Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Biashara ya kununua mazao ya chakula ya msimu na kuuza. Ile ambayo kuna jamaa kakushawishi uanze sijui uende Mtwara sijui wapi Kusini uko.

Ile biashara inataka uwe na elimu kubwa na uzoefu wa mazingira na mazao husika. Ukiwa nje unaona ni mahindi tu, ukiingia field unakutana na mahindi yana namba sijui H30 na ngapi, mara punje ina pumba nyingi mara inatoa kiini kikubwa mara imepinda katikati hivyo gunia halina uzito sana.
Hujaja kwenye mpunga uko utakutana na mbegu zaidi ya nane na huwezi zijua kichwakichwa.

In short tuseme ni biashara ambayo unatakiwa uwe mtu wa kijijini kukekule, sio umetoka Kigamboni wajomba zako wanauza CD na mitumba eti unakurupuka kuuza mpunga. Utaijulia wapi kalima wangu, Zambia, salo, mbawa mbili na India?
Mpaka unakuja kujua mchezo umechoma mtaji tiyari. Ukija kuujua serikali inazuia mazao kuuzwa nje, msimu unaofuata serikali inanunua michele kutoka Pakistan bei inashuka sokoni.

Nilikaa hata msimu haukuisha nikala kona. Kila niliyekutana naye kachoka. Wenye faida ni wanaonunua na kuweka store. Sasa wewe na 10M yako ukiiweka store then ukafanye nini. Nikatimua mbio
Umeandika fasta fasta mnoo. Lakini unaonekana unapenda faida ionekane biashara inapoanza. Hapa lazima ulie sana, utalia mbaka ubadilike mwnyw
 
Mtu akikuona leo hii unavyokula bata, maisha mazuri, usafiri mkali na biashara kubwa mjini, anaweza kudhani umefika hapo ulipo kirahisi rahisi tuu. Mimi mwenyewe nilikuwa nadhani hivyo!

Cha ajabu ni kwamba kila ninapojaribu kutia mguu kwenye biashara nachezea za uso mbaya kabisa najikuta natoka kapa. Mpaka muda huu nimeshajaribu zaidi ya aina 5 tofauti za biashara kuanzia bar, stationary, usafirishaji, kilimo, ufugaji nk na zote hakuna hata moja iliyofanikiwa walau hata kurudisha mtaji!

Nimebaki najiuliza nyie wenzetu mliofanikiwa kutoboa kibiashara je na nyie mwanzo mlichoma mitaji kama sisi? Hebu tupeni akili na sisi tutoboe.

NB: Usije na hoja za "fanya kazi kwa bidii".
Ungekaza hapo kwenye "transportation /logistics" na kwenye "kilimo" ndipo sehemu sahihi zaidi kwa mazingira ya Tanzania
 
Kuna biashara moja hivi tulijaribu miezi ya mwanzoni hivi, tulitengeneza Faida ya 1mil+ ndani ya wiki tatu hivi, ila nisikufiche tulitumia ujuzi wa Ulimwengu wa roho, baadaye tukaona tutumie tu akili zetu na uzoefu maana wateja si tayari wapo, alooo.......walipungua na kuzidi kupungua, hapa tumeamua kutulia tu, tunalisoma soko halafu turudi tena kwenye ulimwengu wa roho.

N:B - Ulimwengu wa roho sio kupitia Shetani tu, hata kupitia njia za Mungu inawezekana.
Na mm nipitisheni kwenye huo ulimwengu wa roho
 
Kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi nikapata kama million 8 baada ya kuchukua mafao yangu NSSF na akiba yangu nikanunua kiwanja nikajenga banda la mpira lilikuwa linaenda vizuri tu ila kutokana na majukumu nikamuachia mtu aendeshe likamshinda ikabidi nikubali matokeo nikaenda zanzibar kuchukua mzigo kama TV used fridge pasi heater nakadhalika kwasababu nilikuwa bize sana na kazi nikamwachia mtu aendeshe akaniibia nikamtimua nikafunga biashara kwa hyo ile million 8 ikapotea kwa style hyo nimeambulia kiwanja tu ila nimejifunza vitu vingi sana sasa hivi najipanga kuja kivingine nianze upya na projects mpya I hope I will succeed next time.
Hapa la kujifunza ni kusimamia biashara yako mwenyewe...biashara zako zilikuwa kwa kuamin watu na kuwaachia waendeshe...pole
 
Chukua muda kujifunza na pia uwe na uvumilivu. Biashara yoyote mpya matarajio ya kupata faida iwe baada ya miaka 2, kwa maana ya kupata muda mzuri wa kulisoma soko na kujifunza changamoto mbalimbali na namna ya kukabiliana nazo.

Ukitaka mafanikio ya haraka hamna biashara ya namna hiyo labda wizi. Lazima uanguke ili usimame imara.

Biashara umefanya kidogo huoni muelekeo unakimbilia nyingine, hayo unayokimbia unatakiwa uyakabili na ujifunze ili kuyashinda.

Kwaheri.
Waathirika wa biashara za kufanya muda mfupi na kudhani utapata faida kubwa ni Watumishi wa Serikali au Wafanyakazi wa Serikali hasa Wastaafu. Mtu hajawahi kufanya biashara akipata mafao anavamia kufanya biashara fulani au hata kilimo cha mazao fulani baada ya miaka 2 anaandika historia ya kufeli. Inatakiwa akiwa amebakiza miaka 5 kabla ya kustaafu inabidi aanze kufanya biashara au kilimo au kuuza mazao ya kilimo halafu atakuwa anajifunza pole pole maeneo anayokumbana na changamoto za shughuli husika. Akija kustaafu anakuwa tayari ana uhakika wa shughuli ya kufanya.
 
Back
Top Bottom