Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimejikuta nacheka mwenyewe maana hii mbinu naitumia kila wkt kumtoroka mwanangu
Enzi za kuzungusha antena ndio ilikuwa mbinu yangu kuu ya kumtoroka binti yangu mpendwa, Mungu ni mwema yuko darasa la tatu sasa.
 
Nikimuona kinyonga nijitemee mate kwenye Nguo ili asichukue rangi ya nguo
 
niliambiwa na jirani ukimaliza kukojoa tema mate usipotema mama yako anavimba matiti... Mapaka Leo hii Nina miaka 20+ natema mate
 
Nilikuwa mkorofi flani na sili mpaka iwepo soda,

Siku.hiyo sijui ilikuwa haipo au waliamua tu kunikomesha maana niliekewa chakula bila soda ..kuona vile nikakataa kula mama akatoka sebleni na kwenda ndani...aliporudi kaja na chupa ya coca cola nikachukua na kuendelea kula lkn kila nilivyokuwa nakunywa nilikuwa nahisi kama haiko vile nilivyoizoea ila nikakomaa nayo mpaka mwisho.

Miaka zaidi ya 20 baadae ndipo marehemu mama yangu akaniambia kuwa ile haikuwa soda ila aliweka chai ya rangi kwenye chupa ya coca cola mradi tu nile!

Ndio hapo nikajua kuwa hakuna anaweza kunipenda zaidi ya mama aliyenizaa!

Sitasahau...nilimtizama kama ni mpya kwangu siku ile!
 
Eti ukinywa maji ya mchele au kukojea juu ya kichuguu ni dawa ya kuacha kukojoa kitandani,
 
Mvua ikiwa inanyesha na jua linawaka basi fisi anazaa.

Ukikosea, kunja kidole cha mwisho then mzazi atasahau.

Ukila ukavimbiwa unaambiwa uzunguke ghala mara 10 huku ukilipuliza ili chakula kirudi ghalani na kuvimbiwa kunaisha.
 
Nilidanganya mjini kuna gari kubwaaaaaaaa ndefu kutoka mwanza mpaka daisalamu (train)
 
Ukichonga penseli pande zote mbili unawatukana wazazi..
 
Nakumbuka enzi hizo tunaenda kutafuta kuni mstuni kulikuwa na matunda pori matamu kweli ,ila unaambiwa ukiyala ndani ya msitu simba lazima wakufanye chakula "unaliwa na simba " so ilikuwa lazima mtafute kuni kwanza alafu mnakula mkimaliza nje ya forest . .....

Kumbe nadharia ilikuwa simple [emoji23][emoji23] kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kushindwa kufanya kilichowapeleka msituni mkaishia kula hayo matunda ....

 
Mama alikuwa akimpata mdogo wangu alikuwa ananidanganya kuwa ameenda kumnunua sokoni!.....Hadi nafika la saba nilikuwa nafikiri kuwa watoto huwa wananunuliwa sokoni!!
Hahahahahahaaaa.

Ingekuwa raha sana kuchagua wenye[emoji196] [emoji196] [emoji196] [emoji196]
 
Nilikuwa naambiwa nikutengenezee njia inayoenda kwa bibi yangu ili nije nipite wakati wa kwenda kumsalimia, hapo nafurahi kweli kweli huku muhindi analiwa tu
 
Mama alikuwa akimpata mdogo wangu alikuwa ananidanganya kuwa ameenda kumnunua sokoni!.....Hadi nafika la saba nilikuwa nafikiri kuwa watoto huwa wananunuliwa sokoni!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nadhani hii 900 ilimpendeza mama hadi kakununua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…