Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Kuhusu mutiny ya 1964 natamani mtu kama Kawawa angeandika memoirs zake kuhusu Kasheshe hilo. Niliwahi kumwuliza Mzee Bomani yeye alikuwa wapi wakati wa mutiny akaniambia alikuwa mmoja wa mawaziri waliopigwa makofi na 'afande', wakati wanamtafuta Nyerere. Wakati huo Mzee Bomani akiishi katika nyumba ile ya waziri karibu na Ikulu.Sasa ilikuwaje Kambona peke yake aliweza kuwasiliana na mutineers bila kupigwa makofi, sijui. Lakini ninachoamini, kama wangejua Nyerere alipokuwa, tungekuwa na kiongozi mwingine hapo 1964.

Mkuu Jasusi,

Darasa zito hili, binafsi I am not a fan wa Kambona, isipokuwa ninaheshimu mchango wake mzito katika kuzaliwa kwa taifa letu, na pia mawazo yake kuhusiana na mwendo ambao ungekuwa ni mwema kwa taifa letu kuliko ule wa ujamaa tulioufuata, kwa sababu ninaona kuwa yeye Kambona then alikuwa na vision ya mwelekeo unaofaa kwa taifa letu kuliko wa Mwalimu, by the fact kwamba leo wapinzani wanaimba wimbo ule ule wa Kambona, then, meaning kwamba tungeujaribu japo kidogo huenda tungekuwa na mtizamo tofauti kicuhumi leo,

Kwa nini Kambona, alikimbia? Maisha yangu yote nikiwa mdogo kupitia elimu ya bongo, nilifundishwa mengi mabaya kuhusiana na Kambona, lakini ninaamini kuwa only one hoja sticks, nayo ni yeye kukimbia Azimio La Arusha, hilo ndilo tulilokuwa tukifundishwa kama hoja ya msingi ya kukimbia kwake, unless kuna sababu nyingine, basi isemwe hapa tule education,

Kuhusu ile mutiny, I smell rat kuhusiana na role ya Kambona, kama ulivyosema ni kweli kabisa, Bomani alikuwa akiishi nyumba ya kwenye kona kuelekea Hospital ya Ocean Road, upande wa kulia alikuwa Jamal, upande wa kushoto alikuwa Mark Bomani (AG), usoni alikuwa Lusinde, kushoto kwake alikuwa Mwakawago, na kulia kwa Lusinde alikuwa Kawawa, ndio unaingia Ikulu kwa pembeni, siku ile ya noma Kambona alikuwa invisible, hawa wanajeshi waliziba njia zote zinazoingia na kutoka eneo hilo, lakini mkuu aliweza kupita kati yao na kuingia Ikulu, baadaye kutoka na kurudi tena, na hatimaye kuanza kuongea na wanajeshi, mpaka kuwashawishi waweke silaha chini, all this time mawaziri na viongozi wote waliokuwa wakiishi eneo hilo, yaani P. Bomani, M. Bomani, Mwakawago, Jamal, Msuya, Kawawa, Dr. Chiduo(ambaye naye alikuwa akiishi eneo hilo), na Mzee Kitenge (aliyekuwa bosi wa Relwe) wote walikuwa mikononi mwa wanajeshi hao, na baadaye waliachiwa kutokana na amri ya Kambona, ambaye baadaye aliapa kuwa alikuwa hajui kuwa walikamatwa, that is a joke kwa Kambona side, ukweli ni kwamba he had a hand on the whole situation, maana jinsi alivyoenda na kurudi kwenye situation nzima, I do not know,

Lakini haibadilishi jinsia kuwa mawazo yake kuhusiana na mwelekeo wa nchi yalipaswa kupewa uzito na Mwalimu, kwenye kuyapuuza na kufikia kukimbia kwake, tulipoteza kichwa kikali kwa sababu binafsi ninaon kuwa sasa hivi tunahangaikia yale yale aliyoyasema then, na pia haibadili ukweli kuwa tuna uchumi uliokwama, na hatujui la kufanya ni kwa sababu msingi iliyopandwa mapema ulikuwa ni wa wasi wasi, na hiyo lawama hakuna wa kumpa zaidi ya Baba wa Taifa letu, haimfanyi Kambona kuwa malaika katika conduct zake na mawazo yake, the matter of fact alinikatisha tamaa kabisa pale siku ile Jangwani, aliposema uongo tena mchana kweupeee!

