Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Tatizo mnaanza na biashara badala ya kuanza kutoa shukrani kwa Mungu.

Fanyeni mambo ya kumpendeza Mungu kwanza... Anza na Philanthropy kama biashara ambayo haiingizi faida ambayo itakufungamanisha na Mungu..

Halafu baada ya hapo ndo ufungue biashara sasa sambamba na hiyo Philanthropy.
 
Nimechoma hela kwenye biashara

1.Mtumba
2.pembe Za ng’ombe
3.Kilimo
4.forex
5.Chakula
6.Samaki&Kuku

Mpaka nimekuja kusettle kwenye cosmetics na hapa nimesettle in a very hard way.. Yaani nilichojifunza
Kwenye biashara kuna muda inabidi ujitahidi kuforce sana mambo na kusimamia biashara mwenyewe

Usiachie mtu biashara yako.
Usiweke mtaji wote kabla haujausoma mchezo.
Kubali kuwa mjinga jifunze kwa watangulizi.
Kuwa na nidhamu ya Pesa.

Kupitia haya angalau biashara inaweza kusimama na kukua.
Samaki zilikuangusha vp mkuu? Ndio nimeanza kufanya now.
 
Fanyeni mambo ya kumpendeza Mungu kwanza... Anza na Philanthropy kama biashara ambayo haiingizi faida ambayo itakufungamanisha na Mungu..
Mkuu comment yako imegraduate. Inavigezo vyote vya kuwa uzi. Tafadhali unaweza okoa kizazi kwa kiextend comments hii na kuwa uzi uliokamilika
 
Mtu akikuona leo hii unavyokula bata, maisha mazuri, usafiri mkali na biashara kubwa mjini, anaweza kudhani umefika hapo ulipo kirahisi rahisi tuu. Mimi mwenyewe nilikua nadhani hivyo!

Cha ajabu ni kwamba kila ninapojaribu kutia mguu kwenye biashara nachezea za uso mbaya kabisa najikuta natoka kapa. Mpaka muda huu nimeshajaribu zaidi ya aina 5 tofauti za biashara kuanzia bar, stationary, usafirishaji, kilimo, ufugaji nk na zote hakuna hata moja iliyofanikiwa walau hata kurudisha mtaji!

Nimebaki najiuliza nyie wenzetu mliofanikiwa kutoboa kibiashara je na nyie mwanzo mlichoma mitaji kama sisi? Hebu tupeni akili na sisi tutoboe.

NB: Usije na hoja za "fanya kazi kwa bidii".
Hadi ufugaji umeshindwa basi chimba kaburi jizike ukawe mfanya biashara kuzimu huenda fungu lako halipo hapa duniani
 
WhatsApp channel
 
Attachments

  • 20231102_082837.jpg
    20231102_082837.jpg
    116.8 KB · Views: 19
Kwenye biashara kuna muda inabidi ujitahidi kuforce sana mambo na kusimamia biashara mwenyewe

Usiachie mtu biashara yako.
Usiweke mtaji wote kabla haujausoma mchezo.
Kubali kuwa mjinga jifunze kwa watangulizi.
Kuwa na nidhamu ya Pesa.

Kupitia haya angalau biashara inaweza kusimama na kukua.
Asante Hornet.. Hapo kwenye kutokumuachia mtu biashara napo ni pagumu sana hasa kama mtu una shughuli zingine au umeajiriwa ni lazima utajikuta mda mwingi haupo. Tatizo pia naona kupata kijana muaminifu na anaeelewa anachokifanya ni shida sana.
 
Back
Top Bottom