Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

Gharama ya kufanya uchaguzi baada ya kifo Cha Magu Si kubwa kuliko HASARA Sa100 anayoingiza Taifa Kwa sasa.

Na Bado miaka 3.
 
Sio kweli kuwa mama hapendwi na
wananchi, ni rais ambaye ameleta utulivu na amani kwenye mioyo ya wananchi wengi. Ila kwenye hili la bandari kazidiwa akili na genge la wanyanganyi, inawezekana yuko Kama picha kuna rais wa nchi hii yuko nyuma ya pazia kashika rimoti yeye kawekwa kama geresha.
 
Mimi kwa upande wangu ngoja ninyamaze tu maan, kuna wengne humu had huw wanatukana ila wanapeta tu

Ila sisi wengne na Damu zetu za Kunguni 😂😁 unawez shangaa Nimelitoa neno humu kesho Nikajikuta Lokapu... Ila niishie tu kusema kwamba 2025 Mabadiliko yafanyike.
 
Tunampenda,Muacheni mama afanye kazi,haitakaa itokee Rais apendwe na Wananchi wote

Watz hamueleweki, Magufuli alipokua hai alipigwa maneno ya kila aina,kaondoka mnaibuka kumkumbuka,Watz wanatakiwa wapelekwe mpera mpera tu
 
ungesema CCM haipedwi ungepungikiwa na nini mkuu
 
Utampendaje mtu ambaye hajachaguliwa na wananchi?yeye amepata urais kwa njia haramu,hivyo hawezi kupendwa.kingine ambacho ni kikubwa zaidi ni ulegelege wa kusimamia rasilimali za nchi.yeye kila kitu ni kusaini tu hata vitu vya hovyo kabisa.mfano mkataba wa uuzwaji wa bandari
 
Ameingia kihalali mkuu, hajajiingiza kwa nguvu uongozini....
 
Too late!!
 
Mkuu awamu ya 5 kulikuwa na Bata? Au umesahau ile kauli mbiu ya Hapa kazi tu! Nakumbusha tu mkuu si kwa ubaya
 
Mm nafikiri utafiti uwe hivi
Mama anapendwa na wenyehela/matajiri kuliko masikini,masikini wanabanwa huku matajiri wakivinjari mijini. ..ile enzi ya unanijua mm nani imerejea kwa kasi kubwa sn
 
Matatizo ya Chadema ni hallucination. Nani kasema rais hapendwi? Watu wanasema rais hajachafuliwa na wananchi.
Kama Kamala Harris. Ni vice president,lakini watu hawataki kuambiwa eti anaweza kuwa rais.
 
Jana niliposti hoja kama hii:


Huyu mama kazi imemshinda. Hata jana kasema mwenyewe kaelemewa na majukumu. Nafasi imempywaya. Hili sakata la bandari ndiyo limedhihirisha kuwa "litmus test" yake. Hawezi kuendelea kuongoza nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…