Ukweli mchungu: Maombi ya kujionesha, hata kama ni ya siku tisa (Novena), Mungu hayasikii

Ukweli mchungu: Maombi ya kujionesha, hata kama ni ya siku tisa (Novena), Mungu hayasikii

Kama hayapokelewi hizo nyumba za ibada ni zanini sasa,! Basi kila mtu aabudu nyumbani kwake tubomoe misikiti na makanisa, mfano maombi ya nchi yatakuwaje ya siri au ufanye maombi na mazimwi yasio onekana? Unajua maana ya jumuiya?

Maombi binafsi.sawa yanaweza kuwa Siri ya mtu.
 
Uelewa wetu wa masula ya kiimani unaongozwa na roho mtakatifu!
Sio utashi!

Usijikweze,utakwezwa!
Mfano mnataka kuombea nchi mtumishi asipotangaza watu watajuane 🤣🤣🤣🤣.


Mapadri hawana familia zao ni waumini sasa wamwambie nani±.
 
leo nakuunga mkuno mkuu,, utawala huu wa hiki chama labda tuanzishe movement za vurugu hizi zingine ni ngumu kutoboa
 
Mahala tumefika, kama dunia sio Tz pekee, watu wamekuwa wabinafsi kupitiliza,hata uhai hauna maana mbele ya "maslahi"...

Bilieve me, wanaotetekeleza haya hawana maisha mazuri hata kidogo, ni vipunje wanarushiwa na wenye mipango ambao ni matajiri wakubwa wa mali na nguvu! ( Vanity) na kwa nguvu zao wanaaminisha watu kwamba ndivo inavopaswa iwe!

Amani ni tunda la haki!
Haki ni msingi wa maisha bora!


America leo kama tunavoona inaenda kushuka kwa sababu ya kuweka maslahi mbele ya haki (Automatically)..na nguvu zake zote, its going down na hakuna anachoweza kufanya, sisi tunaojitafuta tunafuata mikumbo, wachache (A tiny group) wanapanga kimaslahi kuangamiza haki ya watu zaid ya 61m... Hata kukemea tunashindwa!

Tunakemea wanaokemea, Mungu atusaidie!
 
Madaraka ya kulevya kusahau kama kuna viongozi wa dini
 
Maombi ya kujionesha ni hali ya kuomba au kufanya sala kwa kutaka watu waone, waseme na kusifia. Ni maombi ya mtu anayetafuta heshima ya kidini, sifa au umaarufu wa kijamii kwa kutumia jina la Mungu. Mtu anapotangaza mitandaoni ratiba za maombi yake na kupiga kelele “leo siku ya kwanza ya novena, sala yetu ni very powerful, leo siku ya tatu - tunaomba mfululizo, leo tunahitimisha…” huko ni kujionesha; ni kutaka watu wamwone kuwa ni mtu wa kiroho. Ni sawa kabisa na wanafiki aliowasema Yesu kuwa hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.

Yesu Kristo alisema waziwazi katika Mathayo 6:5:
“Nanyi mnaposali, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.”

Maombi ya kujionesha, yanaishia barabarani na mitandaoni tu, hayafiki mbinguni. Na mtu anayejionesha tayari amepata thawabu yake. Thawabu yake ni pongezi za watu, ‘likes’ ‘positive comments’ na kuonekana mtakatifu machoni pa wanadamu.
Ukiwa period na akili nayo inahama?
 
Wewe mwenyewe unatupigiaga makelele huku ili tujue umeokoka, nikuambie tu ukweli, Mungu huwa hana habari kabisa na walokole, ndiyo maana asilimia 99 ya walokole ni masikini na wajinga, ukiacha wale wachache wanaotafuna sadaka za wenzao.
Leo nasimama na mleta mada ila hii comment yako imenifurahisha.
 
Novena dhidi ya mteule wa Mungu Mama Samia haitafanikiwa. Novena ya kisiasa ni kama kumpigia Mungu makelele yasiyo na msingi. Mungu atawaadhibu kwa kupoteza muda kufanya maombi ya kisiasa dhidi ya CCM mkidhani ni novena.
 
Siku ambayo Samia akipokea simu na kuambiwa kuwa mwili wa Abdul umekutwa Ununio nadhani ndio siku ambayo tutaona sura ya huzuni ya kweli ya Mama yenu!

Badala ya kumsaidia awe Rais mzuri nyie mnazidi kumvuruga! Tokea dunia imepata kuumbwa na Mungu hakujawahi kutokea mtu mkamilifu. Mnatengeneza thread na nyuzi ya kumfanya mama yenu ajione ni Serafi ama Makerubi! Wakati akishiba anakwenda chooni, na alivyokuwa Binti alikuwa anaingia Period.

Mnatengeneza theory za kijinga ilihali aonekane ni mtu wa ajabu kuwahi kutokea duniani. Ipo siku mtakuja kusema Samia ni zaidi ya Kina Nyerere! Ipo siku mtasema Samia ndio Rais namba moja duniani tokea serikali zote zimeanza kufanya kazi.
 
Wewe mwenyewe unajionyesha humu kila siku.

Mungu wao na wako ni tofauti, hivyo fanya yako kivyako, nao wafanye yao kivyao.
 
Usihukumu usije kuhukumiwa...

Na after all ni maombi ya kuombea taifa sio mambo binafsi


Lili nafsi yako binti acha kila mtu afanye anachokiamini
 
Kwa wote mnaosali/omba, mkumbuke kuwa kuna mpango wa Mungu (divine plan) na kila jambo/tukio lilishawekwa kwenye mpango huo. Kusali/kuomba jambo hili au lile litokee au lisitokee ni sawa na kumshawishi mungu abadili mpango wake. Dini zinatuchanganya sana wanadamu!
 
