SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Mimi nisipokula ugali week huwa nahisi kuhaha na nitautafuta kokote unakopatikana niukule kwanza.

Ugali huwa ni mtamu sana licha ya kwamba hauliki bila mboga ila utamu wake huwezi kuuona kama unakula kwasababu hauna machaguo mengine ya vyakula kwa maana huo ndio unakopatikana kutokana na budget yako, hapo lazima ukuchoshe.

Na hapo kwenye kula na mboga au bila mboga nadhani inaweza kumake sense ila ni kama inakuja halafu inakataa kwa maana ugali unatokana na mahindi au muhogo sasa ukiangalia mahindi ni kwamba yanauwezo wakutoa vyakula vingi ambavyo mtu anaweza kula bila mboga na the same kwa mihogo.

Kwahiyo maybe kinachofanya ugali ushindwe kuliwa bila mboga ni zile hatua za uandaaji wake Kwahiyo inawezekana kama kungekua na namna tofauti ya kuuandaa ugali basi ungeweza kuliwa bila mboga, kwa maana ugali hauwekwi chumvi hauwekwi mavuta hauwekwi nyanya wala kitunguu wala nazi wala chochote kile kama vyakula vingine vinavyoliwa bila mboga ila wenyewe ni maji na unga tu shwaaaaaaaa unakitoa kituuuuuu 😆😆😆

Ugali uheshimiwe guys.
Ugali nikiula hasa dona nausikia kabisa kwa bwana "Abdallah Kichwa wazi" anakuwa kapata stamina 😂😂😂
 
Mimi nilishakataa Biashara ya Wanangu Kulewa, Mihogo na Ugali nilishamuambia Wife siku ukipika ivo vyakula Watoto watengenezee Msosi wao mwingine, Ila mimi sasa siwezi maliza siku tatu sijala ugali nauelewa sana
 
View attachment 3114645

Ni Chakula cha ajabu huwezi kula bila mboga wala kunywea chai.

Ni chakula maarufu zaidi kwenye sehemu za mateso kama jela, watoto wasiojitambua wanalishwa kinguvu.

vyakula vilivyojitosheleza unaweza kula bila mboga mfano wali, ndizi, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi, n.k,

hapo zamani watumwa walilishwa ugali kwa maksudi ili kuwakandamiza uwezo wa kufikiri, ni dawa iliyotumika kupunguza uwezo wa kufikiria (Thinking capacity), Mtu anaweza kuwa genius anaekula ugali lakini ilibidi awe mara 3 zaidi bila ugali.

kwa hapa nchini ukifuatilia sehem zinazotoa vichwa utagundua hawali sana ugali, lakini bado sio uwezo wao kamili kwasababu siku mbili au tatu za wiki wanakula ugali.

Mboga za majani na samaki wanaweza kuongeza akili lakini kosa linalofanywaa huwa ni kutumia ugali, nguvu ya ugali inaenda kuyeyusha / ku dilute virutubisho vya ubongo.

Ushauri wa bure kabisa, ukitaka kumuongezea mtoto uwezo wa akili usimzoeshe ugali, kiwe ni chakula cha kufanyia mazoezi ajifunze kufinya matonge ili ugenini asitie aibu.
Weka ushahidi wa kisayansi kuhusu kudumaza akili
 
Hapa mtoa mada kaongea kiushabik ila sio kisayansi.
UGALI hapa namaanisha dona na sio sembe dona ilioandaliwa vizuri ina faida mwilini kama ifuatayo.
1. Dona kwa asilimia kubwa ina wanga ambayo huupa mwili nguvu
2. Dona ina kiini tete ile ya njano ambayo inatoa mafuta na protini kwa mbali sana ambayo inasaidia mwili kupata joto na hapa ndio mwili inapopata joto hata kwenye 6 kwa 6 lazima uwe vizuri
3. Dona ina ganda la juu (pumba) ambayo husaidia katika mmeng'enyo wa chakula.
Ukiangalia hapo kwa haraka haraka unaona ukila ugali unapata virutubisho karibia vitatu.

