UKWELI MCHUNGU: Wazazi wengi hawana upendo wa kweli

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Na watoto wakigundua tabia za namna hii Kwa wazazi upendo wao Kwa mzazi unapungua. Pia wao wanapunguza kupendana na kushirikiana.
Wanaishi kinafiki nafiki. Kisa walizaliwa tumbo moja.
Kweli kabisa hapo ni mwendo wa kunafikana tu maana wazazi wenyewe wanaonyesha mfano mbaya.
 
But wewe hapa umejenga hoja kwa jambo lingine. Mleta uzi hajasema kuwa wazazi wote hawapendi watoto wao ile ya dhati ya moyo. Ila ameweka bayana kuwa wengi wao huwa wanaishi na watoto kijamaa kuwa nikusaidia sasa ili unisaidie baadae. So bidii yote ya kuwekeza pesa kusomesha au kupambania mtoto afanikiwe ni aina ya uwekezaji.

Nikuulize, umeshahoji uhusiano uliopo kati ya mfugaji na mifugo yao. Umeona namna mfugaji anavyopata stress pale mnyama au mifugo yake inapokonda, kuumwa au kudhoofu kiafya.

Unaona anavyohangaika na muda mwingine anaweza hata kuingia madeni au kugombana na watu mradi tu mifugo yake iwe salama. Ila mwisho wa siku anafanya hayo yote kwasababu anaipenda, si ni kwasababu anataka inone ikue aichinje ale nyama yake tamu.

Ofcourse wapo wafugaji ambao wanafuga kwa upendo tu anaweza fuga ng'ombe, mbuzi, mbwa, paka, hata kuku kwa upendo tu wa kumtunza ili aishi kwa starehe tofauti na wanyama wengine na unakuta huyu mfugaji ni Vegetarian hatumii nyama kabisa.

Same kwa waza

Sasa kunatofauti gani na wazazi wa sasa?!
 
Pole Sana Mkuu.
Endelea tuu kuwaheshimu Sana wazazi wako.
Ila kimsingi suala la upendo Kama huna lolote ni nadra Sana.

Nakuambia hebu fikiria watoto wamezaliwa wakasambazwa kulelewa na kwa ndugu na hapo kila mtoto na baba yake jiulize hao watoto watapendana ,watakuwa na upendo kwa wazazi wao??
 
Mtoto mwenye kipato akifariki utasikia mama analia MUNGU UMENIWEZAAAA KWA NINI UMEMCHUKUA JIMMY,MBONA UMENIKOMOA MIMI.....,sasa wengine inabidi mstop kulia muangaliane sasa huyu mama alitaka achukuliwe nani?

Na wazazi wengi wakiwa na watoto wengi hawawez balance upendo kwa sababu nao ni binadam mfano mama yangu kuna watoto anawapenda kabisa ile realy ila wengine ni kwa vile unampa hiki na kile
 
Umeongea ukweli kabisa wazazi wa siku hizi wanapenda sana mtoto mwenye uwezo,hata wajukuu wakikutana likizo kale ka mwenye hela kanatreatiwa kama ka princess..tupambane tu kutafuta hela

Upendwe kisa pesa ee
 
Kweli kabisa,unaweza wewe jibana ukampa kahela yeye anakaficha anakuja kumpa mpenzi wa moyo wake.

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Noma Sana hiyo.
Alafu huyo anayempa anaenda kunywea pombe hapo ndio utajua hujui
 
Kuna watu wameumbwa kuishi kwa kufuata mkumbo tu ila sio kuelewa mambo yanakwenda vipi. Kama huyu kasoma ameona hajaelewa badala ya kuuliza maswali apewe ufafanuzi anatapika mashudu na buni inayotengeza kahawa.

Mtu keshaambiwa sio wazazi wote Ila wazazi wengi bado anabisha.
Sema utofauti wetu ndio unatufanya tukamilike
 
Unataka kusema Watu wote wanamali za kuwaridhisha watoto wao?
Upendo ni zaidi ya Urithi
Huyu jamaa hajui anachosema,tangu lini wazazi wote wakawa na Mali za kuwarithisha watoto zaidi hata ya wawili? Kuna wazazi ni maskini,na hawa mara nyingi ndio unakuta Wana hasira na watoto wao,

"Hata mzazi akutese vipi" hiyo kauli iandike tu,alafu iache humu ndugu. Mzazi anayemtesa mtoto wake huyo ni mhuni,na hafai kuwa mzazi,mzazi anatakiwa awe faraja kwa mwanae,nakwambia hakuna maumivu mabaya kama ya kuumizwa na mzazi,Bora uumizwe na mtu Mwingine aise,kumbuka mzazi wako ndio msiri wako,ndio Alfa na omega,yaani yy ndio alikuleta dunia hii,ndio anajua uzuri wako na mafhaifu yako,ikitokea anakutesa alafu eti uvumulie,Hilo umetudanya mchana kaka. Alafu,kama hukupitia machungu ya kulelewa ndivyo sivyo,hutaelewa.
 

Tena Zama hizi ni hatari zaidi hasa kwenye vikao
 
Mkuu uko sahihi Biblia imetabiri kuwa kuna siku upendo utapoa na kila mtu atapenda pesa. So hapo unaona dhahiri ya kuwa mtoto mwenye pesa ndio atapendwa. Pesa itareplace upendo.
 
Walikufanya nini Mkuu?
Walishawahi kumcharaza mtoto wa father mdogo viboko na faini ya mbuzi wawili na debe za mbege juu kisa ni kutohudhuria misiba ya ukoo na kugoma kutoa michango ya ugonjwa, misiba na sherehe mbalimbali za wanaukoo kwa miaka minne mfululizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