Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Mi nashangaa sana hawa weusi wanaoshobokea majina ya kizungu. Ilihali hata kwenye bibble hiyo lugha yao Mungu aliita ya ajabu/isiyoeleweka pale alipowaambia waisrael(weusi) kuwa watakuja maadui zako kutoka mbali wasio na huruma na mkubwa wala mtoto watakuuza utumwani utabebwa na meli kuuzwa mbali na hawa watu makatili ...( sasa unashobokeaje majina ya watu makatili)
 
Ndugu rudi nyumbani kumenoga, Asili yako itabaki yako tu na usijidanganye. Afrika sio rangi nyeusi tu Elewa.
 
Kuna kitabu wajameni mukitafute cha Mch. KAMARA KUSUPA kinaitwa "Kumrudisha Mwafrika kwenye Asili Yake - Mradi Mgumu Kuliko Yote"
kama kuna soft copy basi tupate, na itafaa kama utashea idea yake. Ila mm naijivunia kuwa mwafrika
 
Hizi habari za muafrika kuacha asili yake unaweza kufikiri muafrika kabadilika kawa kama mzungu au muarabu,.
Hali ya sasa Afrika ni kama uarabuni au uingereza, amerika etc. Afrika inapotea katika ramani ya Dunia.
 
Mkuu, nakupongeza kwa hoja zako zilizokuwa factual, consistent and thorough!" Inaonekana wewe kama mimi ni mpenda ukweli, ila huyu jamaa hana aibu, anazungusha ukweli (twisting facts) mradi apate kitu ya kusema!!!
Tamaduni gani ambayo hadi mda huu ww unaikubali ya Afrika? Ukiona hauipati basi jua tayari akili yako imebadilishwa na kuwa na mtazamo mbaya kuhusu Afrika ila kwa sasa haujui tu. Utaanza kuchukia vitu vya asili vya Afrka na baadae utaanza chukia rangi nyeusi kama wadada zetu na baadhi ya watu. Kuna watu waafrika wanachukia rangi nyeusi na kuona ni uchafu. Mambo haya yana side effects nyingi sana kwa kizazi kijacho.
 
Jamaa inahitaji moyo kweli kujadiliana naye maana anajitoa fahamu kabisa.
Watu wameharibiwa vibaya sana hivyo aelimishwe tu kidogo kidogo. Hii ndio hali halisi ya mwafrika na Afrika yake/yetu. Africa will rise up, stand up and glow up like the moon at night.
 
Watu wanajidanganya sana ndg, hawa watu bara letu na Mungu hawataacha salama. Haiwezikani Afrika inakufa kienyejienyeji.
 
Hawa wenzetu Viongozi wao walikuwa wanajitambua kuwa ufake haufai, na unasababisha manyanyaso, utengano na ubaguzi baina ya wao kwa wao. Ss historia inatutambua vizuri ila tunajifanya hatuitambui kwa kufuata zaidi iman, mila na tamaduni za nje. Ila ninaimani kubwa siku moja Afrika Itasimama tena imara.
 
Rais moja Mzungu wa Afrika Kusini aliwahi kufanya utafiti juu uwezo wa Mwafrika Mweusi katika kufikiri, kutenda na kuongoza wengine .

Utafiti huu ulimwezesha kupata PHD.
Katika utafiti wake alihitimisha kwa kusema kuwa , " Mwafrika Mweusi mwenye Akili kuliko wote hawezi kufikiri zaidi ya mwaka moja. (The most Intelligent black African can not think beyond one year). Hata hivyo hii sio asilimia mia moja kwa sababu bado wazungu walikiri kuwa Viongozi kama Hayati Mwalimu J.K.Nyerere walikuwa tofauti sana na dhana hii ya utafiti wa Mzungu huyu.

Mwafrika akikukuta unakula usipomkaripisha atakuita mlafi. Mwafrika akikukuta unafanya kazi akikusaidia atadai pesa. Mzungu akikukuta unakula hata ukimkaribisha hatokula kama ulikuwa hujamwalika. Mzungu akikukuta unafanya kazi atakusaidia na hatakudai pesa.
Kuna kabila moja siwezi kulitaja jina, Vijana wao wakiwa sita wakienda kuiba ng'ombe, wataiba ng'ombe na watamuua mwenye Ng'ombe.

