Uliishawahi kuusikia uchawi au ushirikina huu?

Passion, mimi yalishanikuta nilipofaulu darasa la saba 1978. Tangu hapo nikaamini uchawi upo kwa asilimia 101. Yakikupata utaamini. Niligundua ili uwe na raha na huu ulimwengu ni lazima upate elimu kuhusu ulimwengu wa roho. Ogopa vitu visivyoonekana.
 
Mpaka anachukua nguo yako unayoipenda na kuirudisha, wewe unakuwa wapi??
Km unahisi hivyo kunywa mkojo wako wa asubuhi ila usiwe wa pombe.
Mchawi ndugu rafiki yangu, na nilikuwa siamini hizi mambo kwa sababu sifuatilii sana lakini anayekudhuru ni mtu wako wa karibu. Imagine unakuta ndugu yako wa damu anakufanyia hayo mambo utafikia kweli Kilele cha mafanikio? πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Huwa namshangaa sana mtu anaesema uchawi haupoπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Nina imani yanakuwa hayajamkuta.
Kuna kapumbavu fulani kanaitwa Kiranga kamerogwa ili kakane uchawi haupo wamekaaminisha hivyo ili waendelee kukaroga huku kakiendelea kuamini uchawi haupo.Sasa hivi wanataka kukala nyama kabisa
 
Mkuu katika pita pita yako umehai kutana na mafundi wa ukweli? Maana wengi hapa mjini matapeli sana, eti fundi anavaa cheni na ana account insta!
Waamini uchawi utawajua tu. 1. Kwao mganga kiboko ni yule anayevaa matambala na kukaa kwenye vijumba vya udongo au nyasi tena porini kabisa. 2. Kuna kipindi nilitembelea Kenya, nikakuta wanaamini waganga wakali wako Tanzania na washirikina wengi walikuwa wanavuka mpaka kuja kwa waganga wa Tanzania. Ukienda kwa upande wa Tanzania nako, watu wengi wanaamini waganga wakali wako Kenya, na watu wengi hupoteza fedha kwenda Kenya kufuata waganga. Sijui kwa nini hizi dhana zipo sana i.e mganga mzuri ni yule mwenye maisha ya kifukara, bibi mzee au babu mzee, anaishi sehemu za porini na yuko mbali na pale mteja anapokaa. NB: hakuna uchawi na nishaomba sana kama kuna mtu mwenye nyumba yenye majini au mizimi awasiliane na mimi niende nikalale huko. Au sehemu yoyote ya kukatisha yenye majini.
 
Omba sana yasikukute Mkuu.
 
Hakuna kitu kama hicho, ibada kwa sana na mambo yote tambarare, ushindwe mwenyewe kwa uvivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…