Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Mkuu hili unalosema SIO KWELI ukifuatilia mapato ya mirabaha ambapo pesa zimegawanywa kulingana na umiliki wa % katika wimbo husika, hao wasanii wakongwe pia wamepata. Sio kwamba Majani amejimilikisha 100% bali ni 50% kwa nyimbo ambazo aligharamia na aliingia mikataba na hao wasanii
 
P
Pia dunia nzima hakuna professional studio ambayo ina mtu mmoja tu yaani wimbo ufanywe na kukamilishwa na producer pekee. Hapo kuna music engineer, mastering, composer, mixing and dubbing, nk yaani unakuta wimbo mmoja una mikono ya watu hata sita tofauti lakini anayetajwa kama producer huwa ni HEAD OF THE OFFICE.
Ipo hivyo
 
Mkuu hili ninaongea nikiwa na uhakika wa 100% ni kuwa pale WCB ukiachana na Mavoko na Konde boy, nyimbo za wasanii wengine wooote waliobaki zinamilikiwa na WCB hao ndio COPYRIGHT HOLDERS, wasanii wamebakiwa na PERFOMANCE RIGHTS ONLY yaani leo Vanny akitoka pale basi hawezi kupata hata 100 endapo wimbo wake utauzwa, nasema HATAPATA HATA MIA WIMBO WAKE UKIUZWA unless otherwise waingie makubaliano mengine leo hii kuhusu hicho kipengele.
 
sema ndo hivyo wasanii wanakuwa hawana kitu mfukoni so lazima producer abakie na uhalali wa kumiliki beat... ila kwa msanii kama DIAMOND now hawezi fanya huo ujinga
 
Mwisho wa siku beat inakuwa Mali ya producer
Lyrics msaniii

Ova
 
Wakati hao wasanii wanasaini mkataba hawakuona vigezo na masharti?
Ktk issue ya mikataba lazima uwepo upande utakaoumia na hasa kwa msainishwa kutokana na wenye mikataba hupenda kuangalia na kupima upeo wa anayesaini ukionekana mwepesi unapigwa kitu kizito.

Mf;anachozungumza mdau hapa kilifanyika siyo chini ya miaka 15/20 iliyopita sasa unadhani ktk wasanii wetu wa kipindi kile ni yupi angalao alipata wazo la kusema ngoja nimshirikishe mwanasheria ktk huu mkataba?na hata wakisema watake kuuvunja leo lazima zipo chamber zinazowabana either kutoa kiasi cha pesa kuivunja hiyo mikataba unadhani leo afuatwe Ferooz kwamba toa 100Mill umlipe Majani mkataba uvunjwe hiyo pesa anayo?
 
Noma sana pia nahisi haya mambo hawafanyagii kwa mkataba tu inakuwa kwa maneno.. labda kama mkifanya album ila kama single tu inakuwa kisela kwa mdomo of which mbeleni yanatokea haya
Mkuu maneno yakitamkwa na mkakubaliana tayari ni mkataba
 
Hii kweli kabisa nilishangaa kumuona chege akipita mtaani kuzungusha kapu la dagaa ...nikajisemea hii laana kabisa...
chege kwani nae kafulia kiasi hichi mkuu??? nasiki kundi lao nature tu ndo bado ana maisha...
 
Huoni kama hiyo 40percent ni kubwa sana maana hujawekeza hata mia zaidi ya sauti yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sema ndo hivyo wasanii wanakuwa hawana kitu mfukoni so lazima producer abakie na uhalali wa kumiliki beat... ila kwa msanii kama DIAMOND now hawezi fanya huo ujinga
Zama tulizopo dunia imefunguka sana,leo hii msanii hata asiyejua ABC za mikataba akishika simu yake akiingia mtandaoni anakutana na habari za wasanii wa nchi nyengine wanaokula shavu kwa kusimamia vizuri kazi zao wenyewe so wanapata idea hawa huwezi kuwaingiza mikataba ya kijinga.

Wakati wa kina Gwair sijui Nature hao kina Ferooz hakukuwa na nyenzo za kuwapa taarifa na elimu nyeti kama sasa leo unakuta msanii ana baba ana elimu kichwani,mjomba sijui mume wa dada wote wanakuwa washauri wake karatasi zinakaa kisheria ila kipindi hiko mikataba wanasaini bar tena usiku wamelewa huku mapajani wamekaliwa na kina Kajala na Sinta na mwenzao Masogange unadhani kuna kitu hapo?sidhani hata kama walikuwa wanasoma wanachokisaini.
 
Ndio uko sahihi ila unaweza ujue haki zako lakini bado huna wa kukutoa sababu mziki wa Sasa una mambo mengi mpk mtu atoke Kuna branding za kufa mtu ambazo zinahitaji watu wazoefu kwenye field husika.
Ukiwafuata ndio hivyo wanaweka masharti ya kibepari kama hutaki komaa mwenyewe.
 
Huoni kama hiyo 40percent ni kubwa sana maana hujawekeza hata mia zaidi ya sauti yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijaujua hasa msingi wa mabishano yenu but according to quote uliyom-quote mdau hapo juu bado yeye ana hoja.

Assume wewe leo umekuwa msanii chini ya label tajwa hapo juu,leo 2022 ukashikishwa pen na karatasi kwamba kila utakachofanya ukiwa chini ya mkataba tajwa utalipwa let's say 1mill ukija kuachiliwa mateka wewe baada ya huo muda kwanza hiyo million uliyokuwa unapewa 2022 ni sawa na 200K tu na utakutana na damu changa mtaani zinawika mbaya kabisa na zina management nzuri zaidi yako huku baadhi ya haki zako wakibaki nazo waliokuachia mwanzo.

Nadhani ndo hasa msingi wa hii thread kwamba producer au manager akiingia mkataba na msanii ktk kazi zake huyu msanii nae aendelee kupata matunda ya kazi zake hata baada ya yeye kuwa ameshuka kimuziki na ni matokeo tarajiwa ktk fani yoyote.
 
Mtoa Mada,

Hayo ni masuala ya mkataba. Hao wasanii walikuwa wanajua masharti ya P Funk yakoje na walikubali kufanya naye kazi.

Sasa wewe mtaji wako ni sauti tu unataka ule sawa na mtu aliyeenda jiji la New York (jiji la gharama sana kuishi) kusomea Uhandisi wa Sauti na kununua mitambo na kutengeneza urafiki na ma-DJ wampigie nyimbo za studio yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…