Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Shida ni pale kwenye mikataba unapoamua kushuka signato. Maana hawakuwa na hela ya kununua beat so yeye anakuwa anajitolea bit zote wewe unaleta mashaairi. Ofcoz masta itabaki kwa p funk ni business ambayo hata USA wasanii yamewakuta haya ndio maana hata maiko Jackson aliwaambia vijana wahalikishe wanamili masta zao ili wasife njaa Maana hapo ndio kwenye hela. So nadhani hata rayvanny pia masta anazo diamond. So hata Sasa yanatokea muhimu wasanii walate elimu ya kutosha kuhusu mastaaaaa hizo. Pfunk alitumia mwanya Enzi hizo but now still Kuna wasanii hawamiliki mziki wao
Yaah umaskini ndo Chanzo mkui...!! Wengi wanaona kununua beat na mfukoni mweupe hata akisema akope hana kwa kukopaa bora akubali masharti sema Akifanikiwa kama alivyofanya Konde no sawa kujitoa maana kuwa chini ya Label sawa na kuajiriwaa tuu.. Unapiga hela ndefu ilaa unaambulia kidogo na unaweza usipewe kabisa.
 
Wasanii wetu wengi hawajui sheria ya Intellectual Property..

Kimsingi hata maproducer wengi sana wananyonywa na wasanii.. fikiria msanii nyimbo baada ya kurekodi ikatoboa producer huwa anafaidika vipi?

Kimsingi wote wanatakiwa kufaidika.. kama hawakuingia mkataba wa kinyonyaji
Sasa si anakuwa maeshamlipa kufanya nae kazi maana Ngoma ikibuma ni hasara kwa msanii pia.. Ikiitika acha msanii ale bataa shida inakuja kwenye Maslahi mengine kama beat kuuzwa sijui nyimbo kutumika kwenye Movies... hapo ndo utata huja mwenye akili anapita na mpunga kama upepo kuviziana tu
 
Kuna mwaka nilimskia Dullayo akihojiwa ni kitambo kidogo kuhusu Marco Chali na sababu za yeye kusepa kwa Mshkaji, jamaa alkua hadi analia kwenye Interview.

Muda kidogo ukapita akaja kulalamika Godzilah ( R.I.P) kuhusu the same scenario sijui Jamii haikuelewa au ni kupuuza tu, inasemekana na hali aliyokua nayo mpaka Umauti ni msongo wa Mawazo na kukosa Faida bila kujua pahala sahihi za kupata Msaada.
 
Nakumbuka sio movie, ni ngoma sijui nikusaidiaje ile biti akauziwa tena chameleone akaimbuia bomboclat.. Jay kuulizia p kaishakula hela, chameleone akataka kumpa tena hela Prof akaamua wapige kolabo, ngoma nimeisahau jina.
Ni movie, nyimbo ilitumika Bomboclat, beat ni Nikusaidieje ya Proff, Chameleon alilipwa pesa akampa Majani chake kama prodyuza, Proff hakupata chochote ila nadhani baadae alipewa na Chameleon na collabo wakafanya "Ndivyo Sivyo"
 
Music publishing ni ishu tata sana. Sio huku kwetu tu bali hata huko kwa walioendelea. Kuna mifano kadhaa ya wanamuziki wakubwa ambao walitangaza kufilisika (bankruptcy) licha ya "kuuza" mamilioni ya kopi za rekodi. Mfano Toni Braxton, TLC n.k. Lakini huo ni mjadala wa siku nyingine.

Typical music production (unless kila kitu mpaka kuimba amefanya mtu mmoja) huwa inahusisha producers, composers, melody makers, session musicians na engineers. Hawa huwa wanakuwa na haki zinazoitwa mechanical rights za huo wimbo. Ukiangalia hapo sijamtaja mtu mmoja, MUIMBAJI/WAIMBAJI. Hawa wanakuwa na haki za uimbaji (singing right) kwenye huo wimbo.

