Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

hapo kwenye swala la majina nimegombana sana na huyu mwanamke. nilivyomwambia mtoto wetu atakua na jina la kiafrika alivimba vibaya mno na aliniona kama m'babu, mshamba, wa kuja. niliskitika sana kwasababu sio kosa lake, amekua programmed tangu utotoni kuona cha mzungu ni cha maana kuliko cha muafrika.. tangu utotoni anaambiwa binadamu kutoka israeli ndio Mungu wake, unatarajia nini?
mabadiliko ya hili swala inabidi yaanzie ngazi ya kitaifa halafu yatufikie sisi, bila ya hivyo hamna kitu hapa kitabadilika. lazma serikali itie mkono wake.
Mi nashangaa sana hawa weusi wanaoshobokea majina ya kizungu. Ilihali hata kwenye bibble hiyo lugha yao Mungu aliita ya ajabu/isiyoeleweka pale alipowaambia waisrael(weusi) kuwa watakuja maadui zako kutoka mbali wasio na huruma na mkubwa wala mtoto watakuuza utumwani utabebwa na meli kuuzwa mbali na hawa watu makatili ...( sasa unashobokeaje majina ya watu makatili)
 
Unazungumzia kuanzishwa kwa ukristo au madhehebu na vitabu vyao? maana hata afrika kila kabila lina mila zake ila kwa pamoja mnaita imani au dini za kiafrika.
Na kwanini nifuate walichokiamini watu kabla yetu kisa tu walikuwa mababu zetu wakati wao walifuata hizo imani kwa uamuzi wao kwa manufaa yao kipindi chao,sasa hiki ni kizazi chengine hivyo tunafuata tuamuacho sie kwa kipindi chetu na tunaofaidika ama kutokufaidika ni sisi na pia hata sisi tutakuja kuitwa mababu pia kwa vizazi vijavyo kama mababu ni ishu sana.
Ndugu rudi nyumbani kumenoga, Asili yako itabaki yako tu na usijidanganye. Afrika sio rangi nyeusi tu Elewa.
 
Kuna kitabu wajameni mukitafute cha Mch. KAMARA KUSUPA kinaitwa "Kumrudisha Mwafrika kwenye Asili Yake - Mradi Mgumu Kuliko Yote"
kama kuna soft copy basi tupate, na itafaa kama utashea idea yake. Ila mm naijivunia kuwa mwafrika
 
Hizi habari za muafrika kuacha asili yake unaweza kufikiri muafrika kabadilika kawa kama mzungu au muarabu,.
Hali ya sasa Afrika ni kama uarabuni au uingereza, amerika etc. Afrika inapotea katika ramani ya Dunia.
 
Mkuu, nakupongeza kwa hoja zako zilizokuwa factual, consistent and thorough!" Inaonekana wewe kama mimi ni mpenda ukweli, ila huyu jamaa hana aibu, anazungusha ukweli (twisting facts) mradi apate kitu ya kusema!!!
Tamaduni gani ambayo hadi mda huu ww unaikubali ya Afrika? Ukiona hauipati basi jua tayari akili yako imebadilishwa na kuwa na mtazamo mbaya kuhusu Afrika ila kwa sasa haujui tu. Utaanza kuchukia vitu vya asili vya Afrka na baadae utaanza chukia rangi nyeusi kama wadada zetu na baadhi ya watu. Kuna watu waafrika wanachukia rangi nyeusi na kuona ni uchafu. Mambo haya yana side effects nyingi sana kwa kizazi kijacho.
 
Jamaa inahitaji moyo kweli kujadiliana naye maana anajitoa fahamu kabisa.
Watu wameharibiwa vibaya sana hivyo aelimishwe tu kidogo kidogo. Hii ndio hali halisi ya mwafrika na Afrika yake/yetu. Africa will rise up, stand up and glow up like the moon at night.
 
Mi nashangaa sana hawa weusi wanaoshobokea majina ya kizungu. Ilihali hata kwenye bibble hiyo lugha yao Mungu aliita ya ajabu/isiyoeleweka pale alipowaambia waisrael(weusi) kuwa watakuja maadui zako kutoka mbali wasio na huruma na mkubwa wala mtoto watakuuza utumwani utabebwa na meli kuuzwa mbali na hawa watu makatili ...( sasa unashobokeaje majina ya watu makatili)
Watu wanajidanganya sana ndg, hawa watu bara letu na Mungu hawataacha salama. Haiwezikani Afrika inakufa kienyejienyeji.
 
