Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Ulichoma mtaji mara ngapi mpaka kuja kutoboa kibiashara?

Watu wanauza matambara, mawe na mavi mule ila wateja kibao! Na mapesa kedekede... Ukiwa na macho ya ulimwengu mwingine ndo utayashuhudia hayo hivihivi katu huwezi gundua hilo. Na wao wenyewe wakijua wanakutoa mkuku fasta! 😅🙌🏾

There's no such a thing. Hizo ni story za kusadikika tu hazina uhalisia wowote.
 
Daaah...! Dhahabu hatari sana jamaa yangu. Hapa kichwa kimevurugika. Najikaza tu uanaume ila nina strees za kufa mtu. Nikivuka Salama mpaka mwaka 2025 nitamshukuru MUNGU sana

Chief, ulikua wapi kwenye chain ya gold industry? Broker/dealer, mchimbaji, muuza vifaa na madawa, plants au? Ulipataje hasara?
 
Halafu mara nyingi hela ikishaisha ndio hua unaanza kupata akili ya mambo ambayo kama ungeyafanya ungepiga hatua
Ndio maana nimekwambia ulikuwa unakimbia biashara mapema. Kama biashara ya kwanza imekufa na baada ya kufa ndio ukapata akili. Hata ya pili itakufa ndipo upate akili sababu huwezi pata maelezo yote ya biashara kabla hujaifanya.
Ungepata hela mara ya pili ukarudi kwenye biashara ileile uliyofeli mwanzo kama ni kweli ina faida ungepiga hatua.

Umedisco kusoma Logistics unaenda kuanza upya Marketing. Kwanini usiende kuanza upya Logistics kwingine angalau modules ushapitia na unajua ulikwama wapi.
 
Tatizo mnaanza na biashara badala ya kuanza kutoa shukrani kwa Mungu.

Fanyeni mambo ya kumpendeza Mungu kwanza... Anza na Philanthropy kama biashara ambayo haiingizi faida ambayo itakufungamanisha na Mungu..

Halafu baada ya hapo ndo ufungue biashara sasa sambamba na hiyo Philanthropy.
Philanthropy ndio uanze biashara au unasema charity. Mtu ana mtaji wa milioni tano za kupiga vibarua tiyari unataka awe philanthropist, kwani amekuwa George Soros.

Kutoa fungu la kumi, matoleo, kusaidia wahitaji inatosha sana
 
😁😁😁 noo mkuu gozba nishatoka nipo kahunda sasa hivi, gozba giza lilipofunga nilitoka. Maisha haya.
Tafuta wateja wa dagaa Dar uwaletee dagaa wa Bukoba wanauzika. Kuna mdada anapata profit zaidi ya mara mbili kila akituma mzigo. Kutapeliwa kupo, kupoteza kupo na ndio maana ya biashara. Kuhusu samaki sijui
 
Ndio maana nimekwambia ulikuwa unakimbia biashara mapema. Kama biashara ya kwanza imekufa na baada ya kufa ndio ukapata akili. Hata ya pili itakufa ndipo upate akili sababu huwezi pata maelezo yote ya biashara kabla hujaifanya.
Ungepata hela mara ya pili ukarudi kwenye biashara ileile uliyofeli mwanzo kama ni kweli ina faida ungepiga hatua.

Umedisco kusoma Logistics unaenda kuanza upya Marketing. Kwanini usiende kuanza upya Logistics kwingine angalau modules ushapitia na unajua ulikwama wapi.
Umeongea kitu cha maana sana. Kwa sasa nimeamua kukomaa na biashara moja hiyo hiyo sibadilishi kamwe nachezea za uso ila nakomaa nayo nimeshakata shauri kwamba ntafia kwenye hii hii biashara..!!!
 
Biashara maumivu sana sana sana.
Nakumbuka mwaka 2018, nilipata hasara 1.4M katika kilimo fulani .mwaka 2019 nkafanikiwa kutengeneza 10M+ Kweny biashara (sio kilimo) ,mwaka 2020 nilipata hasara 35M+ (kutoka kwenye biashara,kilimo na kutapeliwa MPK NKARUDI HOME KUANZA MAISHA UPYA) , mwaka 2021 nkafeli zaid katika kila jambo la kiuchumi niliofanya MPK nikawa naogopa kujaribu kufanya jambo lolote.

Ila mwaka 2022 Mungu akanikumbuka,NKARUDI katika form MPK sasa.

NB: 1) kama unahela na unataka ufanye biashara hakikisha unawekeza 25% pekee ya hela yako.na usiongezeee hata sh.kumi MPK ikue yenyewe iwe hata mara 3 ya mtaji ulioanza nao.

2) Epuka kuanza biashara kwa hela ya kukopa,biashara anza kwa hela yako. Na ikikua na kuwa na uhakika wa mapato,ndio unaweza kukopa ili kubust mtaji ikue kwa haraka( leverage).

3) Usichanganye Urafiki,undugu,ushikaji ,ujuaji(egoism) na malengo ya biashara yako

4)Usiitegemee faida au hela itakayopatikana Kweny biashara ikulishe,ikulipie kodi au ikusaidie kwa lolote ndan ya miezi 6 ya mwanzo wa biashara yako.


Binafsi haya ndio machache kati ya mengi niliyoyaona,yenye uwezo mkubwa kukurudisha nyuma sana hata kama ulishatoboa kimaisha.
 
Tatizo ugumu wa biashara hapa Bongo ni wizi , hasa wafanyakazi , ukitaka kuamini hilo anzisha biashara weka mfanyakazi ,yaani wabongo na wizi ni pete na kidole , ni lazima umbane sana hasa kwenye issues za mauzo na stock .
Yaani lazima akulize tu na kibaya zaidi wengi hawana hata aibu ,ukimuuliza atakwambia chuma ulete mara ushubwada gani sijui ,yaani Bongo kama huna muda wa kusimamia biashara yako ,hiyo pesa bora unywee pombe tu

Ndio ile kwenye biashara unakonda kama mgonjwa wa HIV /Aids wa miaka ya 80's wakati mfanyakazi mwizi anazidi kunona kama kitimoto ,
 
Back
Top Bottom