Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Kwahiyo mtu akija kwako kutaka kuchukua ardhi yako utamchekea??utakua mpuuzi wa namna gani.
Hamna alio vamia ilikua propaganda za nyerere kujustify vita yake ya kumsaidia rafiki yake pan afrcanist obote kwa kuumiza watanzania hamna tulicho pata kwenye hiyo vita kabisa.
 
Huu ndio ukweli na Huwa nasema mara nyingi na alifanya hivi makusudi Ili asipate Changamoto ya kutawala.

RC ndio walikuwa wanamsaidia kufanyia umafia Wapinzani wake na mda wake mwingi alikuwa anakaa kwenye makazi ya wamisionari/Kanisa.

Unaacha kuwapa Elimu na kujenga uchumi wa watu wako unatumia rasilimali watu na Fedha eti kukimbia Mataifa mengine Bure kabisa Kwa maelezo ya kindezi eti Waafrika ni ndugu,hovyo kabisa.

Kama.sisi ni ndugu mbona tunapenda Kwa viza kwenye hizo Nchi mnazoita ndugu zenu? Watu wanaongea kireni wewe unasema ni ndugu zako.Eti ooh wasipokuwa salama na sisi hatuko salama,si ulinde mipaka Yako?

Hayo yote plus ujamaa mentality ndio yamezaa Taifa la watu walalamishi wasiojitambua.
 
Ndugu uthibitisho upo mkubwa tu kuonesha Tanzania ni taifa lililojengwa kwenye misingi ambayo siyo ya elimu.

Tunaona kabisa eti kiongozi wa kisiasa kigezo chake ni kujua kusoma na kuandika tu? Halafu kiongozi huyo ndiye anayetunga sheria!!!!

Huoni limejengwa taifa la namna gani?

Nimetoa mifano mingi tu. Kuna mikoa mingi mno hakukuwa hata na shule moja ya sekondari. Just imagin mkoa mzima hakuna shule ya sekondari.

Pili vijiji vingi tu wananchi walishindwa kusoma elimu ya shule ya msingi kutokana na kukosekana kwa shule. Na wengine walikufa kutokana na umbali wa shule. Yaani kata moja inakuwa na shule moja ya msingi tena iliyojengwa na wakoloni.

Hivi na jambo hili unataka kusifu? Kama mtu ali fail lazima tuseme ili tuweze kujua tulipoangukia.

Matokeo haya tunayoyaona ya vijana kuwa machawa ni ukosefu wa Elimu na mwasisi wa jambo hili ni Mwalimu Nyerere.
 
Huyu ndio rais aliyeweza kulinda rasilimali zanchi kama leo hii rais ndani ya miaka 2 tu kashauza kila kila kitu tukimpa miaka 20 hii nchi itakuwa sio yetu tena tutarudi kwenye ukoloni
Juzi mtoto wa samia kaongoza ujumbe kwenda kwa Museveni, hatujui aliongoza ujumbe kama nani. Nyerere angeongoza kwa style hiyo, hawa kina samia hata hii misitu iliyopo wasingeikuta.
 
Kabisa kabisa !!
 
Kumlaumu Mwalimu hakusaidii kitu. Kunakosaidia ni watu kwenda shule na siyo tu kwenda shule ni kupata elimu bora na kuitumia vizuri. Kulalamikalalamika tu hakusaidii kitu mpaka mwisho wa dunia. Ni kama mtu aliyeibiwa pesa kila mara aseme tu ameibiwa na asifanye jitihada za kutafuta pesa zingine, unadhani kulalamika huko kutarejesha pesa zilizoibiwa? Jibu ni hapana. Hivyo, tujifunze kuona matatizo ndiyo, lakini jambo muhimu zaidi ni kutafuta njia za kuyatatua hayo matatizo. Hiyo ndiyo njia ya mafanikio.
 
Asante kwa uchambuzi mzuri..
Hoja yako ni shule za sekondari au shule za msingi kama mada yako ilivyoanza?

Mimi ninaamini,kama ambavyo viongozi wetu wanatuambia siku zote, "Taifa halijengwi siku moja" kama hayo ni ya kweli,basi muasisi nae alifanya sehemu yake,waliofuatia nao wamefanya sehemu yao,maana hatujafika mwisho ndiyo maana hadi leo bado shule zinaendelea kujengwa.

Viongozi kujua kusoma na kuandika,ni jambo tunaloweza kulisahihisha hata kesho tukiamua,halihiitaji kumlaumu mtu aliyeongoza miaka mingi iliyopita.

Kwa ujumla Taifa hili ni letu sote,tukihitaji kulifanya kuwa Taifa bora ni sisi,tukitaka kuendelea hivi tulivyo bado ni maamzi yetu sisi hao hao
 
Kweli tatizo ni watu wenyewe ulafi umezidi sababu ya kutomjua Mungu na pia Ulimbukeni wa kutaka kuwatambia wengine !!
Hata ukilimbikiza mali kiasi gani bado hutotosheka na hutoridhika !
Sisi wanyamwezi huwa tunasema The bigger your income the bigger your problems !!
Kuugua utaugua, kufa utakufa tu na zaidi ni kwamba mtu anakosa kabisa amani katika nafsi yake ! Hata appetite inatoweka ! Mwacheni Mungu aitwe Mungu πŸ™πŸ™πŸ™
 
Matokeo ya kutofundisha Historia ya Nchi madarasani ni haya....
Hivi waliokataa Somo la Historia ya Tanzania walikuwa wana misingi gani?
 
