Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Hakutakuwa na maana ya maisha bila ya upendo na amani
 
Sawa ila kusudio la Mungu kutuumba umejuaje kuwa ni hilo?
Tuliumbwa ili tuishi na thamani ya maisha ni upendo,furaha na amani. Vyote tunavyovifanya duniani ni kwa sababu ya upendo,furaha na amani
 
Tuliumbwa ili tuishi na thamani ya maisha ni upendo,furaha na amani. Vyote tunavyovifanya duniani ni kwa sababu ya upendo,furaha na amani
Mkuu unanilisha mawazo yako wakati unajua kila mtu anaweza kuwaza kivyake na ndiyo maana nimeeleza hapo watu wengine husema kuwa hajaweka wazi kusudio la kutuumba na wala hajishughulishi na jinsi tuishivyo.
 
Hicho kitabu unataka aandike nani ili kiwe reference kwako? Nambie ntampa material ili ukiona handwriting yake uamini.
Sasa mzee si ndio yaleyale uliyokuwa unasema kuwa mwafrika hataamini hadi reference itoke kwenye kitabu cha mzungu. Kwani andiko lako haliwezi kuwa reference kwa wengine siku za usoni?
 
Mimi naona hakuna jambo baya waafrika kuacha mila zetu kwa sababu siku zote inabid kufwata vitu vya mtu aliyekuzidi.

Tunafwata vya wazungu kwa sababu wametuzidi na kuwafwata na sisi twaweza barikiwa kama wao. Endapo tungewatawala basi wao ndo wangefwata mila zeti na tamaduni
 
Wahindi, Wachina hawawafuata wao. Vipi una maoni gani juu ya hilo?
 
Dini za Waafrika ni vigumu sana kuzitenganisha na Mila na Desturi zao, hivyo mimi naona dini za kiafrika na Mila na desturi zao ni kitu kimoja kilekile. Waafrika tuna mila na desturi nyingi toifauti tofauti sana ambazo ni vigumu kuiita dini moja kama ilivyo kwa dini nyingine kubwa mbalimbalui duniani. Na katika mchanganyiko wa mila na desturi hizo mbalimbali zipo baadhi ni nzuri lakini pia ni lazima tukubali ukweli kwamba kuna nyingi mbaya zisizostahili kabisa kuwepo. Nitatoa baadhi ya mifano ya mila hizo mbaya na nzuri,

Mfano wa mila nzuri ni kama vile, kutahiri wanaume, kufanya matambiko ya kuchinja wanyama kama wafanyavyo makabila mengi mfano wachagga huomba miungu yao kwa kuchinja mbuzi, kondoo au ngombe sambamba na kuandaa pombe ya kienyeji(Mbege), mimi sioni mila kama hii ni mbaya hata kidogo kwani haimdhuru mtu yeyote na tena ilileta nidhamu kwa watu kuamini Ipo Nguvu juu yenye uwezo wa kuwaadhibu watendapo mabaya.

Kwa upande mwingine wa shilingi Waafrika tulikuwa na mila nyingine kwa kweli hata Wazungu kuita zilikuwa ni za kishenzi mimi sioni kama walituonea, kuna mila nyingine kwa akili ya kawaida kabisa huwezi ukazikubali, mila mfano ya kutahiri wanawake, kuzika machifu waliokufa wakiwa na watu waliokuwa hai, hebu imagine ni wewe unaambiwa eti uzikwe na maiti ya chifu ungali hai unapumua tena la kushangaza zaidi unaambiwa baadhi ya waliotakiwa kuzikwa na machifu, wenyewe walifurahia kitendo hicho! Kuna mila kama za kuua maalbino pindi tu walipokuwa wakizaliwa hivi, au kuwatupa misituni nk. Tukienda mbali zaidi kuna imani ambazo hata leo hii bado watu wanazo, imani za kishirikina hamna asiyetambua madhara yake katika jamii. Sasa utasemaje kuwa dini hizi zilikuwa zinatufaa?

