Ulichokisema ni kweli mkuu,mimi nimefanya biashara ya migahawa kwa muda mrefu kiasi na biashara ya chakula ndio biashara yangu kuu. Kwa uzoefu wangu wa biashara ya chakula hasara inasababishwa sana na vijana wa kazi kwanza wahudumu,wapishi na wateja pia. Wahudumu ndio wezi namba moja watauza oda 10 na kuleta hela ya oda 5,wataiba hela kama hela iwapo unawapa access ya kufikia droo la hela,wanabana chenji mfano anaenda kununua chumvi ya 1000 anachukua 5000 na chenji hairudi.
Wapishi hawa wanaiba materials kama sukari,mafuta,unga,maandazi nk. Wapishi wanahonga chakula kwa mademu zao au kama wanamahusiano ya kimapenzi na wahudumu(hii ilinitokea mpsihi anatembea na mhudumu kwahiyo mhudumu hali chakula cha ofisi siku ya wali maharage mpishi anatengenezea chipsi yao nzito).
Kuna wateja wezi wanakula nakuteleza,wateja wanaiba chill na tomato sauce,wateja wanaiba chakula kama mishikaki,wateja wanaiba stick,wateja wanaiba vijiko,sahani nk