Needs vs wants. Ukifanya tathmini hio 3m au 4m uliyofikisha kutunza halafu ukatumia, utaona kwamba wala matumizi yake leo hii hayaonekani. Watu kinachowamaliza ni matumizi. Nilitoka Tz maskini hata buku ikawa inanipiga chenga, nikaenda USA nikaanza shika usd 5000 kwa mwezi... ambayo kwa exchange rate ya sasa hio ni zaidi ya tshs 10m. Nikawa nanunua suti za $1000 (Sean John), viatu ni jordans, nike, etc. Bling bling kibao. Magari nikawa nabadilisha kila mwaka (USA gari unalipia kwa mwezi kwa hio ni kama mkopo tu). Matanuzi kibao. USD5000 ikawa hata haitoshi kwa matumizi yangu kwa mwezi.
Kwa sasa nimemudu kuwa saver mzuri. Matumizi yasio na msingi sifanyi tena. Nguo sijanunua sijui miaka mingapi. Nanunua viatu tu mara moja moja. Nimeweza ku-save millions and millions and millions. Na nimejenga sana na nina rasilimamali kibao tena kwa hela binafsi na SIO YA MKOPO. PIA NDUGU SIKU HIZI NIMEWAFYEKELEA MBALI. Hakuna mnyonya damu mkubwa na mbaya kama ndugu ambaye hajapambana kama ww kimaisha ila anataka ale tu kwa mrija kupitia jasho lako.