Ukweli usiowekwa wazi: Hayati Nyerere aliacha taifa letu likiwa masikini sana kiuchumi pamoja na kutoa msaada kwa nchi za jirani

Nyerere aliendesha nchi bila kubinafsisha mgodi hata mmoja wa dhahabu pamoja na kujua hazina tuliyonayo, bila kuuza rasilimali za Taifa Leo hii Tena tupo kwenye mgao wa umeme Kuna watu wanapaza shingo kumlaumu. Hiyo mikataba ya gesi, dhahabu, loriondo iliyoingiwa baada ya yeye kutoka imeisaidia Nini Taifa.
 
Yeye aliwezaje kusoma katikati ya hizo classes? Kwani Sasa hivi hazipo?
 
Hivi unajua Katiba ni Sheria ? Na kama sheria nyingine za kila siku zinavunjwa kila kukicha ambazo zipo wazi kabisa unadhani ni nini kitafanya hawa hawa wasiofuata sheria kuvunja na hio so called nzuri ?

Naona unacomment kwa kuweka mahaba mbele kuliko uhalisia.wewe msomi mzima unaijua hadi jamiiforms unajifanya hujui athari
za katiba mbovu ya nchi hii kwa wasimamizi wa sheria kaika kutekeleza majukumu yao? vitu vingine bora ukae kimya,unajidhalilisha,
 
Huu ni mtazamo finyu kutoka kwako mtoa mada japo una uhuru wa kutoa maoni.

Sijawahi kumkubali mtu yeyeote anaye link matatizo yetu ya sasa na J K Nyerere. Nyerere hadi 1985 katawala miaka 24.

1985 mpaka leo ni miaka 38, halafu vichwa 5 baada ya Nyerere bado tuendelee kumlaumu yeye ? Not fair at all.

Yaani 60% ya Watanzania wamezaliwa baada ya yeye kuacha madaraka, bado kweli tuendelee kumlaumu?

Na 40% wamezaliwa 2000 kuja huku mbele wamekuta amekufa, nao wanamlaumu Nyerere.

Nyerere aliondoka hajachimba madini instead aliacha ameyahifadhi kwa ajili ya kizazi hiki na cha baadaye. Na utajiri uko kwenye madini, bado TAKATAKA kama Muuza Kangala zinamlaumu

Bagonza abakie kwenye madhabahu tu
 

umekubali Katiba Ni Tatizo Hito Aliyeileta Alileta Tatizo.

Hebu Niambie Kwa Namna
Gani Ilifaa Kwa Kipindi kile?

na kwa nini wewe hujachukua hatua kuibadilisha?
 

mkuu ww umeifanyia nini hii nchi???… naamini hamna kwene kizazi chako had unakufa Hamna mtu ambaye anaweza akaleta mchango mkubwa kama Nyerere!!…
 

mkuu ww umeifanyia nini hii nchi???… naamini hamna kwene kizazi chako had unakufa Hamna mtu ambaye anaweza akaleta mchango mkubwa kama Nyerere!!…
 
Mpumbavu ni baba yako na mama
yako waliokuzaa. nini
kinazuia mabadiliko katika nchi hii kama sio katiba yake mbovu?
Umeshindwa nini kuibadili?
Ninyi ndio vijana wa hovyo sana.
Wakati wa Nyerere kulikuwa na vijana waliothubutu kujaribu kumuangusha Nyerere leo kama kweli unaumizwa na katiba unadhani ukija humu na huu upumbavu wako nini kitabadilika?
 
Utapataje mtu makini wa kutuvusha wakati namna ya kumchagua tu ilishanajisiwa tokea enzi zake. Kwa mfano wakati wa kuingia mfumo wa vyama vingi 1992 uliwekwa mfumo wa makusudi 100% wa kihuni ili kubeba watu Fulani Sasa hapo utapataje mtu makini. Katiba mbovu kama hiyo utapataje mtu makini. Kupata mtu makini yapo yanayotangulia kwanza ili kumfikia huyo mtu makini kwa mf katiba nzuri, tume huru ya uchaguzi nk
 
Aliyekwambia mimi msomi ni nani ? Kwahio wewe kama unadhani kuwa na Sheria bora ni Bora kuliko kufuata hizo sheria zilizopo Hongera sana kwa uelewa wako ila kwa taarifa yako unakachofanya sio kuondoa mzizi wa matatizo ni kama vile unaya-pruni magugu badala ya kuyangoa....