Nimeongelea kuna baadhi ya nchi walijenga misingi ya nchi zao katika elimu. Nchi yetu haijajengwa kwenye misingi ya elimu.

Nyerere alikuwa ndiye mjenga msingi wa nchi. Msingi wa nchi umejengwa mbovu. Taifa la watu wasiojiamini, taifa la watu wasio na elimu.

Ilikuweza kujenga taifa imara ni muhimu kutambua makosa yaliyofanyika huko nyuma, nasiyo kuyafumbia macho na kujifariji kwa vitu visivyo na tija.

Tukitambua kuwa msingi wa taifa letu umejengwa vibaya ndipo tunaweza kuubomoa msingi huo na kujenga taifa imara la wasomi.

But tukitukuza hata vitu hivi vya ovyo tutakuwa hatujengi taifa letu. Lazima tuseme ukweli kuwa Nyerere ailiharibu taifa letu.
 
Yeye alijitahidi japo kulipambania taifa hili, je wewe umefanya Nini mpaka Sasa? Compare and contrast.
Kwani unayemlaumu huyo amewahi kuwa Rais wa kwanza wa Tanzania?

Tunamuongelea Nyerere kama Rais wa kwanza wa Tanzania. Alijenga raifa la namna gani.

Taifa lilivyo sasa hivi ni failure yake.
 
Niambie Nyerere alijenga shule ngapi za msingi?
Kipindi kile cha uhuru idadi ya watu ilikuwa ni milioni tisa tu ! Sehemu kubwa ya Nchi ilikuwa ni mapori tu !

Shule zilijengwa kila sehemu palipokuwepo watu na zahanati pia zilijengwa kila mahali palipokuwepo watu !
Huduma zote za elimu na afya zilitolewa bure kabisa tena mpaka vitabu madaftari chakula na madawa yalikuwa ni bure !
Tulikuwa pia tukipewa warrants za kusafiria kwenye mabasi na treni kwenda na kurudi popote pale ulipokuwa umepangiwa kusoma !!
Acheni kukaririshwa uongo, Mwalimu alikuwa ni binadamu na alikuwa na baadhi ya mapungufu lakini Mwalimu alikuwa na nia njema kabisa na taifa na wananchi wake ndio maana hakujilimbikizia mali na wala hakuwapendelea familia yake !
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu !!
 
Chukua Pepsi unywe ndugu. NAKAZIA πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ”¨πŸ”¨πŸ”¨
 
Kwani unayemlaumu huyo amewahi kuwa Rais wa kwanza wa Tanzania?

Tunamuongelea Nyerere kama Rais wa kwanza wa Tanzania. Alijenga raifa la namna gani.

Taifa lilivyo sasa hivi ni failure yake.
Kipindi chake kulikuwa hakuna ufisadi ! Failure ya nchi hii na nchi zote za Africa ni kwa sababu ya UFISADI !! Hata Olusegun Obasanjo alilisema hili mbele ya wakubwa wenzake !!
 
Kati yangu na wewe nani anadanganya?



Naomba unipatie statistics za shule za msingi mpaka 1985 na idadi ya vijiji.

Vilevile nitajie idadi ya kata na shule za sekondari mpaka kufikia 1985.

Ndugu kuna mikoa haikuwa kabisa na shule hata moja ya sekondari.

Ndio maana nikasema kipindi cha Nyerere kusoma ilikuwa ni bahati na siyo haki ya mwananchi.

Ndiyo maana ndani ya katiba iliyoundwa kipindi cha utawala wake, hakuna sehemu imeeleza wajibu wa serikali kuwapatia wananchi wake elimu.
 
Kipindi chake kulikuwa hakuna ufisadi ! Failure ya nchi hii na nchi zote za Africa ni kwa sababu ya UFISADI !! Hata Olusegun Obasanjo alilisema hili mbele ya wakubwa wenzake !!
Niambie nini ilipelekewa mwalimu Nyerere akaandika kitabu cha tujisahihishe kama kulikuwa hakuna ufisadi?

Halafu niambie sababu gani ilisababisha kukawa na azimio la arusha kama ufisadi haukuwepo?
 
Hapa naunga mkono 100%. Unafiki ulioje kusema katiba yetu inalinda dikteta lakini huchukuo nafasi yoyote kuzuia hilo, singlehandedly alikuwa na uwezo wa kutupa katiba bora ya muda wote.
Hata Mimi naamini hilo ndilo lililokuwa kosa lake kuu ambalo hata huko alipo atakuwa analijutia !! Kama mkapa alivyojutia kuviua Viwanda alivyovikuta !!
 
Niambie nini ilipelekewa mwalimu Nyerere akaandika kitabu cha tujisahihishe kama kulikuwa hakuna ufisadi?

Halafu niambie sababu gani ilisababisha kukawa na azimio la arusha kama ufisadi haukuwepo?
Ulikuwepo udokozi sio ufisadi !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…