Nilidanganywa nisipo oga usiku shetani ana pembe kichwani na ulimi wa moto atakuja kunilamba mwili mzima asubuhi nitaamka msafi kwa kulambwa huko.
Kumbe uongo uchafu unaishia kwenye shuka nilikuwa siachi kuoga usiku hata iwe vipi [emoji28][emoji28][emoji28]
Niliambiwa nisipopiga mswaki mara tatu chakula kinachotakiwa kutoka kama kinyesi kinarudi mdomoni ndio nitanuka mdomo kama kinyesi hadi leo nashindwa kuacha kupiga mswaki mara mbili
Ya mwisho kali ni kuwa baba na
Mama wanalala chumbani peke yao na wanajifingia mlango kwa sababu wanakazi ya kuhesabu pesa nyingi sana ili majambazi wasiwaone. Kumbe wana kazi ya kuongeza familia [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]