Baadaye wakiwa safarini kurudi kwao watatu watafanya hila na kuwaua wenzao watu.
Watatu wakifika salama na ng'ombe wa wizi mgawo unakuwa mzuri na hutoa taaifa kuwa wenzao wameuwawa wakati wanaiba ng'ombe.

Nataka niseme tu kuwa nasononeka sana na hulka ya Mtu mweusi kuhusu uchoyo, fitina, wivu, ulafi, majivuno, ukatili, uonevu na mengine mengi. Udhaifu huu ndiyo unatufanya tusiendee pamoja na kuwa na raslimali nyingi.
 
Ndugu rudi nyumbani kumenoga, Asili yako itabaki yako tu na usijidanganye. Afrika sio rangi nyeusi tu Elewa.
Waarabu walikuwa wanaabudu masanamu ila ukaja uislamu ukaenea na leo waarabu uislamu imekuwa ndio asili yao na husikii wakizungumzia habari za asili ya wazee wao waliyokuwa wakiabudu masanamu.
 
Hali ya sasa Afrika ni kama uarabuni au uingereza, amerika etc. Afrika inapotea katika ramani ya Dunia.
Unataka kuniambia muarabu au mzungu akija afrika haoni tofauti anajihisi kama yupo nyumbani?

Waafrika watabaki kuwa waafrika tu kama ilivyo muhindi kubaki kuwa muhindi bila kujari anafuata hinduism ukristo au uislamu.
 
utofauti upo kwenye muonekano tu ila content zinaendana kwa maana Waafrika tunafanya yale ya kigeni. Mwarabu akiingia msikitini anajua kiarabu na quran kuliko waliojenga msikiti na anaeswalisha.

Hivyo hivyo kanisani ni mfumo wa nje unaoratibiwa tu na waafrika.
 
Waarabu walikuwa wanaabudu masanamu ila ukaja uislamu ukaenea na leo waarabu uislamu imekuwa ndio asili yao na husikii wakizungumzia habari za asili ya wazee wao waliyokuwa wakiabudu masanamu.
Walikuwa wanaabudu mbele ya Kitu fulani neno sanamu ni msamiati tu wa kukuzubaisha. Mbele ya mti mkubwa au jiwe ila ndani ya nafsi yao ilikuwa kwa mungu wao yuleyule. Changes na fictious story nyingi wameingiza kwenye maandiko ili tu wakupumbaze.
 
Huo ni mfano wa kabila moja kati ya maelfu. Ila bado Afrika ni imara na inatamaduni nzuri kuliko nje. Watu wanachanganya kati ya tech na tamaduni za wazungu. Kuna maendeleo ya kiuchumi(watu) na maendeleo ya kiroho(dini) .
 
Ukizungumzia habari za msikitini au kanisani huko kinachowaunganisha ni imani zao na si utaifa wa mtu wala jamii ya mtu,ila mzungu akienda china au korea atajiona kama yupo nyumbani hakuna tofauti sana. Hao wahindi mnaowasifia siku hizi movie zao ni mambo ya kizungu tu kwenda mbele.
 
Walikuwa wanaabudu mbele ya Kitu fulani neno sanamu ni msamiati tu wa kukuzubaisha. Mbele ya mti mkubwa au jiwe ila ndani ya nafsi yao ilikuwa kwa mungu wao yuleyule. Changes na fictious story nyingi wameingiza kwenye maandiko ili tu wakupumbaze.
Mungu wao yuleyule yupi? maana huwezi kubadili utaratibu wote wa ibada na bado ukasema unamuabudu Mungu yule yule,basi hata sie waafrika tunaabudu Mungu yuleyule.
 
Mungu wao yuleyule yupi? maana huwezi kubadili utaratibu wote wa ibada na bado ukasema unamuabudu Mungu yule yule,basi hata sie waafrika tunaabudu Mungu yuleyule.
Kwani tangu zamani wazee wetu walikuwa wanaabudu mungu yupi? Ss tulikuwa tunamuomba muumba wetu.
 
Ndugu umesema yote lakini pia umeishia kwa kunena lugha yao ni jinsi gani hata wewe upo na mambo yao ayo unayoyapinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…