Ukweli usiowekwa wazi: Hayati Nyerere aliacha taifa letu likiwa masikini sana kiuchumi pamoja na kutoa msaada kwa nchi za jirani

True
 
Wewe, Mwalimu ni 'Mwenye heri' haambiwi hivyo!
 
Kwa Kila Mwenye Ubongo Unaofanya Kazi Akiweka Mahaba Na Pembeni Hisia Pembeni, Huyo Mzee Lazima Achanwe Kwa Maamuzi Yake Ya Hovyo Yanayoligharimu Taifa Hili Mpaka Hii Leo,
We ni mpumbavu.
Aliondoka madarakani tangu 1985.Leo miaka 38.
Utakuwa ni zaidi ya mpumbavu kumlaumu juu ya matatizo unayopata sasa
 
We ni mpumbavu.
Aliondoka madarakani tangu 1985.Leo miaka 38.
Utakuwa ni zaidi ya mpumbavu kumlaumu juu ya matatizo unayopata sasa
Wewe ndio mpumbavu kama alifanya makosa watu wasisime
 
Alijenga au alirithi kwa wakoloni?

Anyway katika maraisi wenye umuhimu kwa Tanganyika nyerere still namba 1.
 
Nyerere ndo sababu kuu ya umasikini wetu
 
Utajiri ni nini ?

Ni sawa wewe Babu yako hakuuza shamba (na angeweza kuliuza) leo hii wewe unauza kila kitu alafu unasema hio nyumba aliyoacha hakukuwekea bati ndio maana sasa hivi limeoza

Unaweza kuniambia ratio ya shule na ajira zilizokuwepo na uhitaji wa sasa na kipindi yeye yupo ? Hivi unadhani tungekuwa na uwezo wa kukusanya kodi wa sasa (control number) ni mangapi yangefanyika ?

Nyie ndio wale unamlaumu Babu yako kwa Sura yako mbaya (hence haupati wachumba) sababu alimpenda bibi yako mbaya na sio mwenye sura nzuri..., wakati na wewe unaweza kutafuta wachumba unaoendana nao....
 
Wakati anafanya hayo yote,wanafunzi walisoma bure wakipewa madaftari na kalamu shule za msingi,Sekondari walilipiwa nauli ya kwenda na kurudi.Walipewa chakula bure,Vyuo vyote vya kati na chuo kikuu,walipewa chakula au posho ya kujikimu.Walisoma bure.
Ni kiongozi pekee aliyesomesha watu wake wengi sana nje ya nchi Russia,China,India,Cuba,Uingereza,Marekani n.k kwa gharama zote za seikali.

Hospitali zote wananchi walitibiwa bure kabisa.Wagonjwa wote na ndugu zao walilishwa bure hospitali,milo mitatu na matunda.
Mungu ampumzishe kwa amani
 
Kwa Kila Mwenye Ubongo Unaofanya Kazi Akiweka Mahaba Na Pembeni Hisia Pembeni, Huyo Mzee Lazima Achanwe Kwa Maamuzi Yake Ya Hovyo Yanayoligharimu Taifa Hili Mpaka Hii Leo,
Aliondoka madarakani 1984 leo ni 2023 takribani miaka 39 tangu atoke madarakani.
Bado unamlaumu kwa kipi?
 
We ni mpumbavu.
Aliondoka madarakani tangu 1985.Leo miaka 38.
Utakuwa ni zaidi ya mpumbavu kumlaumu juu ya matatizo unayopata sasa

Mpumbavu ni baba yako na mama
yako waliokuzaa. nini
kinazuia mabadiliko katika nchi hii kama sio katiba yake mbovu?
 
Aliondoka madarakani 1984 leo ni 2023 takribani miaka 39 tangu atoke madarakani.
Bado unamlaumu kwa kipi?

Katiba Mbovu Ya Nchi Hii Iliyomfanya Rais Kuwa Kama Mungu Kaileta Nani?
 
Kimsingi hali ya uchumi na Ustawi wa Tanganyika ilikuwa nzuri wakati wa mkoloni.kuliko wakati wa Nyerere na ndio sababu za kung'atuka.

Na alivyokuwa hazimtoshi hakutaka kusomesha Elimu ya maana kwa sababu tuu alikuwa muoga wa Changamoto kutoka Kwa wasomi.