Ngoja nikupe mfano mmoja wa kuvunja Katiba achana na sheria nyingine zinazovunjwa kila dakika Mtikila alishinda kabisa Kesi kwamba kutokuwa na Mgombea Binafsi kunakiuka Katiba..., unajua what happened walirudi wakabadilisha kifungu retrospectively wakaendelea na kanyaga twende.... (hence umuhimu wa watu kufuata sheria na uzalendo is more important)
 
Kuna dini miaka hizo hazikuwa na wasomi. Wenyewe mpaka leo bado wanataka mtoto wa miaka 14 asiende shule bali aolewe
 
Mpumbavu ni baba yako na mama
yako waliokuzaa. nini
kinazuia mabadiliko katika nchi hii kama sio katiba yake mbovu?
Halafu 1985 alivyo staafu akatuwekea Rais wa hovyo,Salim Ahmed Salim ndiye alifaa kutuongoza tungefika mbali
 
Hakuna kitu, soma kitabu cha mwinyi uone, hivyo viwanda vyote nyerere kaviacha vikiwa kwenye hasara, havikuweza kuendana na technology ya kipindi hicho + mitaji hatukuwa nayo as vingi tulikuwa tunapewa misaada, yan tulikuwa tunatoa pesa serikalini ili kuendeleza hivyo viwanda,


Nyerere as president was big failure
 
Sawa wewe sio msomi lakini the fact mwamba unajua umuhimu wa katiba matter most here.
Hiyo kufuata sheria itakuja baada ya kila muhimili kuachwa ufanye kazi yake.
Unataka kusema hujui kuwa katiba ya nyerere imemerge mihimili yote nchi hii into one ???
Raise anateua majaji, watawezaje ku act dhidi ya interest zake???
Wabunge wanaopitisha Mambo bila kuhoji unadhani wanapenda???
Tatizo Ni mifumo mibovu iliyotokana na katiba mbovu ambayo nyerere kaleta.

Mark milley, us too general alipoulizwa wao Kama jeshi watafanya Nini Kama Trump angegoma kutoka madarakani, alisemaa wao watamuondoa kwa nguvu ili kudumisha utaratibu wa kikatiba.
Alisemaa hivi kwa kujiamini kwa sababu ya mfumo Bora wa katiba uliowafanya wao kuwa huru ku act.

Sasa bongo unaweza kufanya maamuzi dhidi ya aliyekuteua??
 
Vijana mapunga wanataka Nyerere angemaliza kila kitu na changamoto.

Wao hawataki kufanya chochote, wanataka bata tu. Ni Kama mibata bukini tu,
 
Hoja yako ni ipi?
 
Umeshindwa nini kuibadili?
Ninyi ndio vijana wa hovyo sana.
Wakati wa Nyerere kulikuwa na vijana waliothubutu kujaribu kumuangusha Nyerere leo kama kweli unaumizwa na katiba unadhani ukija humu na huu upumbavu wako nini kitabadilika?
Kijana wa hovyo baba yako. Wewe kwako hiyo katiba Ni right??
Au Ni means ccm wewe una benefit na upumbavu wa huyo mzee??? Kwa Nini usibadilishe??? Humu tunamchana huyo mzee ambaye ninyi mnamuona wa maana sana na kujizuia msiangalie matakataka akiyofanya.
 
Anza kwamza ku.laumu babako kwa kukuacha katika umaskini.

Nyerere alitoa elimu bure kuanzia primary hadi cbuo kikuu jambo lililowezesha watoto wa maskini tena kutoka makabila yasijua umuhimu wa elimu kusoma, bila hivyo zingesoma familia zile za makabila machache yaliyokua yameamka kama wachaga wahaya na wanyakyusa. Wazazi walilazimishwa kupeleka watoto shule. Matibabu hospitali yaliikuwa bure.
NYerere wakati anapokea uhuru hakukuwa na chuo kikuu lakini alijenga vyuo vikuu viya UDSM, IFM, IDM( mzumbe) nz vyuo vingi vya kati vya elimu, uganga ufundii ili Taifa liwe na wataalamu wa kada ya kati wengi,.

Hakukuwa na viwanda lakini Nyerere alijenga viwanda vingi vya msingi na vya bidhaa i.e. vy cement 3, nguo, kiwanda cha chuma, zana za kilimo , karatasi nk.


ETi shule zilikuwa chache unashindwa hata kuchambua data za populatkon! Watu milioni kumi wakati wa uhuru na hadi anaaondoka madarakani watu walikuwa milioni 23 tu ulitaka idadi ya shule iwe sawa na sasa watu milioni 60? Kila kijiji kilikuwa na shule ya msingi hayo sio mafanikio? Kiuchumi hakuna mtu anaweza kufanya kila kitu lazima achague vipaumbele vichache katika elimu Nyerere alitaka kila mtu apate elimu ya msingi kwanza na pia tujitosheleze kwa wataalamu wa ngazi ya kati.

Nyerere alijenga reli ya Tazara.

Madini aliamua yasichimbwe kwanza hadi watanzania wawe na elimu ya kuyasima.ia vizuri wao wenyewe halafu unamlaumu! Je wale walioingiza nchi katika mikataba ya kiMangungu unawapa sifa zipi?

Umaskini waki haukuletwa na Nyerere.
 
Kwani kalaumi1a nini?
 

Ushauri wangu vijana tuache kulaumu nyerere

Tunafanya na kizazi chetu ili tukumbukwe? Siyo kulaumu tufanye jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…