Ahsante Wakuu!
 
Mzee FMES na wawe kama Jasusi you are filling the gaps kwenye habari muhimu sana. Tangu kuanza mjadala huu nimejaribu kuzungumza na wazee wetu (baadhi umewataja hapa) kuhusu Kambona na Army Mutiny. WOTE hawataki kuzungumzia mmoja akasema its "very sensitive bwana". It is real frustrating!
 
tatizo, hamna tatizo kwani SASA najua kuwa "article flani hivi" ilimaanisha siyo article yako. Maana hata mimi naweza kunukuu mojawapo ya article zangu (za kiingereza au kiswahili) na kuweka hapa na watu wakapata impression labda namnukuu mtu mwingine. Ila nikisema "article flani hivi" ina maana siyo ya kwangu. Sawa mkuu! Hii lugha ya Kiswahili inashida kidogo kwa sisi wengine. Kumbe uliposema "kutoka article flani hivi" ulikuwa unamaanisha hii ya Scott ambayo ina jina lake. Haya tuendelee kukata issue nimekuelewa sasa.

halafu baada ya hapo ikawaje?? umeumbuka!!!! unataka kukamata mwizi pasipo mwizi. Kazi kwenda nje ya mada, yaani sijui ni nini hasa unachotaka ku-prove?? Kweli wakishindwa hoja huleta vioja. It was more than obvious kwamba zile passage mbili si zangu..............kwani hilo nalo mpaka uwe umesoma clinical psychology(diploma) kwi kwi kwi bugando???..........mie silipwi hapa, so na post na kama mtu anataka kujua zaidi atatafuta mwenyewe kwenye web. Unaweka std ya juu sana, ndio maana nikasema wewe mwenzetu upo kazini. Mfano mzuri ni huo wa Scott wa Yale, umeitaka hiyo article kujua zaidi umeipata.........lakini kwa mawazo yako ulitaka mie nikwambie inapatikana wapi!!!. Unafanya hivyo mwenyewe, hii ni forum uncle, sio darasa la clinical psychology pale Bugando!!.
 
Mwanakijiji,
Kuhusu mutiny ya 1964 natamani mtu kama Kawawa angeandika memoirs zake kuhusu Kasheshe hilo. Niliwahi kumwuliza Mzee Bomani yeye alikuwa wapi wakati wa mutiny akaniambia alikuwa mmoja wa mawaziri waliopigwa makofi na 'afande', wakati wanamtafuta Nyerere. Wakati huo Mzee Bomani akiishi katika nyumba ile ya waziri karibu na Ikulu.Sasa ilikuwaje Kambona peke yake aliweza kuwasiliana na mutineers bila kupigwa makofi, sijui. Lakini ninachoamini, kama wangejua Nyerere alipokuwa, tungekuwa na kiongozi mwingine hapo 1964.

Ahsante mkuu,
Hapa kuna pieces kibao za puzzle zinamiss,alafu swali ninalojiuliza ilikuwaje akamshinikiza mwalimu aombe msaada wa waingereza, kama aliweza kuongea nao na wakaanza kukubaliana?

Kama kuna uwezekano wa mama Maria na mke wa Kambona kuhojiwa kuhusiana na hilo tukio, Mzee Kawawa naye atakuwa anajua mengi sana kuhusiana na hilo tukio.
 
Pundit, Kambona hakukataa Azimio la Arusha, ambacho alikitaka yeye ni majaribio kwanza kabla ya kwenda full fledged.. alitaka kama ni vijiji vya ujamaa basi tuwe na vya mfano kwanza n.k

Kama ni hivyo Kambona alikuwa na Ubongo mkubwa kuliko Nyerere.
 
Pundit, Kambona hakukataa Azimio la Arusha, ambacho alikitaka yeye ni majaribio kwanza kabla ya kwenda full fledged.. alitaka kama ni vijiji vya ujamaa basi tuwe na vya mfano kwanza n.k

Huoni kama hiyo ni genius!!!. Hata ukitaka kununua motakaa kwanza unapata "test drive." Kwanini Mzee kifimbo alikataa idea practical kama hiyo??
 