Mtumishi,
Big up,
Umejibu vizuri na kwa ushahidi wa kimaandiko. Ila kwa kuwa mleta mada ni chawa lia lia kama akina Tlaatlaah, ataendelea kuleta ligi.

Nimejiuliza tu, kama yeye ameona wenzake wanaomba isivyo sawa, kwanini asiingie mzigoni kuomba kwa usahihi ili uonevu, wizi, ufisadi, utekaji, ufir*ji, mauaji nk, vikome, haki na amani irejee nchini??
Tunawatu wajinga na wapumbavu sana kwa ujumla wake mkuu.
 
Unapotoa hoja zako jitahidi kulinganisha Agano la Kale na Agano Jipya. Katika Agano Jipya, maombi ya kujionesha hayakubaliki.
Kwahiyo Mungu wa agano la kale na Mungu wa agano jipya ni wawili tofauti?
Hivi una akili sawasawa kweli?

Pentekoste – Mitume na wanafunzi wakiwa pamoja

Matendo 1:14: Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali pamoja na wanawake na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.

Matendo 13:1-3: Katika kanisa la Antiokia, walipokuwa wakihudumu na kufunga, Roho Mtakatifu alisema wamtoe Barnaba na Sauli. Wote wakaomba, kufunga, na kuwawekea mikono, kisha wakawatuma.
 
Wakatoliki hupenda maombi ya kujionyesha sana hasa maaskofu wao


Hivyo vifungu ukivyo nukuu ni vya agano la kale .Kuna tofauti kwenye maombi ya agano la kale ni jipya farisayo mkubwa wewe

Kanisa limeanza agano jipya .

Kwenye maombi ya agano jipya Yesu aliagiza yawe sirini sio kupiga tarumbeta mabarabarani na njia panda kuwa ooh tutakuwa na maombi ya Taifa

Huo ni ufarisayo.Mungu hasikilizi maombi ya kifarisayo kwenye agano jipya.Yakiwemo hayo ya kifarisayo ya katoliki na wapuga filimbi wa Hamelini wenzao akina Gwajima nk
Kitabu cha matendo ya mitume kipo kwenye agano katikati au?

Pentekoste – Mitume na wanafunzi wakiwa pamoja

Matendo 1:14: Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali pamoja na wanawake na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.

Matendo 13:1-3: Katika kanisa la Antiokia, walipokuwa wakihudumu na kufunga, Roho Mtakatifu alisema wamtoe Barnaba na Sauli. Wote wakaomba, kufunga, na kuwawekea mikono, kisha wakawatuma.

Yesu alipokuwa anawaombea makutano hiyo ilikuwa ni sirini?

Tatizo lenu walokole ni uelewa hafifu heri wasabato mnaweza kukaa naye mkajifunza kitu na mkaelewana lakini si ninyi mnakalilishwa sana na kuamini ili hali ninyi ndo mnaenda kwenye senta na vipaza sauti mnaanza kupigia watu kelele.

Ninyi ninyi ndo mnaenda stend kuombea watu ovyo ovyo nk.

Yesu alisema utoapo sadaka hata mkono wako wa kushoto usijue kwa mujibu wa andiko hili yesu alimaanisha nini?

Mfano aliutoa yesu kwa mafarisayo ni kama leo hii uwe kwa waislamu hasa unapofika mwezi wa Ramadan.

Yaani ile funga yao hadi bidhaa zinapanda hata ukiwa na muislamu kwako familia yote itajua na hata majirani watajua kwa fln kuna muislamu na amefunga!


Hizi ni baadhi ya sifa za mafarisayo na ndio maana yesu aliwaita wanafiki.

Walikuwa wepesi kuhukumu wengine (Yohana 7:47-49).

Walikuwa wagumu kwa wengine, wakiweka mizigo ya sheria, lakini wao wenyewe hawakuyafuata kwa moyo (Mathayo 23:4).

Walizingatia sana sheria za nje, lakini wakapuuza mambo ya muhimu zaidi kama rehema, haki, na imani (Mathayo 23:23).

Walijiona wenye haki kuliko wengine (Luka 18:9-14: mfano wa Mfarisayo na mtoza ushuru).

Kwa hiyo Mafarisayo walikuwa ni watu wa dini walioonekana wacha Mungu, lakini mara nyingi walionyesha majivuno, unafiki, na kutafuta sifa, badala ya unyenyekevu na utii wa kweli kwa Mungu.


Hayo yesu aliyajua kwa sababu alikuwa Mungu alikuwa nauwezo wa kutambua kilicho ndani ya moyo wa mtu yaani nje na ndani yesu alikuwa anaona maana alikuwa na uwezo huo!

Mara kadhaa aliwaambie wasafishe vikombe kwa ndani kwanza ndipo na nje vitakuwa safi!! Maana wale watu aliwajua nje ndani.

Sasa wewe na mtoa uzi mmewatambuaje kuwa hawa madre na maaskofu ni wanafiki?

Je kama maombi yao Yana maanisha na Mungu akayajibu?

Wewe ni nani hasa hadi utambue kuwa haya maombi hayapokelewi ikiwa tu hata malaika hama Access ya kujua hilo wewe unajuaje?


Mbona Paulo aliwatanganzia waalike watu kwa ajiri ya maombi ya sabato ya pili yake?
 
Back
Top Bottom