Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Kama ile kesi ya MWANA FA NA AY mpaka wakalipwa BIL 2 sijui na tigo ina maana ukitumikaa wimbo bhasi ndo haki ya msanii kulipwa ila likitumiKA BEAT tu bhasi haki ya producer kulipwaa... ngoma ngumu snaa hii 😀 😀 😀
Mkuu huwezi Jua labda hermy B alilipwa na washikaji.

Au aliuza beat na Kila kitu kuhusu hio beat.

Haya mambo huwa yanatokeaga na wasiojiandaa mapema na mikataba yenye kulinda haki zao huishia kulilia tu.

Wasaniii waache njaa njaa wanunue nyimbo na haki hio nyimbo na Kila kitu

Ila yanapotokea mazali kama haya ya ma movie kutumia nyimbo na beat zao wapige pesa.
 
Nafikiri waliingia mgogoro na Prof. Jay baada ya P. Funk kuchukua hela kwa kampuni ya movie iliyotumia beat ya bombo clat ambapo original ni beat ya nikusaidiaje. Profesa alilalamika kuwa hakupewa hata senti
Jamaa aliweka pesa yote mfukoni[emoji28]. Halafu si ilikia milioni mia!
 
Killer alisepa miez sita tuuu,. Alipoona chenga akachora
 
Maelezo mazuri kabisa P funk ndio mwenye haki na beat

Jamaa mmoja katoa mfano mwepesi sana huko juu na unaeleweka.

Yaani "TOYOTA ikikuuzia wewe crown ukaenda tambia mademu au ukaisajili Uber upige Hela huwezi kuwazuia kumuuzia jirani Yako nae crown nae akapige Hela au akat.om.bee mademu.

Still Toyota wanabaki na haki ya ubunifu wa Crown

Gari ni Yako lakini ubunifu ni wao."

Easy tu
 
Tatizo njaa kaka, ukishashiba ndio udaana kupata akili ila njaa ikikupiga unawaza hela ya kula na kumantain jina
 
yaah sema ndo hivyo sijui nani ana mmenage maana bila hivyo atapotea bila kufaidi pesa zakee..sioni akipiga show akati ndo muda wenyewe..!! apate manager kichwa azungukee aisee kuzikusanyaaa amezubaa sanaa...

Management yake ipo vizuri kwenye kutoa kazi ila kitengo cha kumbrand na kumpa promo marioo naona pamelegea kidogo

Niliona kaenda kupiga show kenya lakini sikuona media tour kwenye vipindi vyenye fan base kubwa kama 10 over 10, wakati kenya kashapenya, ilitakiwa akite mizizi maana naskia hata hela ya show kenya, wabongo hulipwa vizuri kuliko home
 
Ingawa threads zako huwa ni za kichawa ila leo nakuunga mkono. Uko sahihi katika hili suala la P Funk. Hawa wakongwe wamenyonya sana wasanii ikiwemo kuwadhalilisha. P Funk ni kweli ana tuhuma za kuwapiga wasanii. Shukrani nyingi kwa kijana wa Tandale kwa kuleta mapinduzi makubwa na kuwapa wasanii heshima wanayostahili. Kwenye huu muziki naweza sema Diamond ni kama NABII.
 
Brother weka taarifa zako vizuri...

Wasanii wote unwaona Nature na wengine ambao album zao walirekodi kwa majani kasoro Prof J wote hakuna album hata moja wanapata hata 50 kwa sasa zote ukiingia copyright utaona Bongorecords na mzigo unaenda huko.

Kuhusu WCB kukata 60/40 aisee mbona hapo wamewasaidia wasanii bro...hivi unamchukua mtu hajulikani unamlea unampa kila kitu kisha wewe kukata 60% useme ananyonywa? Wakati pesa ya kurekodi inatoka hapo kwenye 60,mavazi na video,promo zote kwenye 60. Niambie msanii gani ukimtoa Ali kiba,Nandy(ambao walikua na backup kubwa ya clouds) anaweza kushindana na msanii wa WCB kiuchumi? Usiseme Harmonize maana yeye ametoka huko..leo hii ukisikia Harmonize kaweza kulipa 600M na Ray 800M kuvunja mkataba utasema walikua wananyonywa kama ni hivyo pesa yote hiyo wamepata wapi?

NB:WCB wana udhaifu lakini wana unafuu
 
Baada ya kushinda kesi, Hermy B akawaambia beat atakuwa anawauzia milioni 8, wakakasirika mpaka wakagombana nae kabisa😃😃 wao wanataka wawe wanalipa laki 5 mpaka single milioni
Kwahiyo Msela[Harm B ]hakulambaga kitu
 
Mkuu umeongea point sana! Mara nyingi watu huwa wanafanya vitu kienyeji halafu ikitokea dili ya hela ndio wanastuka kwamba waliuza game. Kingine kilichochangia ni biashara ya muziki kubadilika, zamani publishing haikuwa big deal kutokana na jinsi muziki ulivyokuwa unauzwa. Lakini siku hizi music publishing is a HUGE business hasa baada ya muziki kuanza kuuzwa digitally. Na ndio maana licha watu kumtukana P Funk, jamaa alishtuka mapema akahakikisha haki zake za publishing zimesajiliwa kisheria na sasa hivi anakula matunda ya jasho lake. Hata Master Jay kwenye interview na Salama alimsifu kwamba jamaa kawaonyesha producers wengine jinsi ya kulinda maslahi ya ubunifu wao.
 
YANI anakwama sana kuhusu show jamaa atashuka umaarufu hajapiga show za maana
 
Hakulamba kitu. Ila hata kina Mwana Fa wenyewe ni kama walichukua nusu ya hiyo hela, nusu nyingine aliichukua wakili wao (Msando) kwa kuwa wao walikuwa wameikatia tamaa kesi na yeye ndio akawekeza akiamini kuwa wanatoboa na kweli wakatoboa.
Kwenye hizo 2b angekuwa producer mwenye akili angekuwa na chake na hapa ndio p funk na Master J utawapenda.
 
Watu mnachanganya publishing na management. Hicho ulichokitaja hapo ni mkataba wa management, hauhusiani na publishing. Hiyo biashara ya sijui 40/60 au 30/70 huwa inakuwa kwenye management. Mkataba huwa kwamba kwa mapato fulani au yote yatakayoingia wakati wa mkataba huo wa management, msanii atapata 60% na management itapata 40% or vice versa or whatever the agreement says. Hiyo haihusiani na chochote kuhusu hatimiliki (publishing). Hatimiliki ni kitu kingine kabisa.

Unaposema Juma Nature hapati 50% unataka hiyo hela aipate on what basis? Ninachojua mimi Nature sio msanii wa Bongo Records siku nyingi. Meaning hata yeye akifanya shoo na akatumia nyimbo alizorekodi Bongo Records hatakiwi kumlipa P Funk kwa sababu sio msanii wake kwa sasa.
 
Nadhani hujafahamu mfumo waubepari unayofanya kazi.
Huo ndio ubepari Sasa...na hakunyonyi sababu aha roho mbaya ila sababu ndivyo inavyostahili.
Kwa nini hao wasanii walienda kwake na wasingejisikia huru kwenda kwenye label nyingin?
Kwani yeye hivyo vifaa vya studio aliokota,? Ujuzi je alisomea bure??
 
Mtoa mada jitahidi kujua namna haki zinazofungamana na mziki zipo vipi na ni nani na nani wanaotakiwa kufaidika na muziki fulani utakua umemaliza kila kitu.
P Funk yupo sahihi, Sallam ameghafirika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…