Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Kwa elimu hakufeli kwani baada ya Uhuru alipeleka watu wengi kusoma ubinafsi wetu ndio tatizo .
 
Nyerere hayupo tena, kama mmeshindwa kutatuta changamoto zenu kwa sasa jilaumuni wenyewe.
 
Hili ndio tatizo na ndio lilitakiwa kuwa bandiko la mada. Mtuhumiwa wa pili ni Ccm, mana baada ya Nyerere kuondoka wanaofuata wote ni vile vile.
 
Yani umeitafsiri UPE kimtaani taani kama wale wanaotafsiri SU - soma ule..
 
Hayo yote hayakusaidii. Pambana na hali iliopo sasa ili kuwe na kesho bora kwa wanao. We umekalia kumlaumu marehemu tu itakusaidiaje kwa mfano?
Nyie ndio ambao mnataka wakina Mbowe waandamane on your behalf huku nyie mmekaa tu kama mazombi.
 
Hoja ya kipumbavu kabisa.

Hivi karne hii lugha nayo ni shida?

Watanzania wameshindwa kufanya nini kwa sababu ya kutokujua kingereza?

What an idiot.
Huyu jamaaa nimpumbavu wa mwisho na ndo hahaha hawahawa unakuta ccm imewaweka mbele waje kujibu hoja za bandari,,,,,mkorea anakuja juu kitekinolijia je anatumia lugha gani???mhindi juzi karusha kiroketi mwezini vip Ali alirushia kingereza???mtazame mchina anavoukimbiza ulimwengu je anatumia kingereza??mtazame mfaransa mtazame mjerumani,,,,,tena ktk maeneo tunawapoteza watoto wenye vipaji niswala lakwamba mtoto akifika secondary abadilishe lugha
 
Kawaida ya watu wavivu hutafuta sehemu ya kutolewa lawama zao.
 
Ndugu yangu. Mimi nipo pale pale tu.
Sijahama kokote naongelea Elimu.

Unaongelea ubora wa elimu!!!! Nakushangaa sana ndugu yangu unapoanza kuwalaumu viongozi wa sasa hivi.

Nyerere hakuweka dira ya elimu kwa Tanzania. Watu wengi waliosoma kipindi cha Mwalimu eidha walikuwa chini ya shule za kidini au walipata support kutoka kwa viongozi wa dini.

Ndugu yangu sijui umri wako na sijui ni wapi wewe umekulia.

Nimekuoa mifano mingi tu, na kwa hali ilivyo sasa. Mikoa kama ya Kilimanjaro na Kagera iliweza kuwa na wasomi wengi kutokana na kuwepo kwa shule zilizojengwa na wakoloni.

Mikoa mingine kama Lukwa, Kigoma, Lindi nk watu walikuwa duni hawakuweza kupata elimu. Matokeo yake watu wa huko hawana elimu na wanaishi tu.

Je, ilshinda nini kujenga shule za msingi kila kijiji na kuachana na kujenga ofsi za chama?

Ilshinda nini kujenga vyuo vya ufundi stadi kila mkoa na kuachana na kujenga viwanja vya mpira?
 
Mzee kuacha madini kisha kuacha taifa lisilo la elimu ya kuyachimba hayo madini tuite ni nini hiyo?

24yrs umeshindwa kusomesha watu wako waweze kuwa na utaalam wa madini tunaita ni faida? Ilimshinda nini kujenga vyuo kila mkoa na ndanj yake wanafundisha taaluma ya madini? Kwanini aliweza kujenga viwanja vya mpira kila mkoa?

Ukweli ni kwamba elimu haikuwa kipaumbele kwake.
 
WATU HAWATAKI KABISA MUNGU WAO NYERERE AGUSWE🤡

Mkosoe Mwinyi wataona sawa, mkosoe Mkapa napo sawa, mkosoe Jakaya napo sawa, mkosoe Magufuli pia sawa, mkosoe Samia pia wanao sawa anastahili kukosolewa tena sana ila mkosoe Mungu wao mchonga meno uone jinsi watavyoweweseka na kugadhabika🤡 kweli propaganda za mchonga kuwa ni mtakatifu zilifanya kazi na zinafanya kazi 🤡
 
Kipindi cha Nyerere ambapo watu walikuwa wajinga na leo nyie werevu mmefanya nini ?

Hao wanaolikoroga huko juu ni wajinga ? Au unataka mkulima / peasant kijijini anayetimiza wajibu wake kutulisha afanye nini ? Aandamane ?

Elimu unapewa au unaitafuta ? Bora kipindi kile kuna grant leo hii hata ukiwa vizuri kichwani huenda unakosa so called mkopo....

By the way don't let schooling interfere with your education..., mambo yanabadilika elimu ni wewe kuweza ku-deal na mazingira yako na watu wenyewe huku chini wanatimiza wajibu wao wanaotuharibia ni hao so called educated waliobadilika kuwa madalali
 
Kipindi cha Nyerere ile education for self reliance ilikuwa ni bora kuliko hizi elimu za phd za kukwapua !! Dili dili kila kona !
 
You nailed it. ! 🙏🙏
 
We dogo Venus Star , una jina zuri la nyota ya Zuhura ila tatizo ni akili finyu!

Baada ya kupata uhuru, ile 1961 Mwalimu Nyerere alipambana sana
1. UJINGA
Elimu ilikuwa inalipiwa hivyo walioweza kuendelea na masomo ni watu wa mikoa yenye mazao ya biashara pekee, Mbeya, Bukoba, Arusha na Moshi - Kahawa. Tanga- Katani, Mwanza - Pamba. Tabora- Tumbaku. Mikoa isiyo na mazao ya biashara, Singida, Dodoma, Pwani na Kusini, ni Shule za Mission zimeokoa jahazi!.

