Ukweli usiopingika: Katika marais waliotumikia taifa letu ni hayati JPM pekee aliyefanya makubwa kwa muda mfupi kuliko marais wote waliotutawala

Ni kweli kabisa, amempoteza ben saanane, amempiga risasi tundu lissu, ameiba uchaguzi, aliliweka bunge na mahakama mfukoni, alikuwa anajua kila kitu. nk
Haya Katika kuinyoosha Nchi iliyojaa majizi ni lazima yatokee.
Mara nyingine majizi yanatengeneza matukio ya kutisha Ili kudhoofisha juhudi za Kiongozi za kupambana na ufisadi.


Kule Zanzibar Mwinyi analeta Maendeleo chanya Lakini kitakachofuata ni matukio ya Ugaidi kutengenezwa Ili kudhoofisha juhudi za kupeza Maendeleo.
 
Wewe Ni kabila gani nimependa mawazo yako ila Happ kwenye wasukuma mh sijakuelewa na sio haki kuhubiri ukabila katika Karne hii
 
Mfuate huko jehanam usitujazie server bure hapa
 
Tatizo la kuishi nchi za kimaskini na zisizo na demokrasi, mkuu wa nchi sio mungu na kumkosoa au kumtukana sio kosa, acha watu waongee sio kuwaua kwa sababu hupendezwi na walichosema
Mkuu hapa kuna watu hawana uelewa wa msingi kabisa wa elimu ya uraia na demokrasia.

Licha ya hilo, hawana hata utu wa kawaida tu, wanafikiri kama wanyama, wanakwenda kwa basic instincts na reflex action kama guluguja.

Ndiyo maana wanafagilia Magufuli kupiga risasi wapinzani.
 
Hivi bora kipi kujenga miundobinu kwenye vichwa vya watanzania au kujenga Barabara na madaraja zenye upigaji? Mwalimu alilinda raslimali zetu hadi watanzania watakapota maarifa.Mwalimu alijenga heshima na kuondoa migawanyiko baina ya watanzania.Anaweza kuwa na makosa kama bindamu lakini ni dhambi kumlinganisha Mwalimu na marais waliomfuata hata wao wanajua wengine walijiita vichuguu wakilinganishwa na Mwl
 

Kila Rais alifanya ya kwake ambayo yamejenga msingi wa Magufuli kufanya aliyoyafanya tuwe na heshima.
 
Hayo mazuri huyaoni kuwa yanamtetea?

Umekosea Sana kumlinganisha Nyerere na Magufuli. 1961 Unalinganisha na 2015. Tatizo watoto wa Leo wamezaliwa wamekuta maendeleo ya Tehama wanadhani hata 1961 mambo yalikuwa hivyo. Pia umekosea kumlinganisha na Mkapa kwa kusema Mkapa hakufanya lolote , tafadhali punguza ujuaji. Kila Rais alikuwa na mchango wake.
 
Kwa hivyo alikuwa Rais wa kuvunja upinzani?. Na mwisho akavunjiia yeye. Kiburi ni kitu kibaya Sana. Alikufa na kiburi chake na masifa.
 
mimi sio msukuma ila jamaa ksongea ukweli

Ukweli gani?. Unamlinganisha Rais wa Mwaka 1961 na Rais wa Mwaka 2015. Yani Magufuli kakuta watangulizi wamejengea msingi yeye kapita tu humo.
 
Ni kweli kabisa, amempoteza ben saanane, amempiga risasi tundu lissu, ameiba uchaguzi, aliliweka bunge na mahakama mfukoni, alikuwa anajua kila kitu. nk
Muulizeni Mwenyekiti wenu vizuri anajua alikompeleka. Muulizeni taratibu ama kwa kumbinya atawaelekeza alipo bwatcheight

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 

Kwa hivyo Lissu na Been Sanaane walikuwa majizi wakapigwa risasi na mwingine kupotezwa?. Magufuli aliangushwa na kiburi na ukatili kwa binadamu.
 
Ni kweli alifanya mengi lakini sifa zilimjaa akajisahau akachukua mpaka utukufu wa Mungu! Ukitaka kuamini mpaka leo kuna wapumbavu wanamwabudu! Mungu akaona isiwe tabu akamfyekelea mbali! Magu hakuuwawa magu alikufa kwa maradhi!
 
Ni kweli alifanya mengi lakini sifa zilimjaa akajisahau akachukua mpaka utukufu wa Mungu! Ukitaka kuamini mpaka leo kuna wapumbavu wanamwabudu! Mungu akaona isiwe tabu akamfyekelea mbali! Magu hakuuwawa magu alikufa kwa maradhi!
Alipigwa pigo kama la Farao wa Misri.Pamoja na Farao kutuachia majengo makubwa mazuri jumlisha na mapiramidi(maendeleo)lakini kutaka kujilinganisha na Mungu kulimgharimu.Kwa nini watu kabla na baada ya kupata madaraka hawajifunzi uchaji kwa Mungu?
 

So what? Badala ya kuangalia mbele ni kulalama kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…