Dini au mila za Waafrika hazina Mungu mmoja, kuna Miungu mingi kitu kinachosababisha mtu kushindwa kuziweka katika kundi moja, Tunachoweza kufanya Waafrika ni kuendeleza zile mila na tamaduni nzuri tu ambazo hazina madhara kwa binadamu. Kwa mfano mambo ya uganga na uchawi hayaeleweki, ni vitu vinavyofanyika kwa sirisiri, na ndio uliokuwa msingi wa dini zetu Waafrika. Sasa mambo kama hayo ya kifichoficho unawezaje kuyaita ni dini inayoweza kumsaidia mwanadamu? Huwezi kumtofautisha mganga na mchawi ni yupi kwani wote wanawadhuru binadamu. Wakati wachawi wakidaiwa kuwaloga watu lakini waganga nao wanalaumiwa sana kwa kusababisha uchonganishi, mauaji na machungu mengine mengi kwa kisingizio cha kuagua watu.

Kingine ni kwamba dini za Kiafrika hazikuwa na miongozo ya maandishi wala vitabu kama zilivyo za wenzetu, miongozo hiyo huwa ndio kama katiba au kanuni za kuziongoza.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, dini hizi za Wazungum, Waarabu na Waasia japo nazo hazipo sahihi kwa asilimia mia moja lakini hauwezi ukazilinganisha na dini za Waafrika, inawezekana nazo zimesababisha madhara fulani kwa wanadamu lakini ni ukweli pia mafundisho yake yameleta ustaarabu kwa kiasi fulani Duniani. Kwanza zimeweza kuwaunganisha idadi kubwa ya watu duniani, zinahubiri kuwepo kwa NGUVU kuu kuliko zote(MUNGU), Zinahubiri ustawi wa binadamu kama suala la watu kuwa na afya njema, elimu na watu kutendeana mema. Dini ya namna hiyo sidhani kama ina ubaya kwa mtu labda tu kuwe na wapotoshaji katika dini husika wanaohubiri vitu vinavyoleta madhara mabaya kwa binadamu wengine.
 
Umu ndani kila mtu anamlalamikia muafrcia, ni muafrica yupi uyo? aya tusaidiane kwasisi wachache tuliokua apa ni hatua gani za awali mmeanza kuchukua ndugu zangu? maana uyo beberu katushika pabaya sana, 90% ya tunachotumia kimehusika na mzungu, Wengi mnalalamika utafikiri uyo muafrica hatokani na sisi, kama vijana waelewa ni solution ipi mmekuja nayo na mmeanza na hatua zipi za awali.
 
Hii sababu ya kutawaliwa, kutawaliwa ni kubaya sana, waafrika tumepoteza vitu vingi sana vya maana. Usidanganyike ndugu waafrika tuna dini zetu nzuri sana kutojua na hazina tofauti yoyote ile kubwa na hizi dini za mapokeo.
 
Mkuu mko sawa kabisa. Miaka ya hivi karibuni namimi nimestuka, baada ya kuona hali inavyokwenda. Kiukweli Niseme kuwa ' Things has fallen apart' Ukichanganya Rangi, Ufukara ni wepesi mtu mjanja kupandikiza uongo ikawa kama gundi kichwani.

Just imagini kuna Mchungaji alikuwa hana kitu, kaja na mbwembwe za kuombea watu wenye shida mbalimbali, alikuwa wakawaida lakini alifanikiwa kuwa anakuja na wazungu anawaita mbele wanasalimia waumini, ila malazi nachakula, Kanisa lina wahudumia. Mbaya zaidi huwezi kutaja mchango kimya kimya, unapewa microphone ukiwa mbele ya waumini, ili ushangiliwe.

Niseme tu kwa ufupi, sasahivi huyo mchungaji amenunua Gorofa Masaki na anaendesha ' HAMA" na VX magari ya kifahari. Mishahara yao naijua ukifanya hesabu mpaka kustaafu kwake hata bei ya gari moja haitoshi. Sasa najiuliza Msisitizo wa saadaka mbona ni kila wakati? Kumbe walio wengi wanadhani wanamtolea Mungu kumbe ni zake na ni Tax free!!!
Waafrika tumeshachemka tayari, bora Mababu zetu hawakuwahi kukutana na utapeli kwa kusingizia Mungu na kuwaambia walipe fungu la kumi na malimbuko na sadaka rukuki huku wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa, huku wachungaji wakifanikiwa kuwa matajiri wa kutupwa.

