Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

umenena ukweli kwa asilimia 80 hata mm huzunguka mikoani sijaona wananchi kumzungumzia mama kwa wema nazani ameasiliwa sana na mtangulizi wake ,mara ya kwanza wengi wanaimani kunamtu anamsaidia sio yy na hili la sasa ndo kabisa inabidi abadili aina ya utendaji[emoji848]
 
Masikini sijui umekusanya wapi hizo data!
Chuki zako binafsi usitujumuishe wote.
Wengine kama watumishi wa Umma tunaamini ujio wa mama ni ukombozi baada ya lile shetani lenu la Chato kututesa
 
Tena aki na mama ndo hawampendi kabisa. Kuna mama mmoja anasikiliza radio one sasa kuna muda wanaweka ujumbe wa Samia Suluhu Hassan utasikia wamama wanakwambia mwenzao "zima kwanza/toatoatoa.../we punguza sauti kwanza/
Wanywe sumu wakafilie mbali.
Samia ndiye Rais hayo mengine hayapunguzi mamlaka yake
 
Na huu ndio ukweli.

Wanaoenda kwenye mikutano wengi wanakusanywa na RCs,DCs,Wabunge n.k tena kwa pesa ndefu.

Mama amekosa mvuto.
Haiondoi ukweli kuwa Samia ndiye Rais wa JMT sio lazima awe na mvuto
 
Tena aki na mama ndo hawampendi kabisa. Kuna mama mmoja anasikiliza radio one sasa kuna muda wanaweka ujumbe wa Samia Suluhu Hassan utasikia wamama wanakwambia mwenzao "zima kwanza/toatoatoa.../we punguza sauti kwanza/
Uko sahihi kabisa. Wamama wengi hawamkubali kabisa huyu Rais. Na hata hoja ya kutopendwa nayo ina ukweli ndani yake.

Maeneo mengi ya vijijini ambako ccm imekuwa ikikusanya kura za bure, kwa sasa hali ni tofauti kabisa. Kuna watu hawataki hata kumsikia, au kumuona kwenye picha. Hii siyo dalili nzuri hata kidogo.

Natamani 2025, angejitoa kwenye mchakato. Ila ndiyo tena. Madaraka yamesha mnogea. Ngoja tuone kitakachotokea.
 
Umetumwa na sukuma gang you cheat yourself,HAKUNA KAMA SAMIAH,JIDANGANYE KIPIMO UTAKIPATA 2025. NI MWENDO WA USHINDI KILA PAHALA,ANAWEZA KUVUNJA REKODI YA WINGI WA KURA.
 
Kwa utafiti Gani ? Mwangalie vizuri sisi wengine tumekufa tumeoza! Wewe ndio humpendi hata hivyo haitakiwi tumpende wote ! Sisi wengine tuna wivu😁
 
kushinda uchaguzi upinzani ni jambo gumu labda katiba ya hii nchi ibadilishwe baazi ya kanuni za uchaguzi zibadilishwe ,Raisi anamchagua msimamizi mkuu wa uchaguzi unategemea nini hapo?wakurugenzi ndo mabosi wa ichaguzi huko chini kabisa unategemea mtu atashinda?labda waamue tu
 
HAKUNA KIPINDI AMBACHO AKINAMAMA WENYE UELEWA WANAFAIDIKA KAMA KIPINDI HIKI MIKOPO IMERAHISISHWA KWELI,LABDA HILO LIMAMA ULILOLIOJI NI LENYE CHUKI YAKE NA MUMEWE LINAIWEKA KWENYE UMMA,ALL BRIGHTY WOMEN LOVE MAMA SAMIAH,MAJINGA NA YASIYOJUA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO NI SHIDA KWAO.
 
Rais gani ameshawahi kupendwa.
Hata Mwalimu alipendwa sababu ya zama za giza
 
Wanawake wajinga na wapumbavu hawawezi kumpenda mama samia hats kidogo!note this!
N.B,Jiepushe nasuala la kuusemea umma,katika masuala ya mtazamo binafsi.
 
Tatizo la Samia anajiweka na watu wa aina flani hataki kuchangamana na wananchi.

Hata akisimama kuongea anapoapisha wateule wake hagusi mahitaji ya wanachi wa hali ya chini ambao ni wengi anazungumza administrative issues tu.

Hayupo attached na watu kabisa anajiweka mbali nao. Uongozi ni kuwa karibu na watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…