Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Aina shida nitaleta uzi.

Watu hawaangalii kilichowekwa wanatazama kinachopatikana.
Na hawazingatii pia kuna uwezekano kinachowekwa hakitoki kwa mkurugenzi 100% kuna mikopo na third party wengine wanasubiri returns.
 
Yeye profesa J why hakwenda kudai haki yake mapema?? Au hajui kama beat ni haki yake maana alilipia kufanya ngoma??
Wenyewe wataalamu wa production wanakuambia msanii anacholipia ni studio time ila "haki ya ubunifu" inabaki kwa producer. Msanii anaweza kumruhusu msanii mwingine atumie mashairi yake ila sio beat ya wimbo huo bila producer kuhusishwa.
 
Haya ni maswali mazuri mno ila majibu yake ni ngumu unless kama mikataba tungekuwa nayo.
amini boss... maana hii kesi ya beat ya MAJANI...wimbo alilipa PROF J akafanya...REMIX CHAMELEON ila mpungaa kaanza kupewa chameleon then majanii.. prof kabaki mtupu wakati jamaa ni legend na naamini anajua stahili zake na maslahi yapoje kimziki.. safari ni ndefu na ngumu kama hata prof j anapigwa za kichwa hatari
 
Lete ushahidi kuwa Bizman kalalamika kudhulumiwa au co_producers (hao akina Soggy , Lamar..) unaodai hapa kudhulumiwa.
 
Yeye profesa J why hakwenda kudai haki yake mapema?? Au hajui kama beat ni haki yake maana alilipia kufanya ngoma??
Profesa anasema alilipa beat hiyo. Kwamba P Funk alimuuzia hiyo beat na hivyo yeye pia angestahili kupata mgao wa mapato ya hiyo ngoma.
 
Mimi siyo mpemba. Kaa mbali na mimi
 
we jamaa muongo criteria za mkataba uliziona

halafu majani kalalamika wanabanwa wakiwa wanatoka ndio kasisitiza


hivi uliona wapi bongo msanii anatoka kwenye lebo halafu anapata pesa ya kumlipa boss.


mbona alikiba wasanii hawana thamani humuongei bongo ukiendelea chuki iko wazi.



Rayvanny na harmonize wananyonywa ........ au wamemyonya nasibu walivyokuja na walivyo ondoka tofauti sana.
 
Kama ni kweli ni ushetani. Ila sasa tatizo ni uhakika kuwa ni ukweli. Wakati mwimgine mambo yanazungumzwa na kuaminika ni kweli ila ukipewa makaratasi ya mikataba unakutana na mambo tofauti.
 
Kama ni kweli ni ushetani. Ila sasa tatizo ni uhakika kuwa ni ukweli. Wakati mwimgine mambo yanazungumzwa na kuaminika ni kweli ila ukipewa makaratasi ya mikataba unakutana na mambo tofauti.
Noma sana pia nahisi haya mambo hawafanyagii kwa mkataba tu inakuwa kwa maneno.. labda kama mkifanya album ila kama single tu inakuwa kisela kwa mdomo of which mbeleni yanatokea haya
 
Huna akili
 
Hivyo ndivyo P. Funk anavyosema na kuuaminisha umma. Anasema kuw msanii hanunui beat ya produsa bali analipia muda wa studio, beat inakuwa mali ya produsa.

Sasa ili uitwe wimbo, maana yake kuna vocals na beat, kwa pamoja ndio vinafanya uitwe wimbo. Kuna msikikizaji atapenda mdundo na kununua huo wimbo, kuna mwingine atapenda maneno na kununua huo wimbo, ni ngumu kujua mtu anaponunua wimbo anakuwa amevutiwa na mdundo au vocals (maneno) au vyote. Ndio maana mgao huenda kwa wahusika wote wa wimbo, waandishi, waandaaji, waimbaji nk

Hii ishu ya Nikusaidiaje, Jay ndie aliyepambana na Chameleone, tafsiri ni kwamba, P Funk alikuwa ameuza beat yake na akaona ni sawa kwa Jay kulalamika, baadae akamzunguka Jay na kuchukua mpunga kwa wamarekani, ndipo hapo mtafaruku ulipoibuka
 
Kijana wa wcb mishipa imekusimama kweri-kweri.

Jibuni hoja za P.funk kwanini Mbosso halipwi pesa yake kama writer wa mashairi anayomuandikia ya Diamond?

Kwanini publishing rights za producer S2kizzy kwenye platforms zimechezeshwa ili asitambulike kama mbunifu wa midundo yote aliyofanya na wcb kiasi kwamba amekosa malipo yake zaidi ya million 110 ????

Mbosso anasepa soon, kaa mkao.
 
Noma sana pia nahisi haya mambo hawafanyagii kwa mkataba tu inakuwa kwa maneno.. labda kama mkifanya album ila kama single tu inakuwa kisela kwa mdomo of which mbeleni yanatokea haya
Umeongea point.
 
Msanii huwa analipia beat au mastering?
hivi producer si anasikiliza wimbo na idea ya msanii ndo anatengeneza beat?? au msanii anapewa beat aweke mashairi??? maana kama unamlipa akutengenezee beat means utakuwa unaimiliki...lakini pia unaweza nunua beat may b kama huwa hela yake ni mamilion
 
Msanii huwa analipia beat au mastering?
Hapa sijakuelewa mkuu, beat ni mdundo, mastering ni kitendo cha kuufanya wimbo uwe na sauti bora na viwango vilivyokubalika..sasa kwa swali lako jibu linakuwa gumu kidogo kupatikana, kabla ya mastering kuna recording na mixing.
 
noma sana label hizii ukiwa hujatoka ndo unaona zina msaada ila ukishahit ukaanza kuingiza mawe ndo unajua unapigwaaa
 
Mchezo ulikuwa hivi. Chamilion alifuatwa kwa kuwa ulitumika wimbo aliouimba yeye. Ila yeye akafanya uhuni wa kutosema ukweli juu ya nani hasa alietengeneza hiyo beat. Na ndiyo maana P Funk ilimuuma sana hii kwani binafsi yeye anafahamu sheria. Kiasi Cha kuamua kwenda Uganda kupigania haki yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…