye elimu ya madini, miamba, uchumi, sheria, uhasibu, hisabati na mifumo ya computer?
Lakini mwisho ukweli hujitenga na uongo, hatimae kifo cha Acacia, kuzaliwa kwa Twiga, kulipwa kwa zile fedha za Goodwill, kutoshitakiwa na kufilisiwa serikali huko MIGA alikosema vimekuja kuwa ushahidi yeye hakuwa sahihi na wale wataalamu aliowatusi walikuwa sahihi.
Lissu akiwa raisi wa JMTZ nchi hii itakuwa imepata pigo kubwa sana.
Kwanza Lissu yeye mwenyewe ni dikteta mkubwa sana kwa jinsi alivyo shiriki mchakato wa kuwafukuza akina
Zitto na mchakato wa kumkaribisha Lowassa CDM kisha kumpa nafasi ya kugombea uraisi kupitia CDM.
Lissu alishiriki au alinyamazia siasa chafu za kumchafua mzee wetu Dk. Slaa mwaka 2015.
Lissu siyo mzalendo ni mjivuni , mnafiki na kigeugeu. Lissu siku zote yupo kwa ajili ya self ego feeding.
Ni afadhari nimpe kura yangu Membe au Mbowe au Msigwa kuliko Lissu.