Tafsiri ya rights zilizotajwa hapo juu ni kwamba kwa namna fulani KILA mtu aliyeshiriki kutengeneza huo wimbo (unless kwa sababu fulani amekubali kufanya bure) anatakiwa kulipwa. Analipwaje ndio mjadala ninaouona kwenye huu uzi. Suala la mshiriki kwenye production atalipwaje huwa liko kimkataba, inaweza kuwa malipo ya mara moja au percentage fulani ya publishing (wenzetu wanaitaga points). Kuna watu wamesema kwamba P Funk amepora haki ya watu aliofanya nao kazi ya production. Tutajuaje kama P alishamalizana nao kimalipo na wakaachia rights zao za publishing? Je, hizo haki zao zimesajiliwa kisheria? Hii ishu nitaijadili kidogo huko mbele.

Again, typical music production huwa inasimamiwa Producer. Kwenye music production kumekuwa na tatizo la watu kuchanganya producer na beat maker au session musician. Kwa kawaida huwa inategemewa producer awe pia musician ili awe na uwezo wa kuendesha zoezi zima la production. Lakini SIO lazima yeye apige vyombo au kufanya programming kwenye huo wimbo unaotengenezwa. Kuna mtu kasema "P Funk hajui hata kupiga kinanda", kwanza sio kweli, P Funk anaweza kupiga kinanda, pili ili awe ame-produce wimbo fulani sio lazima personally afanye beat making, yeye anahakikisha kila mhusika ana-play role yake na standard ya production inakuwa per exellent. Producers wengi wakubwa huko duniani huwa hawapigi vyombo wao wenyewe bali hutumia session musician au beat makers mfano Quincy Jones, Dr Dre, P Diddy, Irv Gotti etc.

Sasa tuje kwenye ishu tata ya hatimiliki aka publishing. Tofauti na watu wengi wanavyoamini, publishing rights sio automatic. Ni lazima ziwe zimesajiliwa kisheria (registered) ili zilindwe, kama umefanya kazi yoyote ya ubunifu bila kuisajili wakatokea wajanja wakasajili imekula kwako. Jamaa watapiga hela huku wewe ukipiga miayo. Huku kwetu nina uhakika kuanzia wasanii, wapiga vyombo na wengineo walikuwa hawalijui hilo ndio maana watu wengi wakiwemo wasanii wanaamini kwamba akienda studio akalipia kurekodi wimbo automatically unakuwa mali yake. Kitu ambacho sio kweli.

Sijajua mikataba ambayo wasanii wa hapa kwetu (wakiwemo wa WCB) huwa wanaingia na lebo huwa ina-address suala la publishing au hapana. Ambacho nina uhakika nacho ni kwamba wasanii wengi (hasa wa zamani) hawako aware kuhusu ishu ya publishing, na ndio mzozo wa Prof Jay na P Funk ulipoanzia.

Actually ishu ya Prof Jay na P Funk kuhusu beat ya nikusaidiaje haikuanzia kwenye beat hiyo kutumika kwenye movie. Baada ya Prof Jay kurekodi wimbo huo na kuhit, Chameleone akamfuata P akitaka atumie hiyo beat, P akamchaji Chameleone USD 2,000. Prof aliposikia akaja juu na kulalamika kwamba beat yake imeuzwa bila idhini yake. Lakini kiukweli Prof hakuwa ma haki yoyote kwa kuwa Chameleone alitumia beat tu, sio wimbo wote. Wimbo wa Chameleone ukaja kutumika kwenye movie ya Queen of Kitwe iliyotengenezwa na Disney na Chameleone akavuta mpunga. P akakomaa na Disney na kwa kuwa sheria ilikuwa upande wake alalipwa. Again Prof hakuwa na haki kwani wimbo uliotumika ni wa Chameleone na sio wa kwake.

