Imagine nyerere angekuwa kama viongozi tulionao sasa kisha ujibu mwenyewe ... Mnaomtukana nyerere ni vijana mliozaliwa miaka 1990.
Nyerere aliacha shirika la ATCL linafanya safari ndani na nje ya nchi. Aliacha TRC na Tazara zikifanya kazi ya usafirisha wa abiria na mizigo kwa kiwango.
Nyerere aliacha nchi ikiwa na viwanda vya kutosha vilivyokuwa vinatoa ajira Textile industries, Tyres Industry, Automobile Industry, cement industries, electronic industries (kiwanda cha redio), viwanda vya kusindika na kuchakata mazao zikiwa katika mfumo wa Cotton Ginnery na National Milling karibu kila wilaya vilikuwepo. Viwanda vya viatu (Bora shoes).
Aliweka mkakati ya kujenga bwawa la kuzalisha umeme kwenye stiggler gorges miaka hiyo.
Aliacha mfumo wa elimu wenye focus ya kuzalisha wabunifu elimu ya leo ni knowledge based.
Aliacha Tsh ikiwa na nguvu.
Hakuwahi kuingia mikataba yenye harufu ya kuuza rasilimali za nchi.
Yako mengi sana.
Iwapo tungefanya jitihada ya kuyaandeleza nchi yetu ingekuwa ni miongoni mwa nchi tatu zenye uchumi imara Afrika.
Aliyoacha nyerere kama tungekuwa positive