Ukweli usemwe: Joseph Haule (Profesa Jay) anahitaji utulivu, hizi pilikapilika za muziki na siasa angeachana nazo

Usipangie wati namna yao ya kuendesha maisha
 
Kuna video niliona jamaa analia kwenye kona yake, vitasa noma.
 
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Eeh maisha ya mwanaume ni kutafuta tu, unazaliwa unatafuta elimu, unatafuta maisha kwa kutafuta hela, unatafuta mali, unatafta mwanamke, unatafta watoto, unatafuta nyumba, unatafuta gari, unatafuta magonjwa ,unatafta kuuguzwa yani we ni kutafuta tu mpaka utapokutana na kifo.
 
Prof Jize bado ana vitu vya Ku offer so aendelee kupambania legacy

Ushauri wako ni mzuri Sana .
Ila pia Kama kuongea Anaweza aendelee kupambania legacy yake.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 aisee nimecheka sanaaaa dah kashata za nazi zimemtoa utu mtu
 
Mkisema anatafuta mkate wake na familia yake ina maana huko nyuma na ubunge hakupata fedha za kuishi muda mrefu bila kufanya hizo kazi tena? Anahitaji kupata utulivu muoneeni huruma. Yule si hohehahe kiuchumi mpaka arudi mbilingeni, huko ni kujitaabisha kulingana na hali yake ya kiafya aliyonayo
 
Ni kama unaishi nje ya tz mkuu hivi unaelewa pesa unavyochomoka kama sungura isitoshe kuumwa . The world doesn't stop cause something show up.
 
ha
Ni kama unaishi nje ya tz mkuu hivi unaelewa pesa unavyochomoka kama sungura isitoshe kuumwa . The world doesn't stop cause something show up
Hajawahi kuuguza hata mgonjwa wa malaria huyu ndio maana hajui ni namna gani maladhi yanafilisi,siku 400+ kitandani hajui ni usiku ama mchana anadhania mchezo mchezo tena figo,yeye mwenyewe akienda hospital akipewa bili laki tu ananena kwa lugha kisa hela nyingi ,kalaki tu,ili hali mwenzake ilikuwa inateketea zaidi ya 8M kwa siku
 
Mwache atafute ugari wake,siasa ndo kazi yake.Ila prof dhis time ukipata ubunge jipange ndugu yangu najua unajua nini cha kufanya.
 
Kwa mara ya kwanza tangu nikujue leo ndio umeongea point
 
Akamatwe mara moja na kufungiwa ndani takriban miaka 10 au zaidi mpaka afya yake itakapotengemaa.
 
Mungu ndiyo anajua hatima ya kila mtu ,inawezekana ukaona kama Prof yupo dhaifu kwa mtazamo wako kumbe akawa imara kukuzidi wewe unayejiona hupo fit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…