Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zile zilikuwa zama za, Vita baridi, alifanya makosa, lakini kuna mengi mazuri alifanya, kumuhukumu kwa Mabaya aliyofanya kipindi kile,kwa kuangalia Leo, sio, sahihi,Alisaidia na kukomaa mataifa ya jirani yapate uhuru akasahau kabisa kuendeleza taifa letu.
Kauli mbiu ya kuwa sisi kuwa huru huku majirani zetu hawako huru sio vyema ilifanya akasau kuendeleza taifa letu.
Aliacha miundo mbinu iko hovyo, shule chache, hospitali chache na kila kitu kikiwa hovyo.
"Catch phrase" nzuri sana kuisikia, hasa kwa watu waliolaza akili kichwani.Kiongozi unafanyiwa assessment kwa matokeo ya maamuzi yako sio nia yako
Hivi unajua Katiba yako kweli ? Hujui kabisa kwamba kuna Separation of Power katika Katiba yako.., ingawa ndivyo navyosema Katiba na kufuata Katiba ni vitu viwili tofautiSawa wewe sio msomi lakini the fact mwamba unajua umuhimu wa katiba matter most here.
Hiyo kufuata sheria itakuja baada ya kila muhimili kuachwa ufanye kazi yake.
Unataka kusema hujui kuwa katiba ya nyerere imemerge mihimili yote nchi hii into one ???
Kwamba unadhani Jaji mwenye principles atafuata kitu sababu Rais alimteua ? na mtu wa hivi unadhani hata Rais asipomteua ataacha kuchukua mlungula ?Raise anateua majaji, watawezaje ku act dhidi ya interest zake???
Kwamba Rais anaweza kumu-punish Mbunge How ? Au hujui kwamba hii ni kutokana na Magenge ya Vyama kila Wabunge kutetea ya Chama chao no matter kizuri au kibaya na vice versa..., ndio maana nikasema hawa wote ni wa kupiga chini....Wabunge wanaopitisha Mambo bila kuhoji unadhani wanapenda???
Kwamba kulikuwa na Angalizo kwamba hio so called Katiba ya Nyerere haiwezi kubadilishwa kamwe ?!!!Tatizo Ni mifumo mibovu iliyotokana na katiba mbovu ambayo nyerere kaleta.
Unadhani hata huku Jeshi ukilipa leeway na wananchi wakaonekana kuliunga mkono au kukubaliana nalo litashindwa kumuondoa mtu yoyote pale...., leo hii Rais yoyote ashindwe unadhani itakuwa kazi kumtoa ? Au no matter Katiba ipoje na mahakamani mtakwenda ila kwa mfumo wake wa wizi na pesa alizoiba ataweza kutumia mlungula kuendelea kubaki alipo ?Mark milley, us too general alipoulizwa wao Kama jeshi watafanya Nini Kama Trump angegoma kutoka madarakani, alisemaa wao watamuondoa kwa nguvu ili kudumisha utaratibu wa kikatiba.
Alisemaa hivi kwa kujiamini kwa sababu ya mfumo Bora wa katiba uliowafanya wao kuwa huru ku act.
Sasa bongo unaweza kufanya maamuzi dhidi ya aliyekuteua??
Wakati wa Nyerere hakukuwa na unemployement kila mtu kuanzia darasa la saba hadi chuo kikuu aliweza kuajiriwa tena bila kulazimika kumjua mtu. Pia ikitokea mtu hana ajira ya kuajiriwa aliweza kupewa ardhi bure na kulima na kujipatia kipato. Leo hii kuna mamilioni hawana kazi na pia hata wakitaka kulima hawana ardhi ya kulilmaUtajiri ni nini ?
Ni sawa wewe Babu yako hakuuza shamba (na angeweza kuliuza) leo hii wewe unauza kila kitu alafu unasema hio nyumba aliyoacha hakukuwekea bati ndio maana sasa hivi limeoza
Unaweza kuniambia ratio ya shule na ajira zilizokuwepo na uhitaji wa sasa na kipindi yeye yupo ? Hivi unadhani tungekuwa na uwezo wa kukusanya kodi wa sasa (control number) ni mangapi yangefanyika ?
Nyie ndio wale unamlaumu Babu yako kwa Sura yako mbaya (hence haupati wachumba) sababu alimpenda bibi yako mbaya na sio mwenye sura nzuri..., wakati na wewe unaweza kutafuta wachumba unaoendana nao....
acha uongo. Mwalimu hakuacha lolote la maana kiuchumi. Aliacha nchi ikiwa hoi. Hata kung'atuka alilazimika. Baada ya vita vya Kagera nchi haijawahi kurudi ilipokuwa kabla ya vita. Hayati Mkapa ndo alifanya makubwa kiuchumi.Imagine nyerere angekuwa kama viongozi tulionao sasa kisha ujibu mwenyewe ... Mnaomtukana nyerere ni vijana mliozaliwa miaka 1990.
Nyerere aliacha shirika la ATCL linafanya safari ndani na nje ya nchi. Aliacha TRC na Tazara zikifanya kazi ya usafirisha wa abiria na mizigo kwa kiwango.
Nyerere aliacha nchi ikiwa na viwanda vya kutosha vilivyokuwa vinatoa ajira Textile industries, Tyres Industry, Automobile Industry, cement industries, electronic industries (kiwanda cha redio), viwanda vya kusindika na kuchakata mazao zikiwa katika mfumo wa Cotton Ginnery na National Milling karibu kila wilaya vilikuwepo. Viwanda vya viatu (Bora shoes).
Aliweka mkakati ya kujenga bwawa la kuzalisha umeme kwenye stiggler gorges miaka hiyo.
Aliacha mfumo wa elimu wenye focus ya kuzalisha wabunifu elimu ya leo ni knowledge based.
Aliacha Tsh ikiwa na nguvu.
Hakuwahi kuingia mikataba yenye harufu ya kuuza rasilimali za nchi.
Yako mengi sana.
Iwapo tungefanya jitihada ya kuyaandeleza nchi yetu ingekuwa ni miongoni mwa nchi tatu zenye uchumi imara Afrika.
Aliyoacha nyerere kama tungekuwa positive
Unajua maana ya katiba?umekubali Katiba Ni Tatizo Hito Aliyeileta Alileta Tatizo.
Hebu Niambie Kwa Namna
Gani Ilifaa Kwa Kipindi kile?
na kwa nini wewe hujachukua hatua kuibadilisha?
Na tuna uwezo wa kukusanya Kodi maradufu.., Kodi ambayo walamba asali hata wasipoweka sera za kuleta ajira zenye ujira kwa watu hakuna wa kuwaambia kitu..., yaani wanafanya kwa kujisikia, ukiuliza eti sio jukumu la Serikali....Wakati wa Nyerere hakukuwa na unemployement kila mtu kuanzia darasa la saba hadi chuo kikuu aliweza kuajiriwa tena bila kulazimika kumjua mtu. Pia ikitokea mtu hana ajira ya kuajiriwa aliweza kupewa ardhi bure na kulima na kujipatia kipato. Leo hii kuna mamilioni hawana kazi na pia hata wakitaka kulima hawana ardhi ya kulilma