Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Ndugu mtoa mada, mimi niliwahi kumsikia JPM akisema kuwa, Gas ya Mtwara ilishapigwa mnada wakati wa Awamu nne, hivyo hatuwezi kufaidi ile Gas sisi kama Watanzania.
Kwa hiyo, kwa kuona hivyo aliamua kuanzisha ujenzi wa Bwawa hilo.
 
Ukimezeshwa betri ukariri maneno unafikiri inakuaje? Wanasema wasichokijua wala kukielewa kama parrots
 
Hao hao wachina hivi karibuni wamejenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme kuliko letu, unazani hiyo ecology walikuwa hawaijui.

Hilo bwawa lao mpaka sasa washakata miti mingapi?
 
Huna gas ww? Kipindi kile bungeni uliambiwa umeme ukizalishwa kwa kutumia gas, bei zitashuka vip tokea waanze kuzalisha umeme wa gesi Cost per unit imeshuka?

Hapo ndipo utapata majibu gas ni ya nani na nani ana control bei ya hiyo gas.

Ndege ni zetu, mbona nauli ni ghali kuliko ilivyokuwa fast jet? Au hizo ndege nazo zina wenyewe kama hiyo gas?
 
Ndege ni zetu, mbona nauli ni ghali kuliko ilivyokuwa fast jet? Au hizo ndege nazo zina wenyewe kama hiyo gas?
Mbona unahamisha magoli? Huwezi fananisha ndege na nishati ambayo ina impact kwa kila raia mmoja mmoja.
 
Africa shida ipo sana kwenye kujali muda.

Yani kujaza bwawa maji rais anafunga safari na convoy yake kwenda kushuhudia?
 
Hivi hii SGR wamekata miti mingapi hadi sasa au hesabu zinaishia bwawani tu?

Kuna uwezekano idadi ikawa kubwa kuliko hata hiyo ya JNHPP.

Hakuna maendeleo bila kukata miti duniani.
 
Waethiopia sahv wanakazana kupanda miti kwao

Ova
 
Bora alikufa mapema, vinginevyo Tanzania ingekuwa na miradi mingi kwa ajili ya sifa ila nchi inaumia
 
Mbona unahamisha magoli? Huwezi fananisha ndege na nishati ambayo ina impact kwa kila raia mmoja mmoja.
Kabla ya umeme wa mafuta mazito, na gas tulikuwa tunatumia umeme wa maji, mbona haukuwa wa bei rahisi? Au huo ni umeme wa maji gani labda. Ukakope fedha zote hizo, kisha utegemee umeme wa bei rahisi?
 
Waethiopia wako kwenye phase 3 ya kulijaza maji bwawa lao

Ova
 

NInakazia;

"Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili."
 
Kama swala ni upatikanaji wa hewa safi. Bahari ipo na ndio inatoa 80% ya oksijeni tunayovuta.

Umetoa wazo zuri sana mkuu. Tupande miti kufidia iliyokatwa problem solved.
Ndiyo mpande miti sasa

Ova
 
Dah,yaani kama ulaya,Mungu ambariki magufuli,
mleta mada kama umeishajenga au unapanga,hata hapo ulipojenga lazima kuna mimea ilikatwa ili upate pa kuishi
unless unaleta uzi huu kutokea porini kama ngedere hapo nitakuelewa.
Hili dude si mchezo

Ova
 
Kabla ya umeme wa mafuta mazito, na gas tulikuwa tunatumia umeme wa maji, mbona haukuwa wa bei rahisi? Au huo ni umeme wa maji gani labda. Ukakope fedha zote hizo, kisha utegemee umeme wa bei rahisi?
Hivi unatizamaga bunge wakati wa sekeseke lile la gesi?

Huja msikia waziri wako akisema umeme wa gas utapunguza gharama za umeme kwa unit?

Mimi nilicho tarajia kwanza gesi ni yetu ,pili umeme uzishalishaji umeongezeka basi hata bei itapungua kama alivyosema waziri wako kipindi maana tuna matilioni ya cubic litre za gasi Mtwara.

Ila duniani kote umeme wa maji uzalishwaji wake ni cheap na ndio maana hata China nae kakimbilia huko huko hivi karibuni kazindua bwawa kubwa kuliko letu la kuzalisha umeme,kwani unazani China alishindwa kuweka power plant ya nuclear.

Miradi inayojengwa ktk nchi yoyote duniani hela yake wanakopa, ila wanacho tuzidi wenzetu wanajua kuisimamia miradi iliyo tengenezwa kwa hela ya mkopo ili irudishe hela.
 
NInakazia;

"Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili."
Punguzeni siasa kwenye mambo ya kitaalam,hivi wakati wanatandaza bomba la gesi kutoka urusi hadi ulaya magharibi huko hawakufyeka miti
Ehhh

Ova
 

Ni kweli umeme wa maji ni cheap, lakini uwekezaji wa huo mradi ni fedha za mkopo. Unajua terms za marejesho ya huo mkopo?

Kwani Magu aliwahi kuweka mkataba wowote wazi hadi uwe na imani naye kwenye mikataba?
 
Duh Trillion 11 ni very expensive, bora hata tungewekeza kwenye Wind na Solar, mikoa ya kati kama Singida na Dodoma ina jua na upepo wa kutosha sana, na story ya gas ni kama ya mabehewa ilivyokuwa hakuna anayesema ukweli,anyway tunaangalia mbele pesa zimeshalipwa, CCM ni ovyo kama panya road tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…