Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Mkuu hatukimbii kwa kupenda, unalazimika kutoka nduki! We imagine mimi kuna wakati nilikua na mgahawa, asubuhi mnanunua kila kitu kwa 200,000 ikifika jioni kufunga mahesabu unakuta kila kitu kimeisha na mmepata 150,000. Hapo una vijana kama wanne wanasubiria ujira na kesho kunatakiwa hela ya sokoni kufuata mahitaji! Kwanini usivizie watu wakiondoka unakunja majiko yako unatia mfukoni na kutoka nduki kali...???[emoji1][emoji1]
Hii issue inaweza kukuuguza presha usipokuwa bandidu, umetoa 200K kila kitu kimeisha ila mauzo ni 150K, hapo umezamisha 50K na bado una wafanyakazi wamekusimamia uwape chao. Kesho utaanza biashara kwa manunuzi ya 120K (baada ya kulipa wafanyakazi) ama utaongezea 80K ili ufanye manunuzi ya 200K kama kawaida.? Vipi hiyo hali ikiiendelea kwa mwezi mzima.?[emoji1]

Kichwa lazima kiwake moto.


Makosa makubwa ya hii issue ni kuuza bei za kisadakasadaka ili kufurahisha wateja, kuruhusu wafanyakazi ndio wawe wanaojua oder ngapi zimetoka na zimeenda wapi halafu wewe usubiri tu kuletewa hela mezani (watauza oder 10 utaletewa pesa ya oder 7 kisha baadae watakudai ujira wao tena).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo haukushirikisha wazee wa kimila kwenye biashara machuma ulete niyakufikia, kuna kutupiana majini mazongo na kuna kutupiana mikosi salala, unafungua duka unaona wenzio wanasonga wewe hamna, wateja wanakupita wengine unawafuata kwa nguvu hamna hawaji kwako

Nenda stand saa kumi usiku stand nzima inanuka udi
Hii nakuunga mkono
Kuna kipindi nilikua Moro, nikafungua kibanda cha chips,niliuza kama siku tano ,maamaaee kilichofuata ,wateja wanapita mbele ya kabati wanaacha viazi wanaenda kupanga foleni Kwa majirani huko,
Asubuhi kila nikienda madukani pale Morogoro mjini kununua vitu ,kila duka unaloingia wanachoma udi mpaka unajiuliza kama wanapunga mashetani
Nikahamisha mavitu yangu mchana kweupe nikaacha Banda
Kwa wenyeji wa Morogoro,wanapafahamu maeneo ya IPOIPO ukiwa unaelekea Sua, mazimbu campus
 
Hii nakuunga mkono
Kuna kipindi nilikua Moro, nikafungua kibanda cha chips,niliuza kama siku tano ,maamaaee kilichofuata ,wateja wanapita mbele ya kabati wanaacha viazi wanaenda kupanga foleni Kwa majirani huko,
Asubuhi kila nikienda madukani pale Morogoro mjini kununua vitu ,kila duka unaloingia wanachoma udi mpaka unajiuliza kama wanapunga mashetani
Nikahamisha mavitu yangu mchana kweupe nikaacha Banda
Kwa wenyeji wa Morogoro,wanapafahamu maeneo ya IPOIPO ukiwa unaelekea Sua, mazimbu campus
Kaka IPOIPO mbona ni location nzuri Sana pale . Huwa natamani Sana nipate frame maeneo Yale . Ila pole kwa changamoto
 
Acha kabisa mkuu. Nimechoma milioni 80 kwenye dhahabu. Imeniacha mbendembende. Daah...! Bahati mbaya napoteza hela na umri ndio umeenda 40+.

Nimegundua ndio maana wakinga wakishika biashara moja ya duka ni hiyo hiyo hawabadiriki.

Hivi najitafuta kwa upya. Duka nililipukutisha kuingiza kwenye dhahabu. Hivi ndio napambania kulirudishia. Bidhaa sina japo biashara ipo. Hapa ili nirudi sawa natakiwa angalau milioni 40 kwa uchache 20 mpya niitupie humo.

Ila unajua nini? Lazima niyarudie madini yanipe hela.
Hongera sana mkuu,nimeipenda kauli mbiu yako kwamba lazima uyarudie madini yakupe ela yaani wewe tayari ni miner na dhahabu Iko damuni kbsa
 
Bro naona wengi wameshauri mambo mazuri tu kama location, juhudi, kufanya utafiti wa biashara unayotaka kufanya, na pia nidhamu ya pesa, inabidi uwe mbahili, narudia tena mbahili kama unaanza.

Kubusu ulimwengu wa roho the choice is yours ila upande wa Mungu, inahitaji usali sana na utoe asilimia kumi za mtaji alafu ukisali kwa Imani then ukipata faida utoe tena 10% ya ile kwa Mungu, 90% ya kwako alafu utakuja kuniambia.

Sali Baba yetu wa Mbinguni kwa Mkristo then omba kwa nia njema, ila sasa usifanye uovu, hata demu usimtamani.
Hapo ndipo biashara inapokuwa ngumu, yani maokoto ninayo halafu nisimtamani demu? 😀
 
Nimechoma hela kwenye biashara

1.Mtumba
2.pembe Za ng’ombe
3.Kilimo
4.forex
5.Chakula
6.Samaki&Kuku


Mpaka nimekuja kusettle kwenye cosmetics na hapa nimesettle in a very hard way.. Yaani nilichojifunza
Kwenye biashara kuna muda inabidi ujitahidi kuforce sana mambo na kusimamia biashara mwenyewe

Usiachie mtu biashara yako.
Usiweke mtaji wote kabla haujausoma mchezo.
Kubali kuwa mjinga jifunze kwa watangulizi.
Kuwa na nidhamu ya Pesa.

Kupitia haya angalau biashara inaweza kusimama na kukua.
Forex ulifanya kwa muda gani?
 
Mtu akikuona leo hii unavyokula bata, maisha mazuri, usafiri mkali na biashara kubwa mjini, anaweza kudhani umefika hapo ulipo kirahisi rahisi tuu. Mimi mwenyewe nilikua nadhani hivyo!

Cha ajabu ni kwamba kila ninapojaribu kutia mguu kwenye biashara nachezea za uso mbaya kabisa najikuta natoka kapa. Mpaka muda huu nimeshajaribu zaidi ya aina 5 tofauti za biashara kuanzia bar, stationary, usafirishaji, kilimo, ufugaji nk na zote hakuna hata moja iliyofanikiwa walau hata kurudisha mtaji!

Nimebaki najiuliza nyie wenzetu mliofanikiwa kutoboa kibiashara je na nyie mwanzo mlichoma mitaji kama sisi? Hebu tupeni akili na sisi tutoboe.

NB: Usije na hoja za "fanya kazi kwa bidii".
Kitendo tu cha kujaribu jaribu biashara kadhaa kinaonesha huna uvumilivu na husomi ethics za biashara husika !
Ipo hivi chagua biashara unayoipenda kutoka moyoni, halafu wekeza muda nguvu na akili yako hapo , biashara ikifeli rudia tena biashara hiyo hiyo huku ukuangalia maeneo Uliyofeli mwanzo na weka mbinu mpya kwa biashara hiyo!
Kubadili biashara hakutakusaidia kitu maana kila siku utakuwa unakumbana na changamoto mpya kwenye kila biashara mpya
 
Back
Top Bottom