Hitimisho ni kwamba music business is very shady, inatakiwa msanii ajifunze SANA sheria za hatimiliki na ahakikishe haki zake ziko documented na zimesajiliwa kisheria ili zilindwe.
Uzi ulitakiwa kuishia hapa
 
Watu ubepari wanauchukulia poa [emoji3][emoji3][emoji3]
Kwenye ubepari hakuna huruma mbele ya maslahi
Kundi la 112 usa lilipotaka kujitoa badboys wakajikuta hadi jina kumbe sio milki yao ndio mwanzo wa kupoteana hadi leo sasa kwa jinsi wanavyoonekana kwenye kideo na boss wao diddy wanabang mtu wa kawaida unaweza kudhani anaweza kuwafanyia hivyo kweli [emoji3][emoji3][emoji3] kawachinjia baharini bila huruma mpaka kesho hajageuka nyuma
Umenikumbusha mbali sana hawa wamba onetwelve walijikuta hawajui wakajua maeeh didy mafia sana alikuwa anampiga big popaa[emoji3][emoji3]
 
Kuna mtu anaitwa p didy au puff daddy aliwapoteza lost boys wakalosti kweli kwa p funk utakuwa huna uelewa au unachuki zako binafsi na p funk wabongo tuache wivu wakishamba
 
Watu wanaingia kazini na kufanya kazi kienyeji mjanja akiona loophole akiitumia mtu anaanza kulalamika [emoji3][emoji3][emoji3]
Aisee majani mtoto wa kichotara yule hzo mbanga anazijua toka kiwanja kwake kuwatia Cha kike kina nature ilikuwa ishu ndgo ya mbele hawakuyajua lkni yeye alikuwa anajua Kila kitu na thamani ya kile anachokifanya kuwa kitakuja kumlipa vyombo vyake elimu yake kina Daz mia mbovu hawana akasajiri ili baadae aje ale kimvulini Leo wanamuona mnyonyajiz[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huyo Sallam SK hakwenda mbali na kuja na details za madai yake dhidi ya Majani tofauti na mwenzake kataja majina, mikataba na hadi kiasi cha pesa. Badala yake anawafanya Watanzania wajinga kwa kuingiza stories za Harmonize na wale makahaba Kajala na mwanae. Sallam SK alitakiwa awe specific and to the point siyo kutuletea taarab za Harmonize na Kajala.
 
Kuna mtu anakula hela ya eazy e na Tupac mpk ss kwa mambo hayo hayo. Unajua mpk Leo Dr. Dree hamiliki the cronic
Yah ndio maana yake hata pac watu walikuwa wanampiga ukifatilia history ya pac we acha album vzte alizofanya death row alifanya bure MALIPO yalikuwa mchongo wa kumtoa jela muda ambao anakufa ndio ilikuwa anaenda kuwa free kufanya album popote sugar akampeleka kaburini ni story ndefu sana Kuna umafia sana kwenye game huko
 
Umenikumbusha mbali sana hawa wamba onetwelve walijikuta hawajui wakajua maeeh didy mafia sana alikuwa anampiga big popaa[emoji3][emoji3]
Hatari jamaa kama kumbukumbu zangu ziko sawa waliambiwa kama ni kutoka bas jina la 112 hakuna kutumia 😀😀😀
Sasa dunia nzima zaidi ya miaka 10 wanajulikana kwa jina hilo wabadili wajiite nani na hawako tena kwenye peak wajiite 120 😁😁😁 mpaka watu waje kuelewa sio leo tena
 