Ndio maana nasema childish, hiyo post unayonikariri nimekopi inasema wazi kuwa si maandishi yangu!!!. Nimeandika "paragraph hizi mbili toka kwenye article flani"...........maandishi yangu mimi ni kwa kiswahili na ya Scott kwa kizungu. Wallahi kila mtu alosoma ile post hata kama ni darasa la pili atajua kuwa maneno ktk paragraphs zile si yangu na hakuna sehemu nilosema ni yangu!!!!!!!!!. Jamaa bwana, kweli mkiishiwa hoja huleta vioja.........jaribu tena!!!!. Wakopie basi post nzima hapa watu waisome tena, waamue kama wewe umenikamata au umejikamata mwenyewe!!!!.

Creativity ni ku-connect dots na hicho ndicho ulichofanya.
 
Creativity ni ku-connect dots na hicho ndicho ulichofanya.

Asante ndugu yangu kwa kuliona hilo......ni juhudi binafsi za kuua mjadala, awamu ya kwanza ilifeli(kuweka mada kwenye udaku), awamu ya pili ikawa kuleta ghasia, utoto na ku-attack hoja za wengine nayo ikafeli, sasa wapo ktk awamu ya tatu ambayo ni ku-attack watoa hoja.....inshallah nayo pia itafeli. Mada hii kama kufa itakufa natural death na sio kwa bullet ya assassin!!!. Mie nitaendelea kuwepo na sita quit kama mchambuzi......kwahiyo haters, nipo hapa to stay.
 
Kuhusu mutiny ya 1964 natamani mtu kama Kawawa angeandika memoirs zake kuhusu Kasheshe hilo. Niliwahi kumwuliza Mzee Bomani yeye alikuwa wapi wakati wa mutiny akaniambia alikuwa mmoja wa mawaziri waliopigwa makofi na 'afande', wakati wanamtafuta Nyerere. Wakati huo Mzee Bomani akiishi katika nyumba ile ya waziri karibu na Ikulu.Sasa ilikuwaje Kambona peke yake aliweza kuwasiliana na mutineers bila kupigwa makofi, sijui. Lakini ninachoamini, kama wangejua Nyerere alipokuwa, tungekuwa na kiongozi mwingine hapo 1964.

Jasusi,Mwanakijiji,Field Marshall,YourName,Maswali,..

hii hoja kwamba Kambona hakupigwa makofi kwa hiyo kunauwezekano alihusika naona haina msingi sana.

kuna kitabu kimeandikwa kuhusu haya "mapinduzi" na hili suala limezungumziwa. wamehojiwa watu wengi,Kawawa,Sarakikya,Sgt.Hingo Ilogi,Emilius Mzena, hata maofisa wa Kiingereza waliokuwepo. wote hao hawakumtaja Kambona kama mhusika.

vilevile kuna wananchi waliouawa ktk "mapinduzi" hayo nadhani maeneo ya magomeni, au ilala. Sasa ktk hali hiyo hiyo kwanini hatuhoji Bomani kupigwa makofi, instead ya kuuwawa?

kwanza ni lazima tu-establish Bomani alipigwa makofi na nani? vilevile lazima tu-establish hao waliompiga makofi walikuwa ktk hali gani.

Maasi/Mapinduzi yale yalikuwa very disorganized. Siyo Mawaziri tu waliopigwa makofi, wako maofisa wa Jeshi waliopigwa makofi na kutiwa rumande.

kwa kumbukumbu zangu ktk kusoma kitabu cha maasi ya 1964, wakati wote wa maasi yale, Sgt.Hingo Ilogi[kiongozi wa maasi] alikuwa akijaribu kuwatuliza askari wenzake. Vilevile madai yao makuu yalikuwa ni vyeo jeshini, na mazingira mazuri ya kazi.

Maswali ya msingi ya kujiuliza ni haya hapa:

1.Kama nia ya msingi ya maasi yale ilikuwa ni kubadili serikali, je majadiliano kati ya Kambona na waasi yalikuwa yanahusu nini?

2.Kama Raisi alikuwa ameshakimbia kwanini waasi wale hawakuikalia Ikulu na kuunda serikali?

3.Kama Kambona alihusika na mapinduzi yale, kwanini hakujitangaza Raisi wakati inaeleweka kabisa kwamba Nyerere alikuwa mafichoni?

