Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Hii issue inaweza kukuuguza presha usipokuwa bandidu, umetoa 200K kila kitu kimeisha ila mauzo ni 150K, hapo umezamisha 50K na bado una wafanyakazi wamekusimamia uwape chao. Kesho utaanza biashara kwa manunuzi ya 120K (baada ya kulipa wafanyakazi) ama utaongezea 80K ili ufanye manunuzi ya 200K kama kawaida.? Vipi hiyo hali ikiiendelea kwa mwezi mzima.?[emoji1]

Kichwa lazima kiwake moto.


Makosa makubwa ya hii issue ni kuuza bei za kisadakasadaka ili kufurahisha wateja, kuruhusu wafanyakazi ndio wawe wanaojua oder ngapi zimetoka na zimeenda wapi halafu wewe usubiri tu kuletewa hela mezani (watauza oder 10 utaletewa pesa ya oder 7 kisha baadae watakudai ujira wao tena).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nakuunga mkono
Kuna kipindi nilikua Moro, nikafungua kibanda cha chips,niliuza kama siku tano ,maamaaee kilichofuata ,wateja wanapita mbele ya kabati wanaacha viazi wanaenda kupanga foleni Kwa majirani huko,
Asubuhi kila nikienda madukani pale Morogoro mjini kununua vitu ,kila duka unaloingia wanachoma udi mpaka unajiuliza kama wanapunga mashetani
Nikahamisha mavitu yangu mchana kweupe nikaacha Banda
Kwa wenyeji wa Morogoro,wanapafahamu maeneo ya IPOIPO ukiwa unaelekea Sua, mazimbu campus
 
Kaka IPOIPO mbona ni location nzuri Sana pale . Huwa natamani Sana nipate frame maeneo Yale . Ila pole kwa changamoto
 
Hongera sana mkuu,nimeipenda kauli mbiu yako kwamba lazima uyarudie madini yakupe ela yaani wewe tayari ni miner na dhahabu Iko damuni kbsa
 
Hapo ndipo biashara inapokuwa ngumu, yani maokoto ninayo halafu nisimtamani demu? 😀
 
Forex ulifanya kwa muda gani?
 
Kitendo tu cha kujaribu jaribu biashara kadhaa kinaonesha huna uvumilivu na husomi ethics za biashara husika !
Ipo hivi chagua biashara unayoipenda kutoka moyoni, halafu wekeza muda nguvu na akili yako hapo , biashara ikifeli rudia tena biashara hiyo hiyo huku ukuangalia maeneo Uliyofeli mwanzo na weka mbinu mpya kwa biashara hiyo!
Kubadili biashara hakutakusaidia kitu maana kila siku utakuwa unakumbana na changamoto mpya kwenye kila biashara mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…