Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ulichokisema ni kweli mkuu,mimi nimefanya biashara ya migahawa kwa muda mrefu kiasi na biashara ya chakula ndio biashara yangu kuu. Kwa uzoefu wangu wa biashara ya chakula hasara inasababishwa sana na vijana wa kazi kwanza wahudumu,wapishi na wateja pia. Wahudumu ndio wezi namba moja watauza oda 10 na kuleta hela ya oda 5,wataiba hela kama hela iwapo unawapa access ya kufikia droo la hela,wanabana chenji mfano anaenda kununua chumvi ya 1000 anachukua 5000 na chenji hairudi.
Wapishi hawa wanaiba materials kama sukari,mafuta,unga,maandazi nk. Wapishi wanahonga chakula kwa mademu zao au kama wanamahusiano ya kimapenzi na wahudumu(hii ilinitokea mpsihi anatembea na mhudumu kwahiyo mhudumu hali chakula cha ofisi siku ya wali maharage mpishi anatengenezea chipsi yao nzito).
Kuna wateja wezi wanakula nakuteleza,wateja wanaiba chill na tomato sauce,wateja wanaiba chakula kama mishikaki,wateja wanaiba stick,wateja wanaiba vijiko,sahani nk
 
Duuuh
 
Aisee, kweli kila biashara na changamoto zake
 
Kaka naomb nije inbox unishaur mawil matatu natamn namim siku moja pia nifany hii biashara
 
Hapa nilipo tu uharo unanijaa kila mara miashara ya mazao nimelaza mill 40....bei badala ya kupanda zimeshuka.....

Na nikiulizakila sehemu mvua zinanyeesha vizuri it means mazao yakikfika level tu bei inashuka tena uhakika wa mavuno

Nikiingia store nasikia vidudu vimeanza kwenye magunia .....nabamiza mlango hasira naenda kwenye K vant

Ukicheki hii ni loss najiulizaga si bora ningejenga fremu tu 🤢🤢

Biashara ya pili ninayomiliki kosta nikiona tu simu za dereva missed call sipokei nazma cm kila siku gari loss,imeharibika,imeshikwa ipo polisi

Suruali zangu zote hazintoshi zinavuka..hadi kichwa kimepungua kapero nikipanda boda upepo kidogo inaondoka na upepo....🥺🤢🤢

Aisee stress za biashara ....ndoa ikasome

Nikipita mtaani nikiona watoto wanacheza wanafuraha naona km wananipigia kelele

Hakuna kitu kibaya km kuona unafilisika gradually ni km unakufa uku unatembea
 
Hongera mkuu, uko kwenye right track
 
Kwakweli wafanyabiashara kazi tunayo 😄😄
 
Hahahah nimecheka sana utadhani mazuri.

I feel u brother.

BIASHAra ni nyoko sana.
 
Lazima niyarudie madini yanipe hela.
Una falsafa kama yangu,kuna biashara ilinifilisi sana ila nikajua wapi nilifeli.

Najipanga upya lazima nitairudia na itanipa hela siku za mbeleni.

Nimegundua tunafeli ili tujue wapi tuzibe ili tusonge mbele.

"SEHEMU NILIYOONDOKA HUKU NALIA LAZIMA NITAIRUDIA ILI NIONDOKE HUKU NACHEKA".
 
"PESA INAWEKEZWA KWA WATU WENYE UJUZI WA JAMBO FULANI ILI IZALISHE".
 
Usikate tamaa.. jaribu kufanya tathmini wapi unapokosea halafu urudi mchezoni kivingine kabisa
 
Mimi nilifanya biashara ya kahawa (kata kichwa) Nikagawa hela kama 13ml kwa minajiri ya kulipwa kahawa kavu kipindi cha mavuno. Kipindi cha mavuno kimefika baadhi ya watu niliowakopesha walikimbia, wengine wanaleta kahawa mbichi ukianika inapungua uzito na zao la kahawa linauzwa kwa kilo lakini tulikubaliana kwa madebe. Nimekusanya zao limeshuka bei zaidi ya niliyokatia kichwa. Katika mzigo wote niliambulia ml 8 Toka 15. Nilichanganyikiwa sana aisee. Ndo maana saivi naona ni Bora kuwekeza UTT tu bas. Bora kupata kidogo chenye uhakika kuliko kingi chenye stress.
 
Mkuu
Unanafaka gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…