Ulaya yakataa kununua gesi ya Urusi kwa sarafu ya taifa hilo

Ulaya yakataa kununua gesi ya Urusi kwa sarafu ya taifa hilo

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepuuzilia mbali takwa la rais wa Urusi, Vladimir Putin la kuyataka mataifa ya Ulaya kununua gesi kwa sarafu ya Kirusi, huku akimshutumu rais huyo kuwa mwenye nia ya kutaka kuvikwepa vikwazo alivyowekewa kutokana na uvamizi wake wa Ukraine.

Macron aliwaambia waandishi wa habari baada ya Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Ulaya wa mjini Brussels kwamba hatua ya Urusi haipo katika makubaliano na haoni sababu ya kutekelezwa kwa jambo hilo. Rais Putin alitoa takwa hilo juma hili katikia kipindi hiki ambacho serikali yake inakabiliwa na vikwazo vikali vinavyoathiri uchumi wa taifa hilo, kutokana na hatua yake ya kuingia kijeshi nchini Ukraine.
View attachment 2164574
Source: DW
Sawa,kama hataki awaache watu.wake wagande kwa baridi
 
Umenena vyema, russia kutaka malipo yawe kwa ruble maana yake anataka aipe thamani pesa yake ktk uchumi ambae anaona mbele utamsumbua zaidi na sio kwamba anaikomoa NATO.

Mambo yakienda hivi, uchumi wa NATO na Russia utatetereka mno apo mbeleni, sijui kwanini Africa hasa TZ tusitazame hizi fursa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania hii chini ya ccm na waziri wa fedha na uchumi bwana lameck madelu ? Au unazungumzia Tanzania diaspora
 
Soma vizuri Macron amempuuza, Marekani jana rasmi ametangaza kuziba hilo gape kwa aliyekuwa anamtegemea Putin na gesi yake, mzigo utatoka marekani, ni vile Putini amepigwa katafunua kwenye hii biashara ya gesi kwa nchi za ulaya
Gas inayopelekwa na meli na gas inayopelekwa kwa njia ya pipeline bei ni tofauti ndugu........

Kwa meli gharama ni kubwa, time inapotea pia, risk nyingi, na marekani anatumia hilo gap kuwashika korodani Nato na ulaya yao.......ndio maana mjerumani kaona mbali kasema hawezi kuacha kutumia gas from Russia.....
 
Marekani ana take advantage ya kuuza gesi kwa wahisani wake wa ulaya badala ya urusi., watu wako vizuri kwenye vichwa vyao Putini hatakuwa na soko tena kwa ulaya labda India na china, ulaya pekee urusi alikuwa anapata 47% sasa ni 0%., tafakari anayeumia ni nani?
Gas saiv huko ulaya imepanda mpaka $3800 per cubic meter......sasa jiulize mmarekani akiifikisha itakua bei gani......? Putin hategemei gas pekee, bado anauza technology sana hasa kwa mifumo ya ulinzi aridhini na angani......na wateja wake wakubwa ndio hao hao ulaya tutaona kama wataacha kununua system hata zikipanda bei.
 
Rais Biden wa Marekani anajadiliana na kufikia makubaliano namna USA itavyowapelekea Ulaya cubic meters 15 bil za gesi asilia kufidia pengo lililojitokeza baada ya kuiwekea vikwazo Russia.

Source: BBC
Saiv cubic meter 1 ya natural gas ni $3,800 haya assume mmarekani mpaka afikishe hapo itauzwa kwa $4000 then zidisha kwa hizo cubic meter 15 billion then utajua nani ataumia maana kutakua na mfumuko wa bei ambao haujawahi kutokea in history......
 
Gas saiv huko ulaya imepanda mpaka $3800 per cubic meter......sasa jiulize mmarekani akiifikisha itakua bei gani......? Putin hategemei gas pekee, bado anauza technology sana hasa kwa mifumo ya ulinzi aridhini na angani......na wateja wake wakubwa ndio hao hao ulaya tutaona kama wataacha kununua system hata zikipanda bei.
ulaya wameachana na urusi kwa kila kitu hakuna mtu atakayelipa rubble ya urusi kushusha dola, watu wako makini na kazi zao
 
Gas inayopelekwa na meli na gas inayopelekwa kwa njia ya pipeline bei ni tofauti ndugu........

Kwa meli gharama ni kubwa, time inapotea pia, risk nyingi, na marekani anatumia hilo gap kuwashika korodani Nato na ulaya yao.......ndio maana mjerumani kaona mbali kasema hawezi kuacha kutumia gas from Russia.....
Mjerumani hajawi kusema hawezi kuacha kutumia gas from Russia...., mradi wa Nord Stream 2 tayari wameunyima leseni hauendelei tena tokea Russia avamie Ukraine lakini soko lao la gesi sasa watanunua kutoka world market apart from America ambao jana pia wametangaza kuziba hilo gap kwa nchi za ulaya
 
Back
Top Bottom