Mwalimu akatangaza elimu bure mpaka chuo kikuu!.

Akakuta wanaofaulu na kuingia sekondari ni watoto wa makabila yale yale the big 5, Wachagga, Wahaya, Wapare, Wanyakyusa, na Wasukuma

Akabadili cut off points za kuingia sekondari kwa mikoa tofauti tofauti ili kila Mtanzania asome.

Baadhi ya makabila ya bushmen kama Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, walikamatwa kwa nguvu na kusomeshwa chini ya ulinzi mkali hadi form IV wote waliishia kupata zero, na waliporudishwa kwenye jamii zao wakazibadili.


Mwalimu Nyerere akaanzisha elimu ya watu Wazima kisomo cha ngumbaro Luna wakati Tanzania ndio tulikuwa na the highest literacy levels Africa!.

Mwalimu alianzisha Elimu ya Kujitegemea, Elimu ni Kazi etc ili Watanzania waelimike.
2. UMASKINI
Mwalimu alianzisha kampeni mbalimbali za Siasa ni kilimo, kilimo cha kufa na kupona, Vijiji vya Ujamaa, alitaifisha kila kitu kuwa mali ya umma, akaanzusha viwanda kila mkoa.

3. MARADHI

Mwalimu Nyerere alitoa bure huduma za Afya.

Tulikuwa tunakwenda vizuri mpaka yule mshenzi nduli Amini alipotuvamia ile 1978 Taifa likaingia vitani kwenye vita vya Kagera ndio sasa tukaharibikiwa.

P
 
NAKAZIA NA KUKAZIA KABISA
 
Mwl alifeli pia kwa kukitukuza kiswahili na kukipromote kuwa lugha ya taifa .
Tunetengeneza taifa ambalo lipo isolated sana na dunia. Watu wanahitaji akina mkandara kutafsiriwa cnn english news.
Warusi wanaongea Kirusi, wachina wanaongea kichina kwanini sisi kuongea kiswahili ionekane ni kosa
 
Niseme japo kwa kifupi kuhusu lawama zako kwa mwalimu hayati JK Nyerere juu ya elimu ya Tanzania.

Mwalimu alipokea nchi toka kwa wakoloni ikiwa na kundi dogo sana la wasomi, na kundi jingine dogo la wanaojua kusoma na kuandika tofauti na majirani zetu.

Kazi ya kwanza ilikuwa ni kupunguza kundi la wasiojua kusoma na kuandika ambalo lilikuwa kubwa zaidi.

Akawa na kazi ya pili ya kuwasomesha vijana watakaosaidia katika idara nyeti kama madaktari na wahandisi. Kumbuka nafasi tunapopata uhuru zilikuwa zimeshikwa zaidi na wageni japo na wenyeji kidogo walikuwepo.

Haikuwa kazi rahisi kwa uchumi wa wakati huo kutoa elimu ya juu kwa watu wengi. Lakini alipambana kujenga shule za msingi,sekondari na chuo kikuu ili kuongeza idadi ya wasomi.

Alitumia wasomi wa idara mbalimbali kama walimu katika maeneo yao. Kwa mfano walimu mahali popote walipo walitakiwa kufundisha si tu wanafunzi, bali hata watu wazima katika eneo hilo japo wajue kusoma na kuandika.

Aliandika vitabu vya elimu ya watu wazima kwa mkono wake na wadau wengine, vikiwa na taaluma mbalumbali kama upishi, ufundi nk.

Kama haitoshi, ili kukuza kwa haraka elimu kwa wananchi, alianzisha mpango wa UPE (universal primary education), mpango ambao umerudiwa na Rais Magufuli. Mpango huu ndiyo ulioipa Tanzania sifa ya kuwa na wananchi wengi wanaojua Kusoma na Kuandika katika bara la Afrika mwishoni mwa miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa miaka ya 80.

Kifupi mwalimu alipambana sana kuiinua Tanzania. Kumbuka haikuwa rahisi kutokana na mabeberu kuwakandamiza waafrika kupunguza kundi la wasomi wasijeleta upinzani wanapotaka kutunyonya.

Kama unaweza kujifunza, jifunze kwanini viwanda vya vyetu vilijengwa kisha vilikufa kwa haraka sana. Moja ya sababu ilikuwa ni kukosa vipuli na nguvu kazi (wataalam) kutokana na wazungu kugoma kuendeleza wataalamu wetu na kutuuzia vipuli.

Kama siyo juhudi zake Nyerere, tungekuwa na maisha kama ya Kenya. Sipati picha ingekuwaje.


Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Najua ndugu yangu Pascal Mayalla bado kumbukumbu unayo baada ya kukutandika kwenye andiko lako la kuwalaumu TEC huku ukitumia andiko la kwenye biblia. Ninauhakika ulijifunza kitu.

Sasa turudi kwenye mada hii.

Mwalimu Nyerere alikuwa ni mzuri sana wa kuanzisha misemo, lakini kwenye utekelezaji ilikuwa big zero.

Swali langu kwako ni dogo tu. Je, Mwalimu ilimshinda nini kujenga shule za msingi kila kijiji na badala yake akajenga ofsi za chama?

Halafu Nyongeza, hivi lengo la UPE ilikuwa ni nini? Kweli alishindwa kuchukua vijana kumi kumi kila kijiji na kwenda kuwasomesha kwenye nchi rafiki? Maana kama una vijiji 20,000 ukichukua vijana 10 kila kijiji utakuwa na wasomi wa ualimu 200,000.

Cha mwisho, ilimshinda nini kujenga shule za ufundi kila mkoa na badala yake kujenga viwanja vya mpira wa miguu?

Hitimisho, Nyerere hakuws na lengo zuri la elimu kwa nchi yetu.
 
Ukabila gani alioukuta?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…