Kiongozi I have very deep infos kuhusu hii game ya bongo music industry hii ni kwa dababu nimefanya kazi kwa karibu na hii industry for the good 2yrs. Kila wakati huwa natamani kuandika gazeti humu nielimishe watu huwa kila nikianza naishoa kati halafu naamua kufuta maana kinachofanyika kwenye industry ni UBAKAJI na kuviziana kwamba atakaemuwahi mwenzake basi ameshinda milele. Sometimes huwa naogopa maana taarifa nilizipata nikiwa nafanya kazi kwenye taasisi ya umma na kwa namna nilivyoji-expose humu ni rahisi sana kuwa traceable ila nitaleta gazeti juu ya game ya muziki na film inavyoendeshwa hapa mjini.
Kikubwa ni kuwa ELIMU ELIMU ELIMU na mbaya zaidi hawa wahusika wenyewe hawapo tayari kupata elimu hiyo na kibaya zaidi ni kuwa wenye hiyo elimu ni wachache maana hata wale wanaojinasibu sana kumbe hawafahamu sana kuhusu COPYRIGHT inavyofanya kazi yaani hadi baadhi ya mawakili.
Sasa kwa kuwa wengi (more than 90%) ya wasanii na managers wao hawana elimu ya kutosha juu ya haya mambo ndio mwisho wa siku wanaviziana na anaemuwahi mwenzie ndio anatoboa
Hiibya kuviziana imenichekesha Sana. Imenikumbusha mfano wa konokono wanaoviziana, atakayewahi kumpanda mwenzie ndio anayembebesha mimba aliyepandwa.
 
yaah sema ndo hivyo sijui nani ana mmenage maana bila hivyo atapotea bila kufaidi pesa zakee..sioni akipiga show akati ndo muda wenyewe..!! apate manager kichwa azungukee aisee kuzikusanyaaa amezubaa sanaa...
Bongo Hakuna shows. Labda uandae mwenyewe
 
Aisee majani mtoto wa kichotara yule hzo mbanga anazijua toka kiwanja kwake kuwatia Cha kike kina nature ilikuwa ishu ndgo ya mbele hawakuyajua lkni yeye alikuwa anajua Kila kitu na thamani ya kile anachokifanya kuwa kitakuja kumlipa vyombo vyake elimu yake kina Daz mia mbovu hawana akasajiri ili baadae aje ale kimvulini Leo wanamuona mnyonyajiz[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Alikua mbele ya muda
Watoto wa temeke walikuwa wanafurahia tu kwenda masaki 😆😆😆
 
Bizman na wengine waliokuwa wanasaidia Majani kwenye production, lini uliwahi wasikia wakilalamika!? Je, wakati kazi zinasajiliwa kwenye mamlaka husika hao waliorodheshwa katika production? Ila usisahau hizo ni kazi za Bongo Records. Kama Kuna makubaliano baina ya P Funk na Producers washiriki hayo yanakuwa ni makubaliano yao binafsi.
Majani hawezi kupiga chombo chochote cha mziki sio kinanda,sio gitaa hata alipiga gitaa kwenye track ya umbo namba 8 sio yeye nimeajiwa kwa sababu ya mziki nilikuwa napiga kwenye live band pfunk namfahamu vizuri ukitengeneza beat au ukiingiza melody ya chombo chochote unalipwa posho kidogo na habari yako inaishia hapo tena anamadharau ya kufa mtu mwamba amini
 
Link ipo chini, katazame huko youtube, like na u subscribe asante sana.

Filamu Pictures, wanawaletea kazi ya filamu ya kitanzania iitwayo PETE

Kutana na Bwana Lidawi, mvuvi mwenye hali ngumu na mke mgonjwa na jinsi anavyoingia matatizoni kutokana na pete ya maajabu iliyofika katika ulimwengu wa wanadamu kwa ajili ya kazi maalum

Kutana na Bwana Songolo mtu tajiri, mkorofi na mkali sana, ambaye nae anajikuta yuko katikati ya mikasa hiyo ipatayo bwana Lidawi

Karibuni
 
Majani hawezi kupiga chombo chochote cha mziki sio kinanda,sio gitaa hata alipiga gitaa kwenye track ya umbo namba 8 sio yeye nimeajiwa kwa sababu ya mziki nilikuwa napiga kwenye live band pfunk namfahamu vizuri ukitengeneza beat au ukiingiza melody ya chombo chochote unalipwa posho kidogo na habari yako inaishia hapo tena anamadharau ya kufa mtu mwamba amini
So yeye anaweza kukusanya watu wakufanya Production tu??? Kama Dj khaled anawaita mnatia verse mnakula mpunga wimbo wakee...
 
Back
Top Bottom