4.Waasi walifikia mpaka kuchagua Mkuu wao wa Majeshi[CDF], kwanini hawakumchangua Amiri Jeshi wao Mkuu?

4.Kitendo cha Nyerere kwenda mafichoni kilikuwa na maana gani? Je, alikuwa ameachia madaraka yake ya Uraisi? Nafasi yake ktk majadiliano na waasi ilikuwa ipi?
 
3.Kama Kambona alihusika na mapinduzi yale, kwanini hakujitangaza Raisi wakati inaeleweka kabisa kwamba Nyerere alikuwa mafichoni?

Mkuu heshima mbele, baaada ya kuongea sana na wazee walio ona kwa macho yaliyotokea, ikiwa ni pamoja na kujadili kwa kirefu sana tabia za kawaida za kisiasa, za Kambona, binafsi ninaamini kabisa kuwa something was not right na uasi na Kambona kuuzima, na yeye pia kwenda kumficha Mwalimu, na yeye tena kuongea na wanajeshi, mkuu it just does not add up,

Viongozi wa enzi zile mkuu, wanasema Kambona alikuwa na tabia moja mbaya sana, ya kujitafutia ujiko wa kisisasa, kwa mfano alikuwa na tabia ya kumuendea Mwalimu kwa siri na kumshauri am-promote kiongozi fulani, Mwalimu akikubali, basi yeye Kambona humuwahi yule mkuu na kumfahamisha kuwa kesho yake atatangazwa kupanda cheo, na ni yeye ndiye aliyempigania sana kwa Mwalimu, maaana Mwalimu, alikuwa hataki kabisaaa, lakini yeye Kambona ndiye aliye-make things mpaka ika happen, sasa in light of this sioni ugumu wa kumuelewwa role yake kwenye uasi huo wa jeshi, na putting in mind kuwa Mwalimu, hakuwa mjinga kiasi hicho cha kuchezewa na Kambona na asijue.
 
Sina source za miaka hiyo na vile vile sikuyaona hayo matukio. Lakini niki-connect dots sipati picha kuwa Kambona alikuwa na tabia mbaya. Hizi ni premises zangu:

1./ Kumbuka CHARISMA ya Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani na alivyovutia watu. Na walioona matukio wanasema kuwa CHARISMA ya Mrema ilionekana kipindi cha Kambona tu. Wakati wa shughuli za kitaifa viongozi waliingia uwanja na watu hawakustuka lakini alipoingia Kambona uwanja ulilipuka. Vile vile Kambona alikuwa maarufu kabla ya uhuru. Kama inavyoonyesha katika mjadala huu, ni yeye aliyeweza kutafuta wanachama wapya 10,000 wa TANU katika kipindi cha miezi sita. Ajitafutie ujiko gani zaidi ya huo. Kambona aliweza kuji-connect na watu wa kawaida kuliko kiongozi mwingine.

2./ Kule Kigamboni kuna mahandaki au mapango ambayo yaliachwa na mjerumani. Aliyechukua nafasi ya ukatibu mkuu wa TANU alifumaniwa kule akipata uroda na kijirusha vibaya vibaya. Na huyu jamaa ana watoto kila wilaya. Kama ni tabia mbaya basi kwanini huyu yake alionekana mazuri kuliko ya Kambona?

3./ Kama alikuwa na tabia mbaya kwani kampeni na propaganda zitumike kuharibu jina lake? Kwanini nyimbo za mchakamchaka zitungwe kwa ajili yake?

4./ Kama makosa yalikuwa ya Kambona kwanini ndugu zake waliwekwa kizuizini mpaka mwaka 1982? Tabia ya Kambona kwanini itese ndugu zake?

5./ Kwanini walisema yeye ni Mmalawi? Wakati anapigania uhuru, umalawi wake ulikuwa hauonekani.

6./ Pia Kambona alikuwa mbunifu, mavazi ya mgolole alianza na viongozi wengine wakaiga ili kupata umaarufu. Watu ambao walikuwa hawajuhi kujitafutia UJIKO kwa wananchi walimuona Kambona kama THREAT.
 
FMES,
Ktk pitapita ya kuuliza wazee waliokuwepo enzi hizo, kuna vitu vya kutilia maanani, je watu hao hawana bias? je uhusiano wao na Kambona ulikuwaje? Nyerere sympathizers lazima watamponda Kambona. Yes, labda hakuwa msafi kihivyo, lakini mtu kuadhibiwa kwa sababu yupo "ambitious na maarufu" nadhani si sahihi.
 
