Ukweli usiowekwa wazi: Hayati Nyerere aliacha taifa letu likiwa masikini sana kiuchumi pamoja na kutoa msaada kwa nchi za jirani

Ni "Kangara" zilizojaa kichwani, hakuna anayeweza kukulaumu kwa hilo.

Hizo kangara zikiisha na ukawa na akili timamu, rudi hapa tujadili (?); hapana, "ufunzwe" wanayojua wanayojua wenye akili timamu.
 
Zile zilikuwa zama za, Vita baridi, alifanya makosa, lakini kuna mengi mazuri alifanya, kumuhukumu kwa Mabaya aliyofanya kipindi kile,kwa kuangalia Leo, sio, sahihi,
Nyerere ndie aliyejenga umoja wa, makabila yote 143! Tukaweza kuzungumza lugha moja,
Hii Hari haikushuka, tu, ilijengwa,
We ulitaka afanye nini, huku kuna Mabepari na kubwa Lao USA, kule kuna wajamaa China na, urusi!
Alitujengea, heshima kubwa kupitia Tume ya ukombozi, kusini mwa Afrika, China ya, Major Hashim Mbita, majasusi wetu walikuwa wanajua kukiwasha kuanzia Msumbiji, South, Zimbabwe, Angola, mpaka Namibia,
Ukifika Morogoro, au Iringa, kuna maeneo yanaitwa Soweto, hayo majina hayakuja tu, ni regacy ya ukombozi, makambi ya wapigania haki, nenda Lindi, Masasi,nachingwea, ukaone ilipo Farm 17,ndio utajua ndoto alizokuwa nazo, Nyerere,
Nchi ilikuwa na wasomi wachache, rasilimali nduni,
Sio, busara, kulaumu waliopita, SEMA wewe sasa hv unafanya nini?
After 30+yrs viongozi wetu wapo bize kufukuzia degree za heshima, na kukuza profile zao kisiasa!
So pathetic,
Baada ya Urusi kusambaratika, ambayo ilikuwa nguzo, ya wajamaa kama Nyerere, akaona hapa akiendelea kubaki ikulu, mazungu yatamchomoa, akaachia, ngazi! 1985+kutoka 1985+mpaka Leo, bado unamlaumu nyerere! Bro be serious!
Richmond, EPA, meremeta, bandari, madudu yote haya bado unasema nyerere ndio chanzo! Ur fucking kidding bro!
Let's be serious!
 
Kiongozi unafanyiwa assessment kwa matokeo ya maamuzi yako sio nia yako
"Catch phrase" nzuri sana kuisikia, hasa kwa watu waliolaza akili kichwani.

Fanya 'assessment' yoyote unayotaka kufanya juu ya utawala wa Mwalimu Nyerere tuone ni lipi hasa litakalobeba usahihi wa msemo huo.
 
Hivi unajua Katiba yako kweli ? Hujui kabisa kwamba kuna Separation of Power katika Katiba yako.., ingawa ndivyo navyosema Katiba na kufuata Katiba ni vitu viwili tofauti
Raise anateua majaji, watawezaje ku act dhidi ya interest zake???
Kwamba unadhani Jaji mwenye principles atafuata kitu sababu Rais alimteua ? na mtu wa hivi unadhani hata Rais asipomteua ataacha kuchukua mlungula ?
Wabunge wanaopitisha Mambo bila kuhoji unadhani wanapenda???
Kwamba Rais anaweza kumu-punish Mbunge How ? Au hujui kwamba hii ni kutokana na Magenge ya Vyama kila Wabunge kutetea ya Chama chao no matter kizuri au kibaya na vice versa..., ndio maana nikasema hawa wote ni wa kupiga chini....

Tatizo Ni mifumo mibovu iliyotokana na katiba mbovu ambayo nyerere kaleta.
Kwamba kulikuwa na Angalizo kwamba hio so called Katiba ya Nyerere haiwezi kubadilishwa kamwe ?!!!
Unadhani hata huku Jeshi ukilipa leeway na wananchi wakaonekana kuliunga mkono au kukubaliana nalo litashindwa kumuondoa mtu yoyote pale...., leo hii Rais yoyote ashindwe unadhani itakuwa kazi kumtoa ? Au no matter Katiba ipoje na mahakamani mtakwenda ila kwa mfumo wake wa wizi na pesa alizoiba ataweza kutumia mlungula kuendelea kubaki alipo ?
 
Wakati wa Nyerere hakukuwa na unemployement kila mtu kuanzia darasa la saba hadi chuo kikuu aliweza kuajiriwa tena bila kulazimika kumjua mtu. Pia ikitokea mtu hana ajira ya kuajiriwa aliweza kupewa ardhi bure na kulima na kujipatia kipato. Leo hii kuna mamilioni hawana kazi na pia hata wakitaka kulima hawana ardhi ya kulilma
 
acha uongo. Mwalimu hakuacha lolote la maana kiuchumi. Aliacha nchi ikiwa hoi. Hata kung'atuka alilazimika. Baada ya vita vya Kagera nchi haijawahi kurudi ilipokuwa kabla ya vita. Hayati Mkapa ndo alifanya makubwa kiuchumi.
 
umekubali Katiba Ni Tatizo Hito Aliyeileta Alileta Tatizo.

Hebu Niambie Kwa Namna
Gani Ilifaa Kwa Kipindi kile?

na kwa nini wewe hujachukua hatua kuibadilisha?
Unajua maana ya katiba?
Unadhani Rais pekee anaweza kutunga katiba?
Katiba ni muongozo wa nchi sio muongozo wa familia ambayo baba anaamua muishije ndani. Kwenu
 
Na tuna uwezo wa kukusanya Kodi maradufu.., Kodi ambayo walamba asali hata wasipoweka sera za kuleta ajira zenye ujira kwa watu hakuna wa kuwaambia kitu..., yaani wanafanya kwa kujisikia, ukiuliza eti sio jukumu la Serikali....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…