1. Sonia Gandi akukataa kwa hiari yake mazingira yalimlazimisha kwanza nikuweke sawa hapa , baada ya Indian National Congress kupata kura nyingi watu walitegemea PM atakuwa Sonia lakini BJP walikataa kwa hoja kuwa huyu sio mzaliwa wa INDIA(foreign born) , tabia zake na tamaduni zake aziko kwenye miiko ya KIINDI( jamii aina cha kujifunza apa ) , ndio maana watu kama Mrs Sushma Swaraj na Sadhri Uma Bharti walitishia kujitoa UHAIA wao kwa kuaribu vichwa vyao iwapo tu SONIA ataapa kuwa PM , haya mambo ndio yalisababisha SONIA kukaa pembeni ata kama katiba inamruhusu lakini watu wamekukataa, angechafua nchi huyu , ndio maana akakaa pembeni , kupisha wenye sifa stahiki kushika usukani
2. Huo ni uongo Gandi alikuwa ni kiongozi wa kiroho wa Wahindu hakuwa na uwezo wa kumfanya Jinnah awe PM kwa namna yeyote ile , Wahindu katu wasingekubali asilani, kuhusu ugomvi wa WASIKH na WAHINDU inaeleweka sababu ni wale walinzi wa kisikh waliomuua Gandi , ndio ugomvi ulipoanza , wala hakuna uhusiano na yale ya kutengana kwa INDIA na Pakistan
3. Leta jina la Muislamu mmoja aliekuwa PM wa INDIA , nafasi nyingine inawezekana kwani ata Kashmir kuna waislamu ambao ni sehemu ya INDIA , sasa unategemea atawaongoza nani , lazima wajiongoze wenyewe kwa kuwa na wawakilishi wao , ambao wanakuwa sehemu ya serikali ya INDIA
Hawa wenzetu Viongozi wao walikuwa wanajitambua kuwa ufake haufai, na unasababisha manyanyaso, utengano na ubaguzi baina ya wao kwa wao. Ss historia inatutambua vizuri ila tunajifanya hatuitambui kwa kufuata zaidi iman, mila na tamaduni za nje. Ila ninaimani kubwa siku moja Afrika Itasimama tena imara.
 
Rais moja Mzungu wa Afrika Kusini aliwahi kufanya utafiti juu uwezo wa Mwafrika Mweusi katika kufikiri, kutenda na kuongoza wengine .

Utafiti huu ulimwezesha kupata PHD.
Katika utafiti wake alihitimisha kwa kusema kuwa , " Mwafrika Mweusi mwenye Akili kuliko wote hawezi kufikiri zaidi ya mwaka moja. (The most Intelligent black African can not think beyond one year). Hata hivyo hii sio asilimia mia moja kwa sababu bado wazungu walikiri kuwa Viongozi kama Hayati Mwalimu J.K.Nyerere walikuwa tofauti sana na dhana hii ya utafiti wa Mzungu huyu.

Mwafrika akikukuta unakula usipomkaripisha atakuita mlafi. Mwafrika akikukuta unafanya kazi akikusaidia atadai pesa. Mzungu akikukuta unakula hata ukimkaribisha hatokula kama ulikuwa hujamwalika. Mzungu akikukuta unafanya kazi atakusaidia na hatakudai pesa.
Kuna kabila moja siwezi kulitaja jina, Vijana wao wakiwa sita wakienda kuiba ng'ombe, wataiba ng'ombe na watamuua mwenye Ng'ombe.

Baadaye wakiwa safarini kurudi kwao watatu watafanya hila na kuwaua wenzao watu.
Watatu wakifika salama na ng'ombe wa wizi mgawo unakuwa mzuri na hutoa taaifa kuwa wenzao wameuwawa wakati wanaiba ng'ombe.

Nataka niseme tu kuwa nasononeka sana na hulka ya Mtu mweusi kuhusu uchoyo, fitina, wivu, ulafi, majivuno, ukatili, uonevu na mengine mengi. Udhaifu huu ndiyo unatufanya tusiendee pamoja na kuwa na raslimali nyingi.
 
Ndugu rudi nyumbani kumenoga, Asili yako itabaki yako tu na usijidanganye. Afrika sio rangi nyeusi tu Elewa.
Waarabu walikuwa wanaabudu masanamu ila ukaja uislamu ukaenea na leo waarabu uislamu imekuwa ndio asili yao na husikii wakizungumzia habari za asili ya wazee wao waliyokuwa wakiabudu masanamu.
 
Hali ya sasa Afrika ni kama uarabuni au uingereza, amerika etc. Afrika inapotea katika ramani ya Dunia.
Unataka kuniambia muarabu au mzungu akija afrika haoni tofauti anajihisi kama yupo nyumbani?

Waafrika watabaki kuwa waafrika tu kama ilivyo muhindi kubaki kuwa muhindi bila kujari anafuata hinduism ukristo au uislamu.
 