Kitu ambacho hakipo kwenye wali au vyakula vya ngano kwani vyote hivi vina wanga tu.
Hoja ya udumavu wa akili naipinga kama ifuatavyo. Sisi wapogoro na wandamba chakula chetu kikuu ni ubwabwa tunaamini ugali ni uji ukila unakojoa saana yaani sisi asbhi tunaamka na ubwabwa mchana ubwabwa na usik lakini ndio akili yetu ikiwaza zaidi ni kwenda kwenye kigodoro.
Sasa wewe mleta mada tuletee rejea ya watu wanaokula ugali kuwa na udumavu wa akili na wale ambao hawali ugali kuwa vipanga

Ila kati ya vitu nnavyoweza kukubali ni kuwa wanaokula ndizi na viazi mviringo na samaki kwa wingi atleast wanakaukomavu wa akili kuliko wengi
 
Vyakula vya kurutubisha ubongo ni.

1.Ndizi
2.Samaki wa maji baridi.
3.Maziwa
4.Nyama

Kama huamini hilo chunguza jamii zote ambazo watu wao hutumia vyakula hivi kwa wingi kisha utakuja na majibu. Utagundua makabila ya Kilimanjaro
(Wachaga,Wapare,Wameru,Wamasai) hawa wengi wako smart sana upstairs. Hawa intake ya maziwa na nyama ni kubwa sana ila wana ndizi na samaki.

Kanda ya ziwa pia (Wasukuma, Wahaya, Wakerewe) humu nako vipanga ni wengi. Hawa intake ya samaki na ndizi ni kubwa sana ila pia wana nyama na maziwa.

Nyanda za juu (Wanyakyusa)
Hawa intake ya ndizi ni kubwa pamoja na nyama na mchanganyiko wa vyakula vingi asilia ndio maana wengi wana miili mikubwa na brain zipo vizuri.

NB: Nimesema samaki wa maji baridi sababu hata Tanga kuna samaki na Zanzibar ila maajabu hakuna 😂
 
Zanzibar na Pemba hawali ugali je wanatoa vichwa/Vipanga?
Ni akili iliyotumika, ni lazima Rais au makamu wa Rais atokee kisiwani, Ardhi yao haturusiwi kumiliki ila wao wanaweza kumiliki mashamba makubwa uoande wetu, Wana sifa za kupata vyeo / kazi sehemu mbili, n.k.
 
Sera ya jela ni kuwa hawawezi kukupa chochote ambacho kitakufanya wewe ujisikie raha.

Sasa ugali kama ni chakula, umefikaje kule?
 
Ulaya ndio maana unakuta mashamba ya mahindi makubwa na wanalishia mifugo tu
 
Naomba nitajie vyuo vitano ulaya na vitano america ambavyo waafrika wanakimbiza
Ninao ushahidi ila kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu sitoweza kuziweka hapa....ila ukae ukijua kitaaluma we africans tupo vizuri mno kuliko race nyingi tu!
 
Hizo kauli zako zenye kuudharau ugali,ungezisema ukiwa hadharani huku kwetu Zambia ungepigwa na raia kama wanavyompiga mwizi wa simu,ugali huku ni chakula cha heshima sana.
 
Weka ushahidi wa kisayansi kuhusu kudumaza akili
Soma Pia:

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akil


Je, JamiiCheck ni wababaishaji?

This myth has been debunked, verified not to be true kwamba Ugali unadumaza akili

Leo imekuwaje wameachia nyuzi hii ambayo wao wenyewe wamjiridhia kwamba sio Kweli?

Kulikoni huko JamiiCheck JamiiForums ?

Ilipaswa Moderators wauzuie huu uzi.

Huu Uzi Unahatarisha Usalama wa Afya za Watanzania, Huu uzi unalenga kuwadhihaki Watanzania.

Maxence Melo Hawa magaidi ya mitandaoni yadhibitiwe. Unaona hii Imekaaje Mkuu?
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Siupendi ugali kwa nguvu zangu zote.

Hauna ladha yoyote ile.

Na uzuri wa kujitegemea ni kwamba unafanya mambo mengi vile unavyotaka wewe.

Kwangu sipiki ugali. Nakula ninachotaka mimi kwa pesa zangu mwenyewe.
 
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

👇🏿

@JamiiCheck
Hivyo, @JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.

Watanzania, muwaogopeni hawa wakina Uncle bright na magaidi wengine wa mtandaoni, they're bigoted racists twats.

While "it is your right to have your own Opinion, You have no rights to your own facts"

Mjitathmini.

cc Wizara ya Afya
 
Back
Top Bottom