Wakuu Maryam na YRS,

Heshima mbele,

I mean hiyo tabia ya Kambona, inaweza kuwa ni tabia mbaya kwa mmoja na ikawa ni tabia ya kisiasa kwa mwingine, na ya kawaida kwa mwingine, lakini ni tabia ya kawaida kwa wanasiasa let me make that clear, otherwise binafsi sisemi kwamba inapunguza anything katika accomplishments za Kambona, no way tena in absolute, wakuu wengi wa enzi hizo tena close friends wake wanakubali kuwa hii ilikuwa ni moja ya tabia za Kambona, ambayo pia inaweza kuitwa kuwa lugha ya kisasa kuwa ni kujichanganya na viongozi au kujiweka sawa na viongozi,

Wengi wao hawataki kuongelea ule uasi kabisaa for now, katika siasa maana yake ni kwamba time bado haijawa tayari, lakini wasiokuwa wanasiasa wanaokubali kuiongelea wengi wana wasi wasi sana na role ya Kambona, kwenye ule uasi, kama vile wanasiasa wengi walivyo na wasi wasi wa role ya Mwalimu, kwenye kuondoka kwa Karume, n ex-PM, binafsi sijui lakini connecting little darts nilizozisikia tayari, binafsi nina wasi wasi na role ya Kambona kwenye ule uasi, lakini haina maana kwamba ina diminish uwezo mkubwa wa Kambona, aliokuwa nao kisiasa, hapana,

Bado ninaamini kwamba he was a leader with great vision, kwa sababu hilo ndio tatizo kubwa linalotukabili sasa hivi as a nation na viongozi wetu wa sasa hawa kina Makamba, Msekwa, na Chiligati hawana vision, yaani bongo tunahitaji kiongozi angalau mmoja tu mwenye vision kama Kambona, ambaye mambo aliyokuwa akiyaona 42 years ago yana-make a sense mpaka leo, Mwalimu alikuwa na maneno mazuri pia lakini only to listen to hayakuwa applicable kwa mazingara ya siasa za kisasa za uchumi mbele,

Kambona, bado ni mmoja wa viongozi ambao walikuwa na vision kali sana, na since then hatuajapata mwingine mwenye vision kama yeye, wanasema maneno mengi wakiwa nje wakiingia wanakuwa wale wale tu, kina Chami,na Kamalla walipokuwa kule Tanzanet, walikuwa wanasema maneno mengi mazuri toka waingie wako kimyaaaa!
 
Marshall,
Nashukuru kuwa umefanya utafiti na kugundua kuwa huyu bwana aliwaliza mapaka mawaziri wenzake. Ukiendelea kidogo hutakuwa na shaka tena kuwa huyu alihusika moja kwa moja na uasi ule. Endelea Marshall, haya mambo ya historia yanapopotoshwa yanachanganya sana.
 
Wakuu Maryam na YRS,

Heshima mbele,

I mean hiyo tabia ya Kambona, inaweza kuwa ni tabia mbaya kwa mmoja na ikawa ni tabia ya kisiasa kwa mwingine, na ya kawaida kwa mwingine, lakini ni tabia ya kawaida kwa wanasiasa let me make that clear, otherwise binafsi sisemi kwamba inapunguza anything katika accomplishments za Kambona, no way tena in absolute, wakuu wengi wa enzi hizo tena close friends wake wanakubali kuwa hii ilikuwa ni moja ya tabia za Kambona, ambayo pia inaweza kuitwa kuwa lugha ya kisasa kuwa ni kujichanganya na viongozi au kujiweka sawa na viongozi,

Wengi wao hawataki kuongelea ule uasi kabisaa for now, katika siasa maana yake ni kwamba time bado haijawa tayari, lakini wasiokuwa wanasiasa wanaokubali kuiongelea wengi wana wasi wasi sana na role ya Kambona, kwenye ule uasi, kama vile wanasiasa wengi walivyo na wasi wasi wa role ya Mwalimu, kwenye kuondoka kwa Karume, n ex-PM, binafsi sijui lakini connecting little darts nilizozisikia tayari, binafsi nina wasi wasi na role ya Kambona kwenye ule uasi, lakini haina maana kwamba ina diminish uwezo mkubwa wa Kambona, aliokuwa nao kisiasa, hapana,