Ndio maana ukishaona Kiongozi anatumia propaganda saana na maneno meeengi ujue hamna kitu hapo..

Tumshukuru Kwa kuondoa ukabila,udini na sera nzuri za Ardhi.
 
Mpumbavu ni baba yako na mama
yako waliokuzaa. nini
kinazuia mabadiliko katika nchi hii kama sio katiba yake mbovu?
Hivi unajua Katiba ni Sheria ? Na kama sheria nyingine za kila siku zinavunjwa kila kukicha ambazo zipo wazi kabisa unadhani ni nini kitafanya hawa hawa wasiofuata sheria kuvunja na hio so called nzuri ?
 
Katiba Mbovu Ya Nchi Hii Iliyomfanya Rais Kuwa Kama Mungu Kaileta Nani?
Miaka 39 kama nchi tumeshindwa vipi kuibadirisha hadi tumsingizie mzee wetu?
Katiba iliyopo ilifaa kwa kipindi kile.
Hata yeye Nyerere aliwahi kusema katiba sio msahafu"
Wakulaumiwa ni wewe uliye hai na unaona kuwa katiba inahitaji mabadiriko lakini hufanyi mabadiriko unataka marehemu ndio wafanye mabadiriko.
 
Ilikuwa nzuri kwa nani ? Muindi, Muarabu au Mbantu..., Ilikuwa nzuri sehemu gani ? Sehemu ambazo wamisionari walikuwa wengi na kuwekeza au Tangayika nzima mpaka kusini ?

Nyerere alijenga umoja wa Kitaifa (kuna shule mbantu usingesoma bila kutaifisha na kusema tuanze moja)..., Ni sawasawa mzee wako amejenga msingi imara wewe kapuku baada ya miaka kadhaa unalaumu kwanini hakujenga ghorofa..., wakati huenda ni opportunity ya kujenga unayotaka leo badala ya angekujengea ingekuwa imepitwa na wakati hence ungehitaji kuvunja....
 
Baada ya kuondoka Wazungu Kwa nini Haki isiendelee kuwa nzuri na badala yake Kila kitu kikahatibika?

Bila Wazungu Nyerere angesoma?
 
Baada ya kuondoka Wazungu Kwa nini Haki isiendelee kuwa nzuri na badala yake Kila kitu kikahatibika?

Bila Wazungu Nyerere angesoma?
Hivi unajua kulikuwa na Classes za Raia aina kama nne; Wazungu, Wahindi, Waarabu na Mwisho wabantu ? Unadhani wewe ungeweza kusoma shule za wahindi au kama baba yako sio chief au mzee wa kanisa ungesoma na machief...., tungeweza kwenda Kenya Route ubepari na familia ya Nyerere kuchichotea ardhi yote kama Familia ya Kenyatta na wengine kuendelea kuwa watazamaji au unadhani hilo lisingewezekana ?

Cha maana ni msingi wa Umoja wa Utaifa / Undugu hayo mengine yote unaweza kuamua hata kuanzia kesho ukayatafuta...., kama ni viwanda vya nguo anzisha, kama ni viwanda vya kubangua korosho anzisha (ila cha ajabu watu mnasema hakuna tunachoweza hivyo tuwape wengine wafanye)..., so unless Nyerere aliwaroga hawa watunga sera sioni kwanini alaumiwe....
 
ok sawa
 
Hili la kupanga watu kwenye vijiji vya ujamaa pamoja na kwamba lilifanywa kwa ukatili na udhalilishaji ila lingeendelezwa na tawala zilizofuata si ajabu REA na RUWASA zingeshafikia 98% ya kaya zote nchini.

Ilikuwa rahisi mno kwa serikali kupatia wananchi hudumu za jamii wakiwa wanaishi pamoja tofauti na hii scattered settlement ya sasa.

BTW:Mzee alikuwa busy kujenga legacy yake tu,hayo "maukombozi" hayana tija kwa nchi wala raia wa kawaida.

Mwenye picha yoyote ya VP au PM wa Nyerere akiwa na hao akina Kaunda,Samora
,Neto, Mandela,Mugabe,Castro etc aiweke hapa!

Huo mchakato alikuwa ameuhodhi kwelikweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…