Ukweli mchungu: Maombi ya kujionesha, hata kama ni ya siku tisa (Novena), Mungu hayasikii

CCM wapo kwenye hatua za mwisho kuelekea kwenye umauti....na ndio wanatapa tapa.......

Kila saa kuna zuka nyuzi na I'd mpya kumnanga Polepole na wapigania haki wengine!!!!

Karibuni kunakuchwa!!!
20241225_191404.jpg
 
wakatoliki wamemkamia nani, mbona ni kama wanaombea nchi na Uchaguzi
Hahahahaaa!
Mwamba na kitambi chote hicho unategemea ujifiche kwenye mkaranga na usionekane?!!!! Huo ndo ukweli, mioyoni mwenu mumemdhamiria Samia........hilo lipo wazi kabisaaaa!!
 
Ezra 10:1–17

Waisraeli walipogundua dhambi ya kuoa wake wa mataifa, Ezra alilia na kuomba mbele za Mungu.

Taifa lote liliungana naye, wakalia na kuomba.

Waliamua kukaa na kufanya mchakato wa kutubu na kuachana na wake wa kigeni.

Mchakato huu wa toba ya kitaifa na utekelezaji wake ulidumu siku nyingi (kuanzia mwezi wa tisa hadi mwezi wa kwanza – karibu miezi mitatu).
 
Maombi ya kujionesha ni hali ya kuomba au kufanya sala kwa kutaka watu waone, waseme na kusifia. Ni maombi ya mtu anayetafuta heshima ya kidini, sifa au umaarufu wa kijamii kwa kutumia jina la Mungu. Mtu anapotangaza mitandaoni ratiba za maombi yake na kupiga kelele “leo siku ya kwanza ya novena, sala yetu ni very powerful, leo siku ya tatu - tunaomba mfululizo, leo tunahitimisha…” huko ni kujionesha; ni kutaka watu wamwone kuwa ni mtu wa kiroho. Ni sawa kabisa na wanafiki aliowasema Yesu kuwa hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.

Yesu Kristo alisema waziwazi katika Mathayo 6:5:
“Nanyi mnaposali, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu.”

Maombi ya kujionesha, yanaishia barabarani na mitandaoni tu, hayafiki mbinguni. Na mtu anayejionesha tayari amepata thawabu yake. Thawabu yake ni pongezi za watu, ‘likes’ ‘positive comments’ na kuonekana mtakatifu machoni pa wanadamu.
 
Mtoa mada yuko sahihi asilimia zote, maombi yakujitangaza Kwa Mungu hayajibiwi kwa mujibu wa biblia
Soma hapo mkuu

Na Yoeli 2:15–17 – Nabii Yoeli aliagiza tarumbeta ipigwe ili taifa lote liitwe kwa kufunga na kuomba rehema za Mungu.
 
Kumbe, kwa mtazamo huu, hakuna haja ya kuwa na nyumba za ibada, maana ukiingia humo kila mtu anajua unakwenda kufanya nini (hence umejionyesha)..!!
 
Soma hapo mkuu

Ezra 10:1–17

Waisraeli walipogundua dhambi ya kuoa wake wa mataifa, Ezra alilia na kuomba mbele za Mungu.

Taifa lote liliungana naye, wakalia na kuomba.

Waliamua kukaa na kufanya mchakato wa kutubu na kuachana na wake wa kigeni.

Mchakato huu wa toba ya kitaifa na utekelezaji wake ulidumu siku nyingi (kuanzia mwezi wa tisa hadi mwezi wa kwanza – karibu miezi mitatu).

Na Yoeli 2:15–17 – Nabii Yoeli aliagiza tarumbeta ipigwe ili taifa lote liitwe kwa kufunga na kuomba rehema za Mungu.
Ngoja mchungaji setfree aje akufafanulie zaidi, usitoke
 
Kuna sababu gani kila siku kuanzisha nyuzi za mimi ni mtoto wa mfalme kama sio kujionyesha(kama wewe ni mtoto wa mfalme si ungekaa kimya tungeona ufalme wa mzee wako?)

RC wametoa taarifa kwa waumini wao kuhusu novena.Ulitaka hiyo taarifa ifike vipi vigangoni na parokiani au askofu angejifungia jimboni na kuanza novena bila kuwaeleza waumini nini kifanyike?Askofu au mtu yoyote anaweza kufanya hivyo bila kuhabarisha umma lakini hayo yanakuwa maombi binafsi na sio ya wote.
 
Mtoa mada yuko sahihi asilimia zote, maombi yakujitangaza Kwa Mungu hayajibiwi kwa mujibu wa biblia
Mathayo 20:29-34
Yesu alipokuwa anaondoka mjini Yeriko, umati wa watu ulimfuata. Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie!” Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie!” Yesu akasimama, akawaita na kuwauliza, “Mnataka niwafanyie nini?” Wakamjibu, “Bwana, tunaomba macho yetu yafumbuliwe.” Basi, Yesu akawaonea huruma, akawagusa macho yao, na papo hapo wakaweza kuona, wakamfuata.

Swali, hawa vipofu hawakuwa hadharani???
 
Kwa kuwa wewe sio Mungu kaa kimya
Pole sana. Kumbe hujajua hadhi yangu? Mimi ni mwana wa Mungu.
‘Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake’ (Yohana 1:12). Kwakuwa mimi ni mwana wa Mungu, siwezi kukaa kimya. Nina wajibu wa kusema ukweli wa Baba yangu.
 
Back
Top Bottom