Bado ninaamini kwamba he was a leader with great vision, kwa sababu hilo ndio tatizo kubwa linalotukabili sasa hivi as a nation na viongozi wetu wa sasa hawa kina Makamba, Msekwa, na Chiligati hawana vision, yaani bongo tunahitaji kiongozi angalau mmoja tu mwenye vision kama Kambona, ambaye mambo aliyokuwa akiyaona 42 years ago yana-make a sense mpaka leo, Mwalimu alikuwa na maneno mazuri pia lakini only to listen to hayakuwa applicable kwa mazingara ya siasa za kisasa za uchumi mbele,

Kambona, bado ni mmoja wa viongozi ambao walikuwa na vision kali sana, na since then hatuajapata mwingine mwenye vision kama yeye, wanasema maneno mengi wakiwa nje wakiingia wanakuwa wale wale tu, kina Chami,na Kamalla walipokuwa kule Tanzanet, walikuwa wanasema maneno mengi mazuri toka waingie wako kimyaaaa!

Wanaomtetea Nyerere kwa uvumbi na ubani, wanasema Nyerere alikuwa sio Malaika. Hivyo alifanya mazuri na mabaya. Na wanadai mazuri yake outweight mabaya.

Kwa mtaji wa posti yako ninayoijibu na premises nilizoziweka ni kweli kabisa mazuri aliyofanya Kambona kwa nchi ya Tanzania yanapita mabaya aliyofanya kwa kiwango kikubwa sana na katika kipindi cha muda mfupi sana.

Ukiondoa nchi Nordic zinazofuata ujamaa kwa kushinda kwenye uchaguzi, viongozi wa nchi zilizobaki wa-eliminate viongozi waliopingana kimawazo.

Mrema alipojitoa CCM tulijua mabaya yake zaidi kuliko pale alipokuwa bado ndani ya CCM. Analogy, mabaya ya Kambona yamejulikana zaidi baada ya kukimbia.
 
Field Marshall ES,

kama Kambona alikuwa na hizo tabia ulizozitaja[kupenda umaaarufu na madaraka] kwanini hakuchukua nchi wakati Mwalimu na Kawawa wako mafichoni?

Kama ni kutokupigwa makofi hata Emilius Mzena hakupigwa makofi. Je na yeye alihusika na hayo maasi? Tuwe makini na haya madai yetu jamani.
 
kama Kambona alikuwa na hizo tabia ulizozitaja[kupenda umaaarufu na madaraka] kwanini hakuchukua nchi wakati Mwalimu na Kawawa wako mafichoni? Kama ni kutokupigwa makofi hata Emilius Mzena hakupigwa makofi. Je na yeye alihusika na hayo maasi? Tuwe makini na haya madai yetu jamani.

1. Wakuu heshima mbele, tunajaribu kuiangalia historia tukiwa na habari chache sana, sasa haya sio madai yetu isipokuwa ni ukweli wa tabia za Kambona, sijamsikia kiongozi yoyote anayemjua kwa karibu askimea kuwa Kambona alikuwa mpenda mdaraka, hapana, lakini nimeambiwa na wengi wanaomjua kwa karibu kuwa alikuwa mpenda sifa sana kwa viongozi wenziwe, hilo sina wasi wasi kuwa ni kweli,

2. Kupigwa makofi kwa baadhi ya viongozi wakati wa uasi ili waseme Mwalimu yuko wapi, binafsi bado sijaweza kuiangalia kama ni hoja nzito kuhusiana na uasi ule, lakini kwa maoni yangu ni kuwa Kambona hakuwa mbongo, alikuwa M-Malawi, je angeweza kuiongoza bongo? I don't think so, nafikiri he was smart enough kuliona hilo mapema, akizingatia kuwa moja ya tatizo la uasi ule lilikuwa kuwataka wanajeshi wa kigeni waondolewe, ili wazalendo washike hatamu, sasa Kambona angeingiaje hapo na kuchukua nchi? Jasusi anaposema aliongea na Mzee Bomani, ninamuamini tena bila any doubt, sasa sio kwamba viongozi wote ambao hawakupigwa makofi walihusika, maana waliopigwa ni wale waliokuwa wanaishi karibu na Ikulu tu,

sasa kwa maneno yako mkuu Joka, una-raise a very intersting ishu kuwa je inawezekana kuwa Kambona alishindwa kuchukua power kwa sababu hakujua Mwalimu na Kawawa, wako wapi? Na hii habari kuwa ni yeye aliyeenda kuwaficha ni fiction?
 