Unataka kuniambia muarabu au mzungu akija afrika haoni tofauti anajihisi kama yupo nyumbani?
Waafrika watabaki kuwa waafrika tu kama ilivyo muhindi kubaki kuwa muhindi bila kujari anafuata hinduism ukristo au uislamu.
utofauti upo kwenye muonekano tu ila content zinaendana kwa maana Waafrika tunafanya yale ya kigeni. Mwarabu akiingia msikitini anajua kiarabu na quran kuliko waliojenga msikiti na anaeswalisha.

Hivyo hivyo kanisani ni mfumo wa nje unaoratibiwa tu na waafrika.
 
Waarabu walikuwa wanaabudu masanamu ila ukaja uislamu ukaenea na leo waarabu uislamu imekuwa ndio asili yao na husikii wakizungumzia habari za asili ya wazee wao waliyokuwa wakiabudu masanamu.
Walikuwa wanaabudu mbele ya Kitu fulani neno sanamu ni msamiati tu wa kukuzubaisha. Mbele ya mti mkubwa au jiwe ila ndani ya nafsi yao ilikuwa kwa mungu wao yuleyule. Changes na fictious story nyingi wameingiza kwenye maandiko ili tu wakupumbaze.
 
Rais moja Mzungu wa Afrika Kusini aliwahi kufanya utafiti juu uwezo wa Mwafrika Mweusi katika kufikiri, kutenda na kuongoza wengine .
Utafiti huu ulimwezesha kupata PHD.
Katika utafiti wake alihitimisha kwa kusema kuwa , " Mwafrika Mweusi mwenye Akili kuliko wote hawezi kufikiri zaidi ya mwaka moja. (The most Intelligent black African can not think beyond one year).
Hata hivyo hii sio asilimia mia moja kwa sababu bado wazungu walikiri kuwa Viongozi kama Hayati Mwalimu J.K.Nyerere walikuwa tofauti sana na dhana hii ya utafiti wa Mzungu huyu.
Mwafrika akikukuta unakula usipomkaripisha atakuita mlafi. Mwafrika akikukuta unafanya kazi akikusaidia atadai pesa.
Mzungu akikukuta unakula hata ukimkaribisha hatokula kama ulikuwa hujamwalika. Mzungu akikukuta unafanya kazi atakusaidia na hatakudai pesa.
Kuna kabila moja siwezi kulitaja jina, Vijana wao wakiwa sita wakienda kuiba ng'ombe, wataiba ng'ombe na watamuua mwenye Ng'ombe.
Baadaye wakiwa safarini kurudi kwao watatu watafanya hila na kuwaua wenzao watu.
Watatu wakifika salama na ng'ombe wa wizi mgawo unakuwa mzuri na hutoa taaifa kuwa wenzao wameuwawa wakati wanaiba ng'ombe.
Nataka niseme tu kuwa nasononeka sana na hulka ya Mtu mweusi kuhusu uchoyo, fitina, wivu, ulafi, majivuno, ukatili, uonevu na mengine mengi.
Udhaifu huu ndiyo unatufanya tusiendee pamoja na kuwa na raslimali nyingi.
Huo ni mfano wa kabila moja kati ya maelfu. Ila bado Afrika ni imara na inatamaduni nzuri kuliko nje. Watu wanachanganya kati ya tech na tamaduni za wazungu. Kuna maendeleo ya kiuchumi(watu) na maendeleo ya kiroho(dini) .
 
utofauti upo kwenye muonekano tu ila content zinaendana kwa maana Waafrika tunafanya yale ya kigeni. Mwarabu akiingia msikitini anajua kiarabu na quran kuliko waliojenga msikiti na anaeswalisha. Hivyo hivyo kanisani ni mfumo wa nje unaoratibiwa tu na waafrika.
Ukizungumzia habari za msikitini au kanisani huko kinachowaunganisha ni imani zao na si utaifa wa mtu wala jamii ya mtu,ila mzungu akienda china au korea atajiona kama yupo nyumbani hakuna tofauti sana. Hao wahindi mnaowasifia siku hizi movie zao ni mambo ya kizungu tu kwenda mbele.
 
Walikuwa wanaabudu mbele ya Kitu fulani neno sanamu ni msamiati tu wa kukuzubaisha. Mbele ya mti mkubwa au jiwe ila ndani ya nafsi yao ilikuwa kwa mungu wao yuleyule. Changes na fictious story nyingi wameingiza kwenye maandiko ili tu wakupumbaze.
Mungu wao yuleyule yupi? maana huwezi kubadili utaratibu wote wa ibada na bado ukasema unamuabudu Mungu yule yule,basi hata sie waafrika tunaabudu Mungu yuleyule.
 
