Uliishi maisha gani baada ya kupoteza Kazi au Biashara?

Hapo kwenye kukataliwa na madem aisee🤣🤣🤣😂😂 acha tu
 
Nyakati ngumu za kupoteza kazi ghafla zilikutana,na toka wakati huo,mpaka leo nsishi maisha ya kuunga kuunga,nikisikia mtu ana pesa,za kumtosheza maisha yake,na kuwapa na wengine,huwa nabaki kushangaa.Hali ni ngumu,haielezeki.
Pole sana ndugu
 
Mimi niko na ajira ila maisha yangu full soltepu.
Kuanzia kula, kuvaa, bili za kodi umeme maji.
Maisha magumu kinoma na hapa niko permanent and pensionable.
Wewe ni mwenzangu kabisa yani kama umeniongelea mimi
 
Pole sana kijana,JF ndio faraja na hongera kwa kulileta hilo hapa maana unaweza kufunguliwa fursa.

Tuko pamoja ila wewe naona una nafuu kabisa hivyo yangu nikieleza hapa utaangua na kicheko ila mwanaume ni kupambana haswa, hivi kibarua/kazi gani ulikuwa unaifanya rafiki?
 
Pole kwa uliyopitia mkuu,sisi ndo tupo kwenye haya mapito tunasonga
 

Nilikua nafanya kazi kiwandani mkuu
 
Mimi Nina swali,sio kwa ubaya.. huwa inatokana na Nini mtu anafanya kazi miaka mitano,but akipigwa chini miezi miwili tu analia njaa,

Hata akiba ya Kuanza biashara ndogo Huwa hakuna??hata Hela ya kula miezi sita wakati unajitafuta hakuna??

Changamoto inakuga Nini??
 
Ni kukaza mkanda. Mwaka wa nne huu mimi ni jobless mambo uliyoandika hapo ndio maisha yangu ya kawaida ya kila siku.

Sio tu kupoteza mpenzi utajikuta umepoteza hadi marafiki na ndugu zako wa karibu.
Kuna kipindi kilifika nilikuwa na wasiliana na maza tu kwenye simu.
 
Mshahara wa 300k 400k hata ukilipwa kwa miaka 10 ukija kusimamishwa mwaka tuu ni vilio na kusaga meno
Hii ni kwasabb mshahara huo ni ngumu mtu kuweka akiba hasa kama ana watu wanao mtegemea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…