We who were born on sixties were fed with misleading stories about Kambona.Had you Mzee Mwanakijiji been active on those days you would have changed hii nchi to a great leanth.
But yes you my big up for this historic post
 
Wakuu,
Nimerudi kuangalia vitu viwili vitatu inaonekana ni kweli Kambona alikuwa anataka umaarufu wa haraka. Kutoa mfano, nina ripoti moja inahusu ishu moja ya "alleged" forged documents kuhusu Marekani kutaka kupindua nchi kwa ushirikiano na wareno mwishoni wa 1964. Serikali ilipata document moja iliyokuwa inaonyesha mipango ya siri ya kupindua nchi. Kambona aliharakisha kukimbia kutoa habari OAU na vyombo vya habari kwamba Wamarekani wanapanga kupindua nchi kwa kutumia mercenaries. Wamarekani wakaleta mtaalamu wao achunguze hiyo paper, balozi wa marekani akaande moja kwa moja kwa mwalimu kumwonyesha ushahidi kwamba ni feki.

Balozi anaripoti Nyerere alishika kichwa na mikono miwili. Akamwambia balozi, and I quote: "I don't know what Kambona is doing"? Wamarekani walitaka Nyerere aseme publicly kwamba ilikuwa ni uongo. Yeye akakataa kwasababu ishu ilishafika mbali sana. It was a major diplomatic dissaster and very embarassing to Mwalimu.

Hii haikuwa mara ya kwanza au ya pili Kambona kukurupuka na kuharibu mambo. Kuna mifano mingine. Nyingine ilitokea 1960 wakati Nyerere amesafiri. Kambona aliwaambia wakoloni tunataka uhuru sasa hivi na alikuwa anaoongea kama mmoja wa viongozi wa chama. Huo ulikuwa wakati Nyerere ana-negotiate na U.K. kuhusu uhuru. Ikaja kuleta matatizo mengi. Kwa ujumla ni kwamba Kambona alikuwa anakosea stepu wakati mwingine. Na nakubaliana nanyi kwamba inaonekana alikuwa anataka umaarufu.

Hii ripoti ninayo. Kinachonisikitisha ni kwamba Bongo hizi ripoti wanaficha, lakini ulaya na kwengine zinapatikana. Mengi wasiyotaka kuongelea yapo kwenye ripoti za nje. Siwalaumu sana, lakina kuna mengi mazuri nchi yetu ilifanya lakini ni vigumu sana kupata access ya data na kuandika hizo historia. Matokeo yake ni kwamba tunaachwa kwenye giza.
 
jokaKuu,
Asante sana kwa mchango wako katika suala hili. Na mimi pia ningependa kukisoma hicho kitabu. Kama alivyosema Mwkjj, inasikitisha kuwa viongozi ambao bado wako hai na wana data za hili sakata wanasita kuzitoa hizo data. Hiyo ni kuviacha vizazi vijavyo gizani na kutunyima historia yetu kamili. Ndiyo maana nimesema ingekuwa bora Mzee Kawawa aandike memoirs zake kwani naye aliona mengi.
Ni kweli uasi ulikuwa disorganized. Na suala muhimu wanajeshi walitaka "Africanization now," Lakini uasi huo pia ulicreate a leadership void. Mimi ninachoamini ni kwamba kama Kambona angejua Kawawa na Nyerere wako wapi, something else may have happened. Kambona asingeweza kujitangaza kiongozi as long as hawa wawili hawajulikani walipo. Waasi wasingeweza kuunda serikali kwa sababu hilo halikuwa lengo lao. Labda kuna wachache tu waliokuwa na lengo hilo lakini si wanajeshi wote.
But all in all there are a lot of blanks that need to be filled. Nasikia kuna mwanajeshi mmoja Mwingereza aliyeshiriki katika kuzima uasi huo ameandika kitabu. I would like to get my hands on it to read his perspective.
 
Back
Top Bottom