Ukweli mchungu: Maombi ya kujionesha, hata kama ni ya siku tisa (Novena), Mungu hayasikii

Ukweli mchungu: Maombi ya kujionesha, hata kama ni ya siku tisa (Novena), Mungu hayasikii

Umeelewa? Maombi ya kujionesha, yenye majivuno na kujitangaza hata kama ni ya muda mrefu, Mungu hayasikii

Maombi anayoyasikia Mungu ni maombi ya faragha, sala inayotoka katika moyo safi na mnyenyekevu, na machozi ya ndani yasiyo na matangazo.

"Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako[sio mtandaoni], funga mlango [hata members wa JF wasijue] na umwombe Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye sirini atakupa thawabu yako." (Mt 6:6)
Walokole huwa mpo kama wehu wakati mwingine
 
Meditation is a true prayer… hata hivyo, wewe kujadili tu hayo maombi ni majibu tayari
 
Soma Mt 28:19-20 ndio utajua ametuambia wapi.

Kama kanisa katoliki lingekuwa hivi walokole wanavyolisimulia, lingeshaanguka mapema sana.

Linaendelea kuwepo, sababu lina kitu ambacho hakuna kanisa lingine lolote linacho.

Focus na imani yako. Pilipili usioila ikianza kukuwasha, ujue una tatizo.

Na hata msemaje, the truth is, hakuna wa kuliangusha. Hata wale waliojipenyeza na kuingia ndani, ili kuliangusha. Wakingiza mambo yao batili, wanaishia kuanguka wenyewe.

By the way, kanisa katoliki lilijua mapema sana juu ya French Revolution na atari zake. Waliposema hawakusikilizwa. Halafu ikawaje?
Hata Tanzania...anayedharau mwiba....
 
Maombi ya kujionesha ni hali ya kuomba au kufanya sala kwa kutaka watu waone, waseme na kusifia. Ni maombi ya mtu anayetafuta heshima ya kidini, sifa au umaarufu wa kijamii kwa kutumia jina la Mungu. Mtu anapotangaza mitandaoni ratiba za maombi yake na kupiga kelele “leo siku ya kwanza ya novena, sala yetu ni very powerful, leo siku ya tatu - tunaomba mfululizo, leo tunahitimisha…” huko ni kujionesha; ni kutaka watu wamwone kuwa ni mtu wa kiroho. Ni sawa kabisa na wanafiki aliowasema Yesu kuwa hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.

Yesu Kristo alisema waziwazi katika Mathayo 6:5:
“Nanyi mnaposali, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.”

Maombi ya kujionesha, yanaishia barabarani na mitandaoni tu, hayafiki mbinguni. Na mtu anayejionesha tayari amepata thawabu yake. Thawabu yake ni pongezi za watu, ‘likes’ ‘positive comments’ na kuonekana mtakatifu machoni pa wanadamu.
Uliwakuta wamesimama wapi wakifanya novena ndugu? Au wanapopeana taarifa na ratiba za ibada wewe ndio unaona ni novena? Hebu jazia nyama hadithi Yako.
 
Uliwakuta wamesimama wapi wakifanya novena ndugu? Au wanapopeana taarifa na ratiba za ibada wewe ndio unaona ni novena? Hebu jazia nyama hadithi Yako.
Sio hadithi. Kuna member mmoja humu aliandika uzi wenye sala ya novena, kisha akaiita sala hiyo kuwa ni "very powerful prayer" kisha akajimwambafy kuwa dini yake ndio mkombozi wa Taifa. Hiyo ni nini kama sio kujionesha na kujivuna?
 
Back
Top Bottom