Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Maombi ya kujionesha ni hali ya kuomba au kufanya sala kwa kutaka watu waone, waseme na kusifia. Ni maombi ya mtu anayetafuta heshima ya kidini, sifa au umaarufu wa kijamii kwa kutumia jina la Mungu. Mtu anapotangaza mitandaoni ratiba za maombi yake na kupiga kelele “leo siku ya kwanza ya novena, sala yetu ni very powerful, leo siku ya tatu - tunaomba mfululizo, leo tunahitimisha…” huko ni kujionesha; ni kutaka watu wamwone kuwa ni mtu wa kiroho. Ni sawa kabisa na wanafiki aliowasema Yesu kuwa hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.
Yesu Kristo alisema waziwazi katika Mathayo 6:5:
“Nanyi mnaposali, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.”
Maombi ya kujionesha, yanaishia barabarani na mitandaoni tu, hayafiki mbinguni. Na mtu anayejionesha tayari amepata thawabu yake. Thawabu yake ni pongezi za watu, ‘likes’ ‘positive comments’ na kuonekana mtakatifu machoni pa wanadamu.