Waarabu na Wazanzibari ni ndugu wa damu na wa asili kabisa maana Waarabu ndio walioleta ukombizi kwa Taifa la Zanzibar.
Waarabu ndio watu walioweza kuishi kijamii pamoja na Wazanzibari kwa miaka mingi hadi kuchanganya damu na Wazanzibar walio wengi na kuishi km jamii moja tena kwa upendo kabisa.
Waarabu ndio walioipa Nchi ya Zanzibar hadhi na heshima kimataifa na kujulikana kama ni nchi, bila ya Waarabu hata hao Vibaraka CCM-ZANZIBAR wasingeweza kupata nyadhifa mbali mbali za utawala hapo Zanzibar badala yake wangekua tu ni watu dhalili kwenye mkoa wa Tanganyika.
Kwahiyo ni wazi kuwa Waarabu walikuja Zanzibar kwa ajili ya ukombizi na kuwasaidia Wazanzibari waweze kuwa watu wenye hadhi na kuheshimika dunianiani kote.
Mwarabu hivi sasa ndio anaeijenga Zanzibar sijamuona Mtanganyika akija kuekeza Zanzibar sekta muhimu kama bandari kujenga majumba viwanja vya ndege naona mikataba imetiwa na waarabu sijamuona hata mtanganyika mmoja au.
Tusisahau fadhila kwa Uchu wa Madaraka na Njaa. WENYE AKILI WAMESHANIELEWA!!
Na anaebisha Abishe kwa Hoja na sio Porojo
Waarabu kutoka Oman ni wavamizi na wakoloni kama wakoloni wengine.
Tuliwaita kweli waje watusaidie kupambana na wareno tukiamini ni ndugu zetu katika imani, lakini baada ya kumshinda mreno wakakhini na kutugeuka, wakamuua kiongozi wetu Mwinyi mkuu na kila aliyekuwa katika sirikali ya wanawanchi wa Zanzibari weusi.
KAMA UNABISHA UTULETEE USHAHIDI WAPI SISI WANAWANCHI WEUSI WA UNGUJA NA PEMBA TULISAINI KUWAKABIDHI MAMLAKA YA VISIWA VYETU.
Hizo ni alama za mtu mnafiki na fisadi katika ardhi, akiaminiwa anakhini.
Wakatutawala kwa ukatili mkubwa na ubaguzi usio na mithali, tukawa watwana na vijakazi katika nchi yetu wenyewe hapa Unguja na Pemba, Wakatuchuuza kama nazi ama karafuu, wakawabaka wakina mama na dada zetu ili hali dada zao ikiwa ni marufuku kwetu wanawanchi weusi.
Ifikie mahala tuheshimiane, madhila waliyopitia wazee wetu tangu mwanzoni mwa mwaka 1800 mpaka 1964 , takriban karne 2 ni balaa na doa jeusi baina yetu na hao waarabu. Matusi ya rejareja kama haya pelekeni kwenye vikao vyenu mkiwa wenyewe sio kwenye kadamnasi kama hii ya vizazi vya waathirika wa idhilali ya waarabu.
Utumwa+ukoloni mkongwe= Mwarabu.
Hatujasahau bado ni miaka takriban 60 tu imepita, tangu tupindue na kurejesha uhuru wetu kama binaadamu.
baada ya waarabu kutukalia kimabavu kwa miaka takriban 130.