kajekudya
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 2,466
- 4,916
Duniani kote hatua kubwa za kimaendeleo zinaathiriwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa kisiasa. Hawa ndio hutoa maamuzi ya mwisho kuhusu mstakabali wa Taifa. Hivyo tutake tustake lazima viongozi wetu wakuu wa kisiasa wawe akili kubwa, na wawe weledi.
Anzia Marekani, njoo Uingereza, pita hapo ujerumani, fika Russia, pita hapo china weka kituo Singapore au indonesia, basi fika hata Vietnam. Utakutana na kiongozi aliyeweka msingi wa maendeleo na lazima alikuwa ni akili kubwa na mweledi.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alianda kundi kubwa la vijana ambao walipata kila kitu na wangeweza kuwa msaada mkubwa sana, vijana ambao wengi wao walikuwa akili kubwa. Bahati mbaya karibia wote walimgeuka, labda Kama Salim Ahmed Salim ambaye bahati mbaya hakufika pale.
Sasa kwa wale wenzagu na mimi mliobahatika kupitia mfumo rasmi wa shule kuanzia vidudu hadi chuo kikuu. Hivi mnawakumbuka watu waliokuwa wanajishughulisha na siasa mashuleni hadi vyuo vikuu?
Ukweli ni kwamba walio wengi ni wale akili ndogo, wale akili kubwa mlikiwa busy kutafuta "division one" au GPA kubwa ili mbakizwe chuoni au muajiriwe chapu mkiingia mtaani. Wakati huo akili ndogo walikuwa busy kwenye korido za chama kutafuta connections, mwisho wakawa UVCCM, wakaingia kwenye data base Cha Chama.
Sasa Hawa ndio wenye chama, ndio wanaosemwa wanakijua chama, siyo wakuja, wao ndio watagombea ubunge, watakuwa mawaziri, wenye bahati wataukwa Urais, kwani elimu yake ikoje? Watateuliwa kuwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri, hawa ndio Sasa wanafanya maamuzi makubwa yanayohusu Nchi hii.
Huku pembeni wanapata ulinzi maridhawa kabisa kutoka kwa ndugu zao wale aliowasema Simbachawene kuwa wanadumu sana huko malindoni.Nyinyi na akiri zenu kubwa mnaishi kuambulia viteuzi vya hapa na hapa na kupiga vi dili vya hapa na hapa lakini akili zenu hamna sehemu mnaweza
kuzitumia kwa manufaa ya Taifa.
Mpo mnatekela maono ya akili zile zilizopata division 4, 3 Bila kusahau gentleman, mkijitahidi mnaishi kupendekeza tu, mara moja moja mnachomoza kwenye ngazi za juu Ila kwakuwa ngazi zote za kisiasa lazima zipate baraka za chama na kwakuwa 90% ndani ya chama ni wale niliowasema basi mnaishi kupigwa vita. Ndiyo, miamba iliyowekeza kwenye korido za Rumumba na siyo kwenye maarifa ndiyo imeshika hatamu.
Niwahakikishie ndugu zanguni tutaendelea kuongoza na Hawa watu wa aina hiyo kwa miaka mingi ijayo kwakuwa they are the only type available at disposal.