Ulawiti watoto: Ipo shida kubwa kwenye Taasisi ya Kanisa Katoliki

Kwani ni nani hasa anaezuia mapadri kuoa au mkristu kuoa wake zaidi ya 1?

Kama leo papa akasema ni ruhusa mapadri kuoa na wakristu wote wanaweza kuoa mke zaidi ya mmoja... ndo tayari mambo yote yataendelea!!?
 
Kwani hayo yako katoliki tu, jiulize kwa nini wengine hawasemwi
Ni kweli kabisa. Hayo yanatokea katika kila sehemu ya kuabudu kutoka na usiri na ushawishi walionao wakuu wa makanisa. Lakini ndani ya kanisa catholic ndio kalikuwa kamchezo. Halafu kukawa na siri kubwa ingawa wahalifu walifahamika. Watuhumiwa walikuwa wanahamishwa kwenda sehemu nyingine pale wanapotuhumiwa kuwapakata vijana wadogo.
 
Na kwenye dini nyingine walikuwa wanafanyaje
 
Mbona padri kimario aliwekwa hadharani?
Wewe unaamini katika mapadre wote wa kanisa katoliki hapa Tz ni huyo mmoja tu. Je kesi yake iliendaje? Kanisa katoliki hasa Marekani na Ulaya liliamua kukabiliana na tuhuma hizi za ulawiti baada ya kubanwa na vyombo vya habari, Sheria na madai ya malipo ya fidia yalikuwa mengi sana hata kuhatarishi kufilisika kwa Kanisa nchini Marekani (Boston USA). Katika madhehebu yote - kanisa katoliki hasa uko Majuu limeamua kushughulikia na kujisafisha. Shida ni huku kwetu- Kanisa Katoliki linapuzia na waumini wengine ambao wanatakiwa kuwa makini na kuwa mashahidi wa vitendo hivyo nao vile vile hawataki kuamini.
 
Many are deceived, very sad!..
 
Mara ngapi tumesikia maustadhi, wachungaji na viongozi wengine katika jamii wakifanya vitendo vya kulawiti na kubaka hoja Yako Ina chuki ndani yake juu ya kanisa katoliki, ulawiti na ubakaji ni janga la Dunia nzima kila mmoja Kwa nafasi yake asimame kulipinga hadharani na kulilaani
 
Kesi ya padri kimario ilienda vizuri hadi akafungwa, sema alikuja kutoroshwa jela akapelekwa msumbiji hadi mauti yalipomkutu, kuhusu mapadri wa huku kwetu sina ushahidi kama bado wanalawiti watoto maana sasahivi wameachiwa mno kupiga mademu hadi inafikia hatua tunanyang'anyana mademu kitaa
 
Sio kuishia kulipinga na kulaani tu bali na kuchukua hatua kwa kuondoa mazingira yenye kupelekea kuweza kufanyika hivyo vitendo ili tuweze kuvipunguza katika jamii.
 
Sio kuishia kulipinga na kulaani tu bali na kuchukua hatua kwa kuondoa mazingira yenye kupelekea kuweza kufanyika hivyo vitendo ili tuweze kuvipunguza katika jamii.
Hiyo ni nature huwezi kuiondoa watu wameoa lakini Bado wanafanya hivyo vitendo
 
Hiyo ni nature huwezi kuiondoa watu wameoa lakini Bado wanafanya hivyo vitendo
Huwezi kuacha kufunga milango ya nyumba yako halafu useme et wengine walifunga milango ila wezi walivunja na kuiba, kwahiyo kama kweli hatuvipendi hivi vitendo kwenye jamii basi lazima tuondoe mazingira rafiki ya kuwezesha kufanyika hivyo vitendo kadri tuwezavyo ili vipungue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…