Mungu wao yuleyule yupi? maana huwezi kubadili utaratibu wote wa ibada na bado ukasema unamuabudu Mungu yule yule,basi hata sie waafrika tunaabudu Mungu yuleyule.
Kwani tangu zamani wazee wetu walikuwa wanaabudu mungu yupi? Ss tulikuwa tunamuomba muumba wetu.
 
Afrika ina dini ambazo ni nyingi sana kuliko bara lolote lile Duniani. Dini hizi nyingi zimepigwa ban na watu wa nje(whites) kwa sababu tu ya inferior ya mtu mweusi wa zamani. Kuishi kwa kumtegemea mzungu kwa kila kitu hadi ikapelekea hadi sasa watu wanategemea pia dini za kizungu.

Hakuna kabila hata moja Afrika ambalo limepoteza imani ya dini yao, ndio maana hata waendao makanisani hutembelea kwa mababu zao kupata kinga. Dini zote Afrika zilikuwa hazihusiani na uchawi ila mtu mweupe ndiye aliempa mtu mweusi uchawi kwa mafunzo maalumu akimdanganya ya kiimani.

Uchawi Afrika uliletwa na mzungu na ukweli huu haupingiki. ukiachana na hayo lakini pia upande wa maadili hapa nianze kwa salamu


U hai? ndugu hata kama haupo hai ila ukweli ukifikie huko huko ulipo. Nani aliyekuambia kuwa Afrika watu walikuwa wanavaa nguo full mwili mzima? Angalia wamasai japo na hao pia wamejaribu kubadilika. Ila hali ilikuwa mbaya sana zamani.

Watu walikuwa wanazuii tupu tu, Vikande vyote vya nyuma vilikuwa wazi na hakukuwa wa kushangaa katika hili kwa sababu ndiko tulikotoka. Ujio wa white man ukatibua hali ya hewa wakabadili,mtindo wa mavazi,dini, elimu, lugha, biashara na kila kitu.

Sasa katika mambo waliobadili pamoja na nidhamu na kusema nchi za Afrika hawajastarabika kwa sababu wanatembea uchi, wanaabudu madudu, wanaongea lugha chafu n.k. Watu wa Afrika walilazimishwa kukopi mila na mitindo yote ya Kizungu.

Unaposema vijana wetu hawana maadili ni kutukana wazee wetu wa zamani ambao walikuwa wanawinda,na kupiga ngoma uchi.

Hawa wapuuzi wa kizungu ndio walioita matabibu wetu kwa jina baya eti Matabibu wa kichawi(witch doctor) na wao kujiita Doctors, physician mara sijui wakemia n.k. Wakasema kupiga ngoma ni ushamba ila tupige miziki ya kisasa n.k.

Sioni jema la wazungu katika imani, wala tamaduni na wala technology kwa sababu naamini tungepigana na hali zetu. Wale wanaoenzi mababu zetu siku hizi wanajiita TIBA MBADALA sijui ndio nini. Wajiite wauguzi na wataalamu wa tiba na magonjwa mbalimbali.

Afrika without White's countries is possible, hatujachelewa sana tuanze ku uphold vya kwetu ili vitusaidie na sisi kwa masilai yetu. Hivi vya kuletewa havitufai kwani "NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI MA**KO" na ndio mana mambo hayaendi kama ilivyotakiwa.

Nawachukia wa Asia na dini zao i.e Christian and Muslims. Ww ndugu yangu mtoto na mjuu wa Likangamai hayo mambo utayaweza? Ndio maana kulikuwa na mabala na aina ya watu na mila tofautitofauti, sasa ya nje ya nn na kuona kama vile ulichelewa kuvipata?

Kwani wao walikuwa hawajui kama Afrika kuna watu? mbona wamefika baada ya manyanyaso mauaji na dhulma kwa ndg zetu? Nini za Asia ni dini za ukweli kwa Asia na dini za Afrika ni za kweli kwa Afrika tu?

Jambo gani jema limewahi semwa na hao watu juu ya mababu zetu? wamewatukana sana kupitia imani zao na leo wamefanikisha kutufanya ndg,jamani tunaenda wapi na ilihali tunakotoka tunakudharau?

NAIPENDA AFRIKA SANA NA HATA NIKIWA JIRANI NA MZUNGU WOTE WE FEEL DIFFERENCES ON EACH AND EVERYTHING.RELIGION, LANGUAGE, STYLES,CUSTOMS, COLOUR, AWARENESS, ASSERTIVENESS STATUS, RECOGNITION e.t.c.

Ukweli haupingiki hata mniue hadi nife
Ndugu umesema yote lakini pia umeishia kwa kunena lugha yao ni jinsi gani hata wewe upo na mambo yao ayo unayoyapinga
 
Back
Top Bottom