Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Comment nzur Sana[emoji4][emoji106]
 
Kichawapoteza wengi kibiashara,

Ni kuanza biashara ukiwa na matarajio makubwa mno kuliko uhalisia.

Mfano Ni wale wanaofungua maduka ya dawa kwa kuangalia faida ya kila dawa bila kuzingatia gharama halisi za uendeshaji wa biashara ya Duka la dawa.
 
Aisee nimejifunza kitu hapa..
 
Nimeifanya hii pia. Nakuelewa sana.. Tena mimi nilikua nawafuga mwenyewe.
 
nakumbuka niliweka hapa bandiko la mashine gani nzuri ya kuchana mbao wadau wakashauri nichukue husqvana... acha kbs kazi yoyote ya kuambiwa usiende kichwa kichwa kama hujawahi kuifanya ndio kilichonitokea mim
Pole mkuu ,kwa hiyo ilichezea mbata ,mitama, mateke na chembe kidevu za kutosha au sio ? [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Tenaa umenikumbusha aisee hii biashara nilipigwa "double impact" matata sanaa😄😄

Mimi nilitafuta eneo nje ya mji nikajenga mabanda, nikaweka vifaranga vya kitimoto nilianza na kama 20. Nikaweka mtu wa kuwasimamia, kuwalisha nk.. Walipoanza kukua nikatafuta eneo mjini nikaweka jiko, nikatafuta kijana wa kukaanga na kuchoma kitimoto. So nikawa naenda mwenyewe shamba, nachinja, naleta mjini nakaanga nauza! Waliongezeka hadi wakawa 100 na kitu.

Kwa kifupi nilikuja kupigwa na kitu kizito na jamaa wote wawili.. wa shamba aliekua anasimamia, na wa mjini aliekua anachoma! Nilichezea za uso nikatoka niko hoi bin taabani mpaka leo sina hamu😀😀😀
 
Pole mkuu ,unaweza share jinsi walivyokufirisi ?
Itakuwa msaada kwa wengine
 
Pole mkuu ,kwa hiyo ilichezea mbata ,mitama, mateke na chembe kidevu za kutosha au sio ? [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
unawaza kuendelea roho inagoma yan huwezi tena mlima ni mrefu ulipigiwa mahesabu hewa, lkn pia unawaza kuacha ukimbie roho pia inagoma maana umeshakula hasara ya pesa karibia 3/4 ya pesa yako unaamua ukomae kumbe ndio unaendelea kuteketeza zaidi.... Mwisho wa siku unaamua kukimbia tu ila tayari umeshachelewa hela imeenda yote.
 
chief, gas buku?
vibarua unawalipaje, na wanakula wapi?
transport cost ya kuchukua mzigo sokoni?

ushuru wa usafi halmashauri ?

bado cost za flemu.

ndio maana kiuchumi wanasema every one can invest , but not every one can do business.

lazima uwe na passion,capital,experience na Network kubwa ndipo unaweza penya kirahis kwenye biashara
 
Kodi, usafi, ushuru, flemu unalipa kila siku?

Transport cost hujaiona kwenye misc.?

Hujaona nimemtajia est. profit kabla hajalipa vibarua.

Unahisi kwanini nimepigia hesabu kilo moja tu na kwa wateja watano, kwani atapika kilo moja kwa vibarua wote wanne. Na kwanini nimepigia kwenye gross profit sio net profit.

Biashara inabidi iwe liquid, iwe na running capital. Nimepiga hesabu ya kurejesha running capital, sio kupata faida kwenye running capital na wala sijagusa fixed expenses.

Mtu anashindwa kutumia 200,000 ya kila siku ya kununua nyanya na mchele akiuza anapata 150,000 uanze na kumwambia kodi na ushuru. Anza na kuitoa hiyo 150,000 iwe 200,000 iliyoingia. Then ulipe wafanyakazi upate faida, then twende kwenye hizo kodi na ushuru. Mtu kujumlisha hajui unamwambia habari za kuzidisha.
 
Nina ndugu yangu analipa madeni (uzuri ni mfanyakazi wa serikali) sababu ya Hii biashara ya madini

Bahati mbaya yeye aliingizia na ushirikina, mganga akalamba hela na shimo likalamba pesa

Siyo mchezo..

Pole sana utainuka tu pambana.
Hawa waganga mnao walaumu huwa wanachukuwa Kia's gani Cha pesa mban Mara nyingi Sana mganga anachukuwa kambuzi na jogoo saanaaa na laki tano hv ,Sasa Ni Kia's gani mnawapa mganga je Ni milion 2 ,3,5
 
Hawa waganga mnao walaumu huwa wanachukuwa Kia's gani Cha pesa mban Mara nyingi Sana mganga anachukuwa kambuzi na jogoo saanaaa na laki tano hv ,Sasa Ni Kia's gani mnawapa mganga je Ni milion 2 ,3,5

Waza nje ya Box chief

Shida siyo pesa unayompa mganga

Shida ni pesa unayopoteza kwa matumaini aliyopewa na mganga

Na hamna mahali mganga amelaumiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…