Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Andika business plan , alafu kopa.
Sema hakikisha unasimamia Hesabu wewe, ukiwaachia wafanyakazi utaliwa shoti, wale wasiguse pesa ndo maana wafanyakazi wengi wa serikalini biashara zinawashinda.
Mkuu unagonga kwenye mshono.. mi mwenyewe ni mfanyakazi ila napambana huko nje sema ndio nachezea za uso. Saa nyingine nadhani hata kale ka uhakika kwamba mshahara upo siwezi kufa njaa pengine kananifanya nisiwe serious saana kama inavyotakiwa..?
 
Kuna shortcuts huko na kamwe huwezi ambiwa ila kwa mtu anayekuamini sana.
 
Mara nyingi sana
 
Mimi ninachoona siyo Kila biashara inanafaa
+Nashauri biashara yako ya kwanza iendane na profession yako(una ujuzi mwingi zaidi hapa) mfano mfamasia afungue famasi etc
+Kingine it takes time aisee......inaonekana Tanzania kuchomoka ni wastani wa miaka mi tatu hivi
+Ukiweza kwepa Kodi kwepa sana ......hizi Kodi sijui malipo ya nn yanakula gharama sana
+Biashara yako iwe chini ya kampuni ...ni rahisi zaidi kudeal na kampuni kuliko jamaa wa mtaani tu.hata serikali inafanya kazi na makampuni
+Hakikisha biashara yako haiweke rehani mtaji wako(Kwa mfano kwenye kukopesha etc)
+Chagua biashara ambayo mteja analipa kwanza ndipo anapata huduma na siyo anapata huduma halafu malipo baadaye



Nawaza hivo tu....
 
Mkuu unagonga kwenye mshono.. mi mwenyewe ni mfanyakazi ila napambana huko nje sema ndio nachezea za uso. Saa nyingine nadhani hata kale ka uhakika kwamba mshahara upo siwezi kufa njaa pengine kananifanya nisiwe serious saana kama inavyotakiwa..?
Yes .
Na kwasababu hiyo kuna uwezekano Kanisa unaowaajiri wanakuibia ndo maana unaona hasara kwasababu husimamii, huna mke? Kama unaye, mfanye kama msimamizi wa mahesabu, awe anazishika yeye, utakuwa umewin . Mbinu hii wanatumia wahindi.
 

Aisee umesema ukweli mtupu.
 
Nilichoma 78 million na madeni juu zaidi ya millioni 30 dadeq mpaka Leo najikongoja biashara sio pow inabidi uwe na moyo wa ziada laa sivyo unaweza kujinyonga[emoji23]
Aisee kwakweli inataka moyo wa chuma kukabiliana na hiyo hali.
 
Achana na madini utachakaa


Hiyo milion 80 yako kama unachimba lazima uwe kichaa !


Na ubaya wa madini yanakupa bonge la hopes ila ndio unakuwa unapotea hivyo.


Kama una chimba acha huo upuuzi komaa na duka

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Kuna bro wangu mmoja nae aliwekeza kwenye bar nadhani alichoma kama 25- 30m au zaidi pale manake ali decorate sana. Siku nimekutana nae namuuliza vip bar inaendeleaje? Jamaa hakua hata na hamu ya kuliongelea hilo suala akaniambia dogo we acha tuu..!
Nilichoma 78 million na madeni juu zaidi ya millioni 30 dadeq mpaka Leo najikongoja biashara sio pow inabidi uwe na moyo wa ziada laa sivyo unaweza kujinyonga[emoji23
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…