Kwa hali iliyopo sasa Viongozi wa kiserikali wasipoingilia kati, umasikini utaongezeka kwani hata katikati ya wiki kuanzia saa 4 za asubuhi kuna kuwa na Ibada na maombi siku 40. Sasa najiuliza, hivi ni Mungu gani anayetumia muda mwingi kwenye maombi? Kazi za kumletea mtu kipato zinafanyika saa ngapi?. ' HILI NI JANGA JIPYA KWENYE HIZI DINI ZA KIDHUNGU"
 
Umetowa wpi hii kuwa miungu iligawana mabara? Leteni ushahidi ili mutupe nguvu ya hoja.
 

Umejenga hoja murua kuzisemea dini za kiafrika.
Lakini mimi napata shida moja,kule kwetu Giningi kuna mahali wachawi wanakutana kufanya wayafanyayo ya kimila.

Kule Rufiji hujengwa vibanda vya kinyamkela,
Kule moshi ndowatu huenda kwenye mlima Uleee mrefu K/Njaro NK ,lakini waabudu hao wote hakuna andiko wala dalili ya kimaono iliyowazi kushuhudia uwepo wa yule wanayemuabudu.
Wote wanamuabudu au kumtumikia Shetani ambaye hutolewa matambiko na kuondowa mateso kwa wamuaminio.

Kweli watu waliheshimu hizo mila na kuwa na nidhamu fulani,ila hakuna hatua yoyote iliyofuatia baada ya kucheza ngoma na kula vibudu,watu hawa walibaki mafukara ,wagonjwa,na hawakuwa nauwezo wa kuyamudu mazingira yao wenyewe,Mpaka walipokuja wageni wenye dini za kiasia na kuanza kuwaelimisha dini zao na elimu zao na kuwasaidia kujiboresha kimazingira.

Hakuna mwafrika hata mmoja aliyegundua chchote cha kumsaidia binadamu zaidi ya kuvaa magome ya miti na panga na mkuki wa kuwindia ,basi.
Hatukujuwa na bado hatujuwi thamani ya Madini tuliyonayo kwenye nchi zetu wenyewe.Hio miungu yetu haikutusaidia lolote na haitusaidii hadi leo pamoja na kuwa bado baadhi yetu tunaikweza na kuipa matambiko.

Uuwaji wa Maalbino na kutowa kafara mbali mbali kule migodini hakukusaidia kuitowa dhahabu wala Tanzanite kwenye migodi na kuileta juu ili tupate maslahi.lakini Wazungu wameleta Mamashine makubwa ambayo kwayo milima hutawanywa na Dhahabu kutolewa na kuwanufaisha wachimbaji husika.

Magari,Matreni,Ndege,na baskeli zote hutoka kwao.ndo maana wakisema hata wao kuwa ni miungu tunaweza tukawa na sababu ya kuwaabudu.Kwa kuwa wanacho cha kutonesha cha maajabu na ambacho sisi hatuwezi kukitengeneza.Hii computer na Simu ni maajabu tosha ya kuamini kuwa mvumbuzi wake anaweza kuitwa mungu.lakini waungu wale wa kunywa damu na kupigiwa ngoma ni lazima watoweke sasa na hawana tena watu wa kuwaamini isipokuwa mapunguwani.


sasa hapa swali ni moja
NI IPI DINI SAHIHI NA YA KWELI? NITAKUFUNULIA UKINIHOJI
 
Acha kwenda kanisani kabisa. Uendelee kutambika. Acha kuwa ndumilakuwili. Usiionee haya hiyo imani/dini yako ya Kiafrika unayoipenda huku unaiendea kwa kujificha. Hakuna atakaekuzomea.
 
umesema sawa 100% niko pamoja na wewe umefafanua vilivyo na nadhani hata mimi umenifilisi. ☑ 👍
lakini hapa kidogo ulipo sema ''japo nazo hazipo sahihi kwa asilimia mia moja'' panahitaji uchambuzi.mdoogo.
Miungu ipo mingi kama zilivyo dini zenyewe,Ila miungu hio inajifafanua kutokana na imani husika nakwa hiyo dini hiyo huwa sahihi kwa mujibu wa hichi kitabu naimani iliyomo humo kwa waamini wake tu.
lakin iko dini Inayoziunganisha dini zooote ambayo imezi taja na kuzikosowa na kutowa njia ya kati iliyo nyooka kwa ini zote ,kwa mujibu wa dini hiyo,hizo dini zote zimejumlishwa na kufanywa moja na Muumba mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…