Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

UPUUZI MTUPU - POROJO TU
 
Sitengenezi mazingira ya kubishana, nazungumzia niliyoshuhudia kwetu ambako naona tofauti kubwa na baadhi ya maeneo walikoendekeza midundiko, vigodoro na cherekochereko
Mzee unaweza kujifariji lakini kusema ukweli Tanzania ni moja ya mataifa yenye watu wasio na elimu.

Lakini takwimu zipo kwenye mtandao. Literacy rate ya Tanzania miaka ya 1970 to 1980s ilikuwa haifikii hata 50%. Inamaana zaidi ya nusu ya watanzania walikuwa bado hawana elimu.
 
Mkuu sijaongelea hapa dini ya kiislamu acha kuingiza dini ya wstu katika mijadala. Kwani wasabato sio wa Kristo? Acha kubaguwa madhehebu ya wengine plz
 
Kuendelea kumlaumu Nyerere miaka 60 baada ya uhuru ni sawa na kumlaumu babu yako for your failures. Baba yako had an opportunity na wewe ushakua mtu mzima you can correct them as well. Cheap excuses ndo zinafanya muendelee kuwa hapo mlipo.
 
Usitake kuleta utetezi usio na maana, Nyerere kachukua Nchi kutoka Kwa mkoloni Iko organized na Ina miundombinu yote yeye kaiz yake ilikuwa ni kuifanya iwafaidishe wote.

Sasa yeye akaanza na swaga zake za ujamaa na ukombozi wa Africa,kazunguka Dunia nzima sijui alikuwa anafafuta nini.

Kuna Nchi Nyarere hajakanyaga Dunia hii?
 
Naunga mkono hoja 💯💯
 
Sas Kwa nini umtoe kwenye lawama na ameongoza miaka 25?
 
Mkuu sijaongelea hapa dini ya kiislamu acha kuingiza dini ya wstu katika mijadala. Kwani wasabato sio wa Kristo? Acha kubaguwa madhehebu ya wengine plz
Wewe mada inahusu mapungufu ya Mwalimu Nyerere katika uongozi,Kanisa Katoliki limeingiaje hapo? Unajifichia kwa mgongo wa kuyasemea makanisa mengine wakati kwa nyuzi kibao tu nakujua misimamo yako Vs Ukristo kwa ujumla wake.Jikite kwa mada na liache Kanisa Katoliki pembeni kama ni hivyo.
 
Angola asilimia kubwa ni wakatoliki. Wamekaa kwenye vita kuanzia 1975 mpaka 1991. But kwa sasa uchumi wao ni mkubwa kuzidi wetu kwa mbali tu.

Kuanza kulaumu kanisa kwa madhaifu ya kwake Nyerere binafsi ni kutowatendea haki wakatoliki
 
Kongole kwa muanzisha mada.
Nimesoma michango mingi,nimeona mada kama hii ina tija katika kuleta mabadiliko ya nchi yetu kuliko zile mada zinazoanzishwa kwa minajili ya udini.
Nitaweka mchango wangu kulingana na michango ya wanajamvi hapo nitakapo pata muda.
CC: Bams
Chige
 
Kuendelea kumlaumu Nyerere miaka 60 baada ya uhuru ni sawa na kumlaumu babu yako for your failures. Baba yako had an opportunity na wewe ushakua mtu mzima you can correct them as well. Cheap excuses ndo zinafanya muendelee kuwa hapo mlipo.
Tunaongea kama taifa, ukizungumza habari ya mmojammoja wengine tupo very fortunate.
Kama una maisha mazuri na waliokuzunguka wapo kwenye hali duni na wala hilo halikuumi basi ni wazi hata wewe uko kinyume na Nyerere. Nguzo kuu za siasa zake zilikua 'UTU, USAWA na UHURU'
 
Alikosea Sana kwenye elimu alipewa fedha za fidia kutoka uingreza kwa ajili ya elimu kwa watanzania

Alichokifanya akafudisha walimu wa UPE wale wanaosoma darasa la Saba mara mbili halafu wanaenda kufundisha mashuleni

Halafu hizo fedha badala ya kuwekeza kwelikweli kwenye elimu yeye eti Ili kufuta ujinga watu wazima ikawa lazima kwenda shule hata umri wa miaka 79 eti ajue kisima na kuandika

Eti wazee wanaenda shule wakajifunze. Matokeo yake walikua wanasinzia tu
 
Miundombinu yote ipi hiyo kiongozi?
So Nyerere alikuta Tanganyika ina shule za kutosha, barabara za kutosha, zahanati kila kijiji, maji kila kona, watanzania wote wana elimu ya vyuo vikuu ama unataka kusema nini?

Maana hiyo ndio miundombinu yote ya msingi inayohitajika.

So Nyerere alikuta yote akaharibu na sera zake za ujamaa, sio? Aisee.
 
Mwalimu tumlaumu kwa jambo moja tu.
Katiba.
Mwalimu alikuwa na kila uwezo wa kuhakikisha anaacha katiba bora kwa ustawi wa Taifa,lakini pamoja na yeye kutambua ubovu wa katiba,hakufanya jambo lolote kutoa huo ubovu.
Watu wajinga hata uwashushie katiba kutoka mbinguni haitawasaidia!
Elimu kwanza, wakishaelimika wataandika katiba yao wenyewe. Unadhani leo wanaiozungumza na kuielewa haswa habari ya katiba ni asilimia ngapi ya watanzania?

Marekani kura ya wananchi (popular vote) haimpeleki mgombea wa kiti cha uraisi madarakani.
Kwa ufahamu wangu hakuna nchi yenye katiba bora, ila kuna nchi zenye watu walioelimika haswa, mf. China katiba ya kibabe (tena pengine mwalimu alikuwa influenced huko) lakini mambo yanaenda kwa kasi mpaka wamagharibi wanaachama midomo. ELIMU ELIMU ELIMU nakuita mara tatu, shuka tanzania utukomboe!
 
Nyerere alikuwa na mapungufu yake ndiyo kama hayo uliyoyasema lakini kwa kiasi kikubwa alifanikiwa katika mambo mengine mengi na akang'atuka. Shida kubwa ya taifa letu, kama ilivyo Kwa mataifa mengine mengi Afrika, ni mfumo wa umasikinishaji jamii. Uongozi hauko radhi kuachia wananchi wake wainuke kiuchumi. Kwa hiyo mambo mengine yote ambayo yanaweza kumuinua mwananchi kiuchumi yanaminywa. Ndio maana inapotokea Kuna fursa za kuinuka kiuchumi kupitia mitandao kama YouTube basi inaweka kodi kandamizi; hata ikitokea la kutokea mchicha ukawa unapiga hela za export utasikia kuna bodi ya mchicha imeanzishwa na lazima exports za mchicha zipitie huko halafu mara walima mchicha hawapigi tena hela.
Kuna wasomi wametafiti hizi mambo wakaandika kitabu kinaitwa "Why Nations Fail" kama bado ni vema ukakipitia.
Nyerere alikuwa visionary sema vision yake ndiyo ilikuwa chenga. Alitafsiri vitabu vya ujamaa na kuvisambaza. Walau yeye aliamini ujamaa na kusambaza itikadi. Sasa hivi viongozi wetu hawaja-solidify nini wanakiamini wala kusambaza itikadi zao kama Nyerere. Ipo haja ya kufanyika Kwa juhudi hizi kama kutafsiri baadhi ya chapisho na vitabu na kusambaza Kwa wananchi pamoja na wanafunzi mashuleni ili kuwajenga wajue mambo yalivyo. Kutegemea shule za kata tu haitoshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…