Biashara maumivu sana sana sana.
Nakumbuka mwaka 2018, nilipata hasara 1.4M katika kilimo fulani .mwaka 2019 nkafanikiwa kutengeneza 10M+ Kweny biashara (sio kilimo) ,mwaka 2020 nilipata hasara 35M+ (kutoka kwenye biashara,kilimo na kutapeliwa MPK NKARUDI HOME KUANZA MAISHA UPYA , mwaka 2021 nkafeli zaid katika kila jambo la kiuchumi niliofanya MPK nikawa naogopa kujaribu kufanya jambo lolote.
Ila mwaka 2022 Mungu akanikumbuka,NKARUDI katika form MPK sasa.
NB: 1) kama unahela na unataka ufanye biashara hakikisha unawekeza 25% pekee ya hela yako.na usiongezeee hata sh.kumi MPK ikue yenyewe iwe hata mara 3 ya mtaji ulioanza nao.
2) Epuka kuanza biashara kwa hela ya kukopa,biashara anza kwa hela yako. Na ikikua na kuwa na uhakika wa mapato,ndio unaweza kukopa ili kubust mtaji ikue kwa haraka( leverage).
3) Usichanganye Urafiki,undugu,ushukaji ,ujuaji(egoism) na malengo ya biashara yako
4)Usiitegemee faida au hela itakayopatikana Kweny biashara ikulishe,ikulipie kodi au ikusaidie kwa lolote ndan ya miezi 6 ya mwanzo wa biashara yako.
Binafsi haya ndio machache kati ya mengi niliyoyaona,yenye uwezo mkubwa kukirudisha nyuma sana hata kama